Ukimsikiliza Kagame anavyozungumza hivi sasa, unaelewa kabisa huyu mtu anawajua majirani zake inside out kiasi ambacho hawawezi kumwambia chochote au kufanikiwa kumfanya chochote.
Ukimsikiliza Kagame vizuri utaelewa kuwa, kwa sasa anajua kabisa kuwa Tanzania ni Taifa ambalo limeshajifia kimfumo, kiasi ambacho mifumo yake inaingilika na iko wazi kutokana na kuendeshwa na siasa na Wanasiasa badala ya Wataalam na Utaalam.
Taifa lolote imara duniani linafanywa kuwa imara na uimara wa Taasisi zake kuu 4 ambazo ni Idara za Ujasusi wa Ndani na Nje, Mahakama, Jeshi la Ulinzi na Utumishi wa Umma.
Ukifuatilia mwenendo wa Tanzania kwa takribani miaka ishirini sasa utagundua kuwa, Taasisi hizi Kuu ambazo ndizo zingepaswa kulifanya Taifa letu liwe imara zimekuwa compromised na Chama cha Mapinduzi.
Taasisi hizi sizo zinazoamua mustakabali wa Taifa letu, Sera zake, Uchumi na Maendeleo yake bali zimedhibitiwa kabisa na Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachoamua mwenendo na Utendaji kazi wa Taasisi hizi.
Sio hivyo tu, kutokana na kuhodhiwa kwa Taasisi hizi, maamuzi na ushauri wa kitaalam wa Taasisi hizi kwa nchini Tanzania umekuwa ukiangalia maslahi mapana ya CCM ili kuhakikisha kinaendelea kuwa madarakani na kutawala hili Taifa badala ya kuangalia mustakabali mpana wa Taifa letu na Wananchi wake kwa miaka mingi ijayo. Hii ni kwa sababu uteuzi wa Viongozi wa Taasisi hizi umekuwa ukizingatia unyenyekevu wao kwa Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake ila sio umakini, weredi, uwezo wa kiakili na uwezo wa kiutendaji.
Ni bahati mbaya sana watu mbalimbali waliowahi kuonya kuhusu haya kwa kulazimisha mfumo wa nchi ubadilike kwa kuipatia Tanzania Katiba Mpya iliyo bora walikuwa wanadharauliwa sana na kuitwa majina mbalimbali ikiwemo kuwashawashwa na kuambiwa kila zama zina majira yake hivyo watulie tu.
Inaelezwa pia kuwa, kwenye Taasisi hizi, Viongozi walioonekana au wanaoonekana kufanya kazi kwa kuzingatia misingi na kusema ukweli bila hofu kwa vipindi tofauti wanaondolewa kwenye nafasi zao na kuwekwa wale wasiohoji na wanakubalina na kila kitu kwa Maslahi ya Chama cha Mapinduzi na Viongozi wake wala sio maslahi ya Taifa.
Kwa Tanzania ya leo sasa, Idara zake za Ujasusi ni kama zimekufa. Kwa maneno ya Kagame kuwa wanajeshi wake wanaweza kutembea kilomita 2000 kushambulia maeneo ambayo mnayatumia kutushambulia ilimaanisha kuwa mifumo yake ya Ujasusi kwa sasa inaweza kufika Dodoma kwenye Ofisi Kuu za Serikali au hata Dar es Salaam kwenye Ikulu kongwe zaidi na Taasisi zetu nyeti za kifedha na kushambulia.
Naionea huruma sana Tanzania.
Sasa tunavuna mavuno ya kuwaendekeza kwa muda mrefu Wanasiasa kuwa juu ya mifumo na Utaalam.
Rest In Peace Tanzania.