KERO Ukiukwaji wa Haki za wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kijana nakushauri usiingize siasa kwenye taaluma. Utaumia wewe pamoja na kuwaumiza wazazi wako.

Fuata taratibu za malalamiko zilizopo chuoni. Njia uliyotumia kukimbilia hapa jukwaani haikubaliki. Umeruka ngazi nyingi sana mpaka unakuja kwenye public.

Fuata taratibu za chuo. Elimu ni pamoja na nidhamu. Fuata kilichokupeleka chuoni uanahatakati utaukuta mtaani. Heshimu Heshima ya taasisi iliyojiwekea kwa miaka mingi. Makosa hayakosekani kwenye taasis yoyote duniani lakini jambo la msingi ni kufuata taratibu sahihi
 
Tumia akili.
Chuo kinategemea ada za wanafunzi kuendesha pilika za kila siku.

Kwahiyo mwaka mzima wanafunzi wasome bure, running costs za chuo zitoke wapi? Wakope bank?
Utakuwa na chance kubwa ya kulipwa kama mwanafunzi anajua akilipa atapata matokeo yake na kuendelea na shule kuliko kumfukuza mwanafunzi katikati ya semister, na kama unategemea school fees kulipa mishahara ya mwezi unaokuja au miezi mitatu funga tuu sio chuo hicho
 
Kazi ya chuo kusomesha waliolipa ada

Mambo ya ada ya Bodi ya mikopo na wazazi huko ukereketwa wake apeleke Bodi ya mikopo na Kwa wazazi au wadhamimi walipa ada

Analeta taharuki isiyo na kichwa Wala miguu chuoni Hana akili mjinga huyo hata Ingekuwa Mimi ningempa zero
Kwa Kozi Anayosoma alitakiwa ajue kuwa chuo hakihusiki na ada Wala boom.Mayowe yake Chuoni Sio mahali pake
 
KAma kulikua na shida angemfata huyo Prof. Mallya (course instructor).
 
Tafsiri yako ni kwamba chuo ambacho ulikishutumu awali kimemtuma seminar leader kukushughulikia? Umeenda kwa prof kutafuta msaada ukakosa? Unaomba uongozi wa Chuo huku? Kwani haujui taratibu za kutatua changamoto za ndani ya taasisi?. Umeambiwa uhame kundi sababu haujawasilisha vizuri kwa nini usiwasilishe upya?. Unaleta hoja za kitoto sana. Hapo seminar leader ana kosa gani? Sio vitisho ndio ukweli kwamba usipopresent tena una carry. Sasa leta usela mavi wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…