Ukitazama CV ya Elimu ya Waziri Mkuu Majaliwa Kassim utaelewa kwanini ametoa wazo la wenye Degree kwenda VETA

Brain Kingdom

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
7,002
Reaction score
14,570
Ifahamike CV ya Elimu ya Kassim Majaliwa ni hovyo na ya kuunga unga tu kwahio sio ajabu kutoa wazo hilo kuhusu wahitimu wa shahada za vyuo vikuu kwenda VETA.

Kujadili ushauri wa kipuuzi na wa kijima, ni upunguani, huyu Waziri Mkuu amefika mwisho uwezo wake wa kufikiria na ni Waziri Mkuu pekee ambaye hajaacha legacy yoyote ile hadi sasa.

Hivi anajua wahitimu wa VETA hadi sasa ni wangapi na wako wapi na VETA ina fani za aina gani ni ziko ngapi.

Pia soma Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri

Anajua carrying capacity ya VETA? Anajua Ability ya VETA kwenye mawanda yote?

Tuzikatea dharau kwa nguvu zote, CCM tafadhari inapaswa kujiweka mbali na mawazo ya hovyo kama hayo ya Majaliwa.

Ni aibu kuwa na Taifa lenye kuokota okota watu kwenye nafasi nyeti kama ya Waziri Mkuu.

Hatupo tayari kulea matamko ya kifedhuri na yenye kutweza sifa za wahitimu wa shahada za vyuo vikuu.

Hii ni vita tusikubali dharau
 
Kwani misingi ya elimu inasemaje? Na mitaala ni nini? Waziri mkuu yuko sahihi na ametoa ushauri huo kwa wakati sahihi kwa mukhtadha wa wahitimu wengi kuzagaazagaa mitaani bila ajira huku wana shahada zao na umri unaenda hawajaajiriwa kutokana na nafasi za ajira kuwa chache. Kuliko mwenye degree akae tu mitaani bila ajira bnra aende VETA akapate ufundi. Soko la ufundi ni kubwa na halina mipaka. Sasa una degree fulani unasubiria nafasi ya ajira itokee na waombaji wako wengi si ujajikuta unazeekea mitaani bila ajira huku una degree fulani? VETA, LABOUR FORCE SKILLED, THE FUTURE OF TANZANIA
 
Kwa nini wasitengeneze nafasi za kuajiriwa by kuweka kikomo cha ubunge miaka mitano? Hapo sii tayari tunakuwa tumesaidi vijana kupata ajira kwa kupokezana kuingia hapo mjengoni kila mtu apate kiinua mgongo cha mil200.
 
20250317_041832.jpg
 
Waziri alikuwa na maana chanya tu tofauti na ulivomwelewa, VETA itakusaidia kupata kipato angalau cha kuendesha maisha ukiwa unasubiri ajira .
Afu kingine hajakulazimisheni kwenda ila alitoa ushauri na ni ushauri mzuri kwa vijana wote wenye akili timamu.
 
Hivi mbona kama watu mnakuza sana mambo?
Hivi mliosoma wa nchi hii mnajionaga namna gani? Mbona mnashindwa kuwa wasomi? Mi nahisi hii nchi ina Wahitimu sio wasomi! Ushauri mmoja tu una thread 700 utadhani alisema jambo la kutishia amani ya nchi huko duniani watu wana elimu ya ubobezi wa vitu vi3 tofauti ila hapa watu wakiambia wakaongeze na ujuzi wanaona kama wametupwa Gaza
 
Kwani misingi ya elimu inasemaje? Na mitaala ni nini? Waziri mkuu yuko sahihi na ametoa ushauri huo kwa wakati sahihi kwa mukhtadha wa wahitimu wengi kuzagaazagaa mitaani bila ajira huku wana shahada zao na umri unaenda hawajaajiriwa kutokana na nafasi za ajira kuwa chache. Kuliko mwenye degree akae tu mitaani bila ajira bnra aende VETA akapate ufundi. Soko la ufundi ni kubwa na halina mipaka. Sasa una degree fulani unasubiria nafasi ya ajira itokee na waombaji wako wengi si ujajikuta unazeekea mitaani bila ajira huku una degree fulani? VETA, LABOUR FORCE SKILLED, THE FUTURE OF TANZANIA
Kwenda VETA na kwenda Chuo Kikuu kuchukua Degree nini kilipaswa kutangulia?

Nadhani kama taifa tulishakosa focus siku nyingi sana. Nchi inaendeshwa kwa mihemko ya nani anatawala wakati huo. Miaka ya 2000 tulipata waziri anaitwa Mungai, aliondoa masomo karibu yote ya Michepuo kule Sekondari, akaunganisha Physics na Chemistry, huku Taifa, Serikali na wasomi wote wakimuangalia tu.

Mwaka 2006 Peter Msolwa akiwa waziri wa Sayansi na Elimu ya juu akaja na falsafa yake ya kuua ngazi ya kati ya elimu ya ufundi (FTC) na Advanced Dipoloma katika vyuo vya technical na vyuo vya kati vilivyoanzishwa ili kutoa elimu inaitwa Compitent based.

tukaja hapa kati kila Chuo cha Elimu ya Juu hadi SUA na Mzumbe vikalazimishwa kuanza kutoa degree za Elimu bila kufanya analysis ya kutosha kama kweli tunawahitaji hao walimu wote kwa idadi yao; leo tunawaambia waende VETA maana Serikali haiwezi kuwajiri wote.

Hii elimu ya VETA ilipaswa kuwa ya lazima mapema kabisa kabla mwanafunzi hajenda A-level au Chuo chochote cha kati. hii inesaidia hata mwanafunzi anapojiandaa kuendelea na ngazi ya juu ya elimu aweze kujiendeleza katika fani ya ujuzi wake.
 
Ifahamike CV ya Elimu ya Kassim Majaliwa ni hovyo na ya kuunga unga tu kwahio sio ajabu kutoa wazo hilo kuhusu wahitimu wa shahada za vyuo vikuu kwenda VETA.

Kujadili ushauri wa kipuuzi na wa kijima, ni upunguani, huyu Waziri Mkuu amefika mwisho uwezo wake wa kufikiria na ni Waziri Mkuu pekee ambaye hajaacha legacy yoyote ile hadi sasa.

Hivi anajua wahitimu wa VETA hadi sasa ni wangapi na wako wapi na VETA ina fani za aina gani ni ziko ngapi.

Pia soma Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri

Anajua carrying capacity ya VETA? Anajua Ability ya VETA kwenye mawanda yote?

Tuzikatea dharau kwa nguvu zote, CCM tafadhari inapaswa kujiweka mbali na mawazo ya hovyo kama hayo ya Majaliwa.

Ni aibu kuwa na Taifa lenye kuokota okota watu kwenye nafasi nyeti kama ya Waziri Mkuu.

Hatupo tayari kulea matamko ya kifedhuri na yenye kutweza sifa za wahitimu wa shahada za vyuo vikuu.

Hii ni vita tusikubali dharau
kuandika kwenyewe hujui,eti ufedhuri,kuna ubaya gani kwa mhitimu wa chuo kikuu kusoma veta?
 
Tatizo ni kwa vile aliyewaambia wasomi waende VETA ndiye huyo huyo wasomi walikuwa wanamsubiri awapatie ajira.

Uhalisia wa mambo huku mtaani ni kwamba kuna wenye degree kibao walishajiongeza mapema hata kabla ya hilo tamko.
Kuna waendesha boda, wajenzi, machinga n.k
Hawa wanajiingizia kipato bila kelele.
 
Ni aibu kuwa na Taifa lenye kuokota okota watu kwenye nafasi nyeti kama ya Waziri Mkuu.
Umezunguka sana, wewe sema alikuwa mwalimu.Nakukumbusha tena baba wa taifa hili alikuwa mwalimu! Aliyemfuata naye alikuwa.............Magufuli naye alikuwa....................

Jifunze kujenga hoja na upunguze mhemko! Dunia ya leo bado unalingia shahada???????
 
Ndo maana nchi imekwama kusonga mbele pamoja na rasilimali lukuki maana maticha ticha wamekuwa wengi kwenye nafasi nyeti za juu.
 
Kwa nini wasitengeneze nafasi za kuajiriwa by kuweka kikomo cha ubunge miaka mitano? Hapo sii tayari tunakuwa tumesaidi vijana kupata ajira kwa kupokezana kuingia hapo mjengoni kila mtu apate kiinua mgongo cha mil200.
wameishapunguza mihula ya kukaa bungeni
 
Unaweza kuhitimu degree na ukarudi veta kujifunza fani tofauti na shahada yako na sio lazima, hii inakuja pale unapohitaji utaalamu mwengine juu ya fani flani na endapo utaalamu huo inapatikana veta. Tunaweza kufikiri kwa kutumia ubongo na si vidole vyetu.
 
Back
Top Bottom