KERO Ukiukwaji wa Haki za wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

KERO Ukiukwaji wa Haki za wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kijana nakushauri usiingize siasa kwenye taaluma. Utaumia wewe pamoja na kuwaumiza wazazi wako.

Fuata taratibu za malalamiko zilizopo chuoni. Njia uliyotumia kukimbilia hapa jukwaani haikubaliki. Umeruka ngazi nyingi sana mpaka unakuja kwenye public.

Fuata taratibu za chuo. Elimu ni pamoja na nidhamu. Fuata kilichokupeleka chuoni uanahatakati utaukuta mtaani. Heshimu Heshima ya taasisi iliyojiwekea kwa miaka mingi. Makosa hayakosekani kwenye taasis yoyote duniani lakini jambo la msingi ni kufuata taratibu sahihi
 
Tumia akili.
Chuo kinategemea ada za wanafunzi kuendesha pilika za kila siku.

Kwahiyo mwaka mzima wanafunzi wasome bure, running costs za chuo zitoke wapi? Wakope bank?
Utakuwa na chance kubwa ya kulipwa kama mwanafunzi anajua akilipa atapata matokeo yake na kuendelea na shule kuliko kumfukuza mwanafunzi katikati ya semister, na kama unategemea school fees kulipa mishahara ya mwezi unaokuja au miezi mitatu funga tuu sio chuo hicho
 
Kazi ya chuo kusomesha waliolipa ada

Mambo ya ada ya Bodi ya mikopo na wazazi huko ukereketwa wake apeleke Bodi ya mikopo na Kwa wazazi au wadhamimi walipa ada

Analeta taharuki isiyo na kichwa Wala miguu chuoni Hana akili mjinga huyo hata Ingekuwa Mimi ningempa zero
Kwa Kozi Anayosoma alitakiwa ajue kuwa chuo hakihusiki na ada Wala boom.Mayowe yake Chuoni Sio mahali pake
 
Mbona kama unajipigia promo asee. Acha wenge soma we dogo. Acha kabisa ujinga wa kujiona tayari wewe ni Zito Kabwe au Lissu.

Upo University aisee, hakuna njia rahisi kumaliza degree. Pambana Acha kulia lia

Maelezo yako hayana uzito kwamba umeonewa. Soma, acha kutafuta huruma haupo sekondari hapo.

We bure kabisa, yaani unam challenge seminar leader Jamii Forums ili kupata attention? Acha ujinga dogo uta disco kweli!
KAma kulikua na shida angemfata huyo Prof. Mallya (course instructor).
 
Habari,

Naitwa Abdul-Aziz Ally Carter, Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) nasomea Historia na sayansi ya siasa, namba yangu ya usajili 2021-04-01016

Siku za karibuni nimekuwa active katika harakati za chuo hasa kupigania maslahi ya wanafunzi waliozuiliwa kuingia katika mitihani kwa kushindwa kulipia Ada na kucheleweshwa kwa malipo ya Boom.

Toka niwe active katika harakati hasa kipindi hiki, Maisha yangu yamekuwa magumu kitaaluma hasa katika Uwasilishaji (semina),

Katika semina ya leo, ya kozi ya "Public administration in Tanzania" yenye kozi code PS 341, Siku ya Jumanne Saa 8:00 mpaka 9:00 , inayofanyika Venue ya SR 5 na kusimamiwa na Kiongozi wa semina ( Seminar leader) aitwaye Moses Boaz,

Course instructor wa semina hii ni Prof E.Mallya, Ofisi yake ni namba 802 Jengo la COSS Tower.

Katika Uwasilishaji (presentation) ambapo kikundi cha watu watano (5) walifanya Uwasilishaji na Mimi nikiwemo,

Kiongozi wa semina ( Moses Boaz) alisema nimekosea kutoa maana ya msamiati uitwao " Politicization"
UTATA;

Kwanza, maana ya msamiati huo niliutoa kwenye vyanzo vya vinavyoaminika vilivyopo kwenye course outline iliyotolewa mwanzo wa semister,

Pili; Kiongozi wa semina ana wajibu wa kumrekebisha/ kumsahihisha mwanafunzi pale anapokosea katika semina kwa lengo la kumsaidia na kumjengea uwezo,

Tatu; Katika kikundi cha Uwasilishaji cha watu watano ( 5) ambacho kimekutana, Kikajadiliana na kukubaliana maudhui ya Uwasilishaji, ni mtu mmoja tu aliyekoselewa kwa vitisho ambaye ni Mimi ( Abdul-Aziz Ally Carter),

VITISHO;

Kwanza; Kiongozi wa semina alitaka Mimi pekee yangu kati ya watu watano (5) Kulihama grupu hilo na kuamia grupu lingine kwa lazima,

Pili, Kiongozi wa semina alisema atanipatia "zero" kwenye kazi ya alama kumi (10),

Tatu, Kiongozi wa semina amesema nisipojiangalia nita rudia kozi mwakani (carryover),

Kiongozi wa Semina ( Moses Boaz) alianza kuzitoa Kauli na lugha kali kama hizi juu yangu katika semina ya wiki iliyopita tukijianda kuhudhuria muadhara wa Uprofesa.

USHAHIDI:

Kauli hii kaitoa kwenye chumba cha semina kikiwa na wanafunzi wote wa semina hiyo,

Wanafunzi ni mashahidi.

MTAZAMO WANGU;

Kauli na Vitisho vya namna hii vimeanza baada ya harakati za kuwapigania wanafunzi waliozuiliwa kufanya mitihani kwa sababu ya kukosa Ada,

Kiongozi wa semina, Alihusisha maswali yangu ya kutaka kujua sababu za kauli alizotoa na harakati zangu kuanzia wiki mbili nyuma.

Kiongozi wa semina alizungumza kwa Hasira na Jazba, katika mazingira ambayo Jazba na Hasira haikupaswa kutumika,

Kwa mazingira hayo, nahitimisha kwamba sababu ya kilichotokea kati yangu na msimamizi wa semina (Moses Boaz) ni Harakati na siyo makosa ya Uwasilishaji.

WITO;

Wito wangu, Naomba mamlaka zinazohusika, Ukiwemo Uongozi wa chuo, Wizara ya Elimu kufanya uchunguzi dhidi ya swala hili,

Ili niweze kusoma kwa Amani na Utulivu kwa kipindi chote nitakachokuwa chuoni.

Ahsante.
Tafsiri yako ni kwamba chuo ambacho ulikishutumu awali kimemtuma seminar leader kukushughulikia? Umeenda kwa prof kutafuta msaada ukakosa? Unaomba uongozi wa Chuo huku? Kwani haujui taratibu za kutatua changamoto za ndani ya taasisi?. Umeambiwa uhame kundi sababu haujawasilisha vizuri kwa nini usiwasilishe upya?. Unaleta hoja za kitoto sana. Hapo seminar leader ana kosa gani? Sio vitisho ndio ukweli kwamba usipopresent tena una carry. Sasa leta usela mavi wako.
 
Back
Top Bottom