Ukitaka kupima akili za Watanzania (Typical African minds) angalia nyuzi zinazotrend hapa jukwaani

Ach
Ni wivu tu wa likes comments na trending ya uzi, kwakweli inauma sana mtu kuandika uzi wa kipuuzi kwa mujibu wako akapata page 50 kwa masaa kidogo tu wakati wewe unaandika madini na unaenda wiki hata page 5 hufiki,
Acha tumpe likes
 
Ni muhimu kuzingatia kile unachokihitaji zaidi katika ulimwengu wa mitandao ya kijamii, Kama dhamira yako ni kuelimisha watu basi fanya hivyo bila ya kuangalia response ya watu kwenye mada yako itakuwaje, jamii forums ina wageni wengi wanaosoma mada mbalimbali kuliko Members wake, Nyakati zimebadilika na hata watumiaji wengi wa hivi leo wengi wao ni vijana ambao damu zao zinachemka kwa kiasi kikubwa tarajia mada zao nyingi kuegemea upande wa mahusiano sababu ni moja ya eneo ambalo wanatumia muda wao mwingi kuishi kuliko mengine, yote ya yote tukubali nyakati zinabadailila
 

Watu nje ya hapa wanapitia magumu
Wakija humu wakakuta watu wanaomba ushauri wa maendeleo hasa kuhus biashara ndio utashangaa
Mtu ana laki tano anaomba ushauri afungue biashara ipi watu wengine wanamjibu njoo kidimbwi tudiscuss… plus a lot of negativity
Mifano ni mingi ila ndio uhalisia wa maisha yetu
Ukiwa na umaskini lazma karoho mbaya kawepo kwa waliofanikiwa pia
 
Inategemea tu, mbona hii inatrend sana?!!!! Kupitia uzi wako huu na kasi yake ya wachangiaji, you have another think coming!


Hata hivyo kuna ukweli ndani yake; tena kuna vidume vijinga humu kazi yao ni kujibebisha tu kwa kina joanah, kapeace &Co. Wakiona demu ameanzisha uzi mbio zenyewe za kuchangia si za nchi hii.
 
Sawa mkuu. Mimi sipingani na wewe ila nimeangalia mda mrefu kwanini mada zisizo make sense ndio zina wachangiaji wengi?

Ndio nikahitimisha kuwa wajinga ni wengi maana kama vitu visivyo make sense ndio vinapendwa basi wajinga ni wengi.

Hiyo ndio ilikua point yangu. Samahani kama nilikuwa too personal
 
I don't have another coming, mimi sio muanzishaji thread hovyo. I am too reserved.

Nachangia zaidi na hata hizo nyuzi za kijinga huwa nachangia lakini huwa najiuliza kwanini ujinga una mashabiki wengi sana?
 
Whowebe kumbe we ni genius, mbona ulikuwa hujanambia
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
JF ni kichaka, kuna makubwa humu ndani wacha kabisa
Tofauti yake na Tandale kwa Tumbo ni kwamba tuko nyuma ya keyboard tuu.
Lakin mi naona siku zinavyozidi kwenda tunaharibika sana siyo Jf tu hata Twitter miaka ya nyuma ilikua ni mtandao ambao huwezi kuanzisha mada za kipuuzi lakin sahiv imekua ni sehemu ya mada za ngono hata kufungua Twitter public unaogopa tena bora hata Facebook inayooneka ya watu wa ajabu lakin angalau wamestaarabika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…