deepsea
JF-Expert Member
- Aug 10, 2013
- 3,287
- 944
Umenikumbusha stori ya Zamani, enzi za miaka: Ni hivi, nilikuwa na shangazi yangu dada ya Baba yangu alikuwa akiishi Kinondoni shamba, shangazi yangu alikuwa na mabinti wawili kati ya hao mabinti wawili mkubwa alikuwa mzuri kupita kiasi, yaani yule dada binamu alinifanya nisiache kwenda kwa shangazi kila mara, kwa kweli nilimpenda dada binamu, ila kuna kitu kimoja nilikuwa nakereka nacho, alikuwa anaringa sana, ilikuwa nikifika shangazi ananikaribisha vizuri sana na kuwaita wadada waongee na mimi! Yaani alikuwa kama hanijui vile.....!
Sasa hivi, ukimuona anatia huruma kama nini wajanja walimzalisha mapema ,hakupata mtu wa kuishi naye, shule hakuipenda, alijua ataolewa kwa uzuri aliokuwa nao.
Pole yake
