KERO Ukiukwaji wa Haki za wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Risk ndio kama hiyo kutafuta huruma huku mitandaoni ...Haukatazwi ila chuo wahadhiri wana nguvu kuliko kitu chochote .
 
Ukiwa mkweli Sana, uliyenyooka ktk mambo yako, mpinga wizi, rushwa, ufisadi, dhuluma au mpigania haki, basi tambua ya kwamba Afrika siyo mahali salama pa kuishi.
 
Na naona umeleta fullname yako mpaka taarifa zako zote binafsi, dogo mjanja sana! Unajitafutia Fame, pande na connection zako mapema.

Angalia usije kuishia kubaya kama Abdul nondo
Apigwe BAN haturuhusu majina halisi hapa jukwaani
 
Huyo Boaz malizana nae nje ya maeneo ya chuo. Mwambie ukiendelea kunitisha hivi, mimi chuo nitaacha na wewe huu ndo utakuwa mwaka wako wa mwisho kuitwa Mussa Boaz. Usiongeze neno wala usipunguze. Alafu endelea na mishe zako.
 
PS 223 ulipata Supp.
Hivi kweli International Relations II ni ya kupata Supp.
Wewe ni kilaza.
Kuwa kilaza ni jambo lingine na kutishiwa ni jambo lingine. Nyie ma ticha wa UDSM kuna siku mtakuja kuwa mandondocha nawaambia. Bado hamjakutana na akili mbovu.
 
Moses boaz ataona umemchafua hapo. Jiandae na chuki zaidi ya alizokuonyesha ! Nakumbuka wakati nipo chuo mwaka wa kwanza kuna somo nilipata marks kidogo nikaenda kwa lecturer alinijibu kunya sana .nanukuu ' wewe bado mdogo utarudia tu mwakani kwani shida nini' ili niuma sana mana sikustahili kupata zile marks ndogo kiasi cha kupitwa na vilaza.
 
Future yako ushaanza kuiharibu kwakuchagua hayo masomo now baada utetee ugali wako unajichanga nya nasafari yawengine..
Jitafakari..
Kila mtu ana safari zake mzee, hatuwezi wote kufanana. Kama moyo wake unamtuma kufanya harakati za kutetea watu, afanye anachokipenda.
 
Kila mtu ana safari zake mzee, hatuwezi wote kufanana. Kama moyo wake unamtuma kufanya harakati za kutetea watu, afanye anachokipenda.
Kuna muda lazima ujitafakari ukifuata moyo kwakila jambo nakuacha viungo vingine hilo nitatizo
 
Baadhi ya vyuo hizo commitment form bado zipo na zinasaidia mno wale wanaotegemea boom kulipa ada.

Hiyo ya Udsm sijui imekuaje hawana hiyo kitu aisee. Boom kuchelewa ni kawaida, vyuo janja vikajilinda kwa style hiyo.
Commitment paper ilisaidia na still ingewasidia wanafunzi wakimaskini kuweza kutumia boom kujilipia Ada zao..
 
Pole sana kamanda.Mimi NAKUSHAURI , KAMA ULIVYOELEZA HAPA ANDIKA BARUA KWA DEAN OF FACULTY ELEZEA SCENARIO YOTE PIA AMBATANISHA NA PRESENTATION YA SEMINA NA PIA TOA ANGALIZO LA MBELENI KUWA HUYO MSIMAMIZI BOAZ AMEKUTISHIA NA HUNA IMANI NAE.KATIKA HIYO BARUA PIA TOA NAKALA KWA MAKAMU MKUU WA CHUO NA DEAN OF STUDENTS KWA TAARIFA NA PIA NAKALA KWA CHAMA CHA WANAFUNZI THEN ENDELEA NA MASOMO.HIYO ITAKUSAIDIA HUKO MBELENI IWAPO HUYO BOAZ ATAKU VICTIMIZE KWA NAMNA YOYOTE ILE ITAKUWA RAHISI KWAKO KU REFFER HIYO BARUA ULIYOPELEKA.PIA MJULISHE LECTERER WA HIYO KOZI PROF MALLYA NAE MPE NAKALA YA BARUA
 
Kwani Mnyika na Huyo Nondo wana hasara gani pamoja na kutomaliza chuo? Waliomaliza chuo hao wana nin ambacho Nondo na Mnyika hawana? Hatima ya maisha ya mtu ipo mikononi mwa Mungu tu.
ndio nmemwambia mwamba vita alioingia awe anamaanisha John Mnyika alikua anajua nin kitamtokea na hakurud nyuma hata baada ya vitisho na kufukuzwa chuo
kanondo hakakurudi nyuma hata baada ya kutekwa nyara kusitishiwa usajari wake wa chuo
huyu mwamba wetu anatakiwa ajue hilo kwamba akifukuzwa shule aendelee kukaza na anachokipigania kitamtoa kama hao ndio naana sijamtajia waliofukizwa vyuoni sababu ya harakati na saiv wanaokota makopo mtaani na hao ndio wengi sasa
 
Hhah hivi unajua kama watu wajamii moja ubebana
 
Dawa ya wasiolipa school fees sio kuwazuia kuingia darasani, kama wameanza semister acha wasome wamalize ila usiwape majibu ya final mpaka wamelipa school fees, itapunguza matatizo kila upande
Tumia akili.
Chuo kinategemea ada za wanafunzi kuendesha pilika za kila siku.

Kwahiyo mwaka mzima wanafunzi wasome bure, running costs za chuo zitoke wapi? Wakope bank?
 
Pole! Tz ni chuki, visasi na kukomoana, ambapi hujui chanzo ni nini. Mwenye nafasi fulani, haitumii kwa ustawi wa jamii bali kuididimiza. Nchi kamwe haitaendelea!
Tukiongelea haki za wanafunzi, inakuwa aje mpaka siku za mapumziko za mwisho wa wiki mnatakiwa kwenda na wakati mwingine kufanya mitihani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…