Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Vice versa is true
 
Nafungua Uzi kwa kusema Dar es salaam ni mkoa kama mikoa mingine, nashangaa mnavyoikuza kanakwamba ni paradiso kiasi cha kusema kuna Dar na mikoani.
Huo msemo wa Dar na mikoani naomba muufute kwa maana Dar ni mkoa.
 
Sasa ww huna mtaji na mambo yenyewe unayaona yalivyo kwanini usizame mikoani ukalime Mihogo upate mtaji uludi dar ufanye kazi halali sio kukaba kaba Asilimia 70 ya wakazi wa DAR wanaishi kijanja janja tu hawana Cha kufanya na lait kama magu angekuwepo ujanja ujanja ulikuwa unawatokea puani WEWE NUNUA SIMU YA LAKI 8 Mimi laki. Nane nikinunua mbuzi 16 kwa mwaka wanazaa mara mbili nakuwa 32 halafu watoto nawo wanazaa safi huku mambo mengine yanaenda lakin sio mbaya
 
Hizi akili zenu za kwenye makaratasi zingekuwa sahihi wote mnaoikashifu Daslam mngekuwa mabilionea.

Hayo magazijuto unayopiga hapo ukiwa na njaa wenzako wengi tu waliyapiga na mpaka kesho wapo apeche alolo.Bwanamdogo Daslam ni mji wa kipekee kama ukishindwa kuishi Dar wewe utakuwa kiazi mbatata wa mwisho na hutaweza kuishi hata huko mikoani.

Huyo unayemsema alikuwa anakomesha mission town yeye mbona alikimbia chaki akaenda kwenye vieteee😂😂😂 kijana acha stori za pauka pakawa my friend usione mtu anaitwa tajiri ukazani anauza upuuzi upuuzi sijiu mikate na karanga.

Hapa duniani unatakiwa uwork smart not harder.Hard workers wote ni slaves na hawatatoka huko mpaka mwisho wa dunia.

Hela inafata mkondo hela haitaki kelele.Kaa vizuri na anza kusalimia watu utakula mema ya nchi.
 
Nafungua Uzi kwa kusema Dar es salaam ni mkoa kama mikoa mingine, nashangaa mnavyoikuza kanakwamba ni paradiso kiasi cha kusema kuna Dar na mikoani.
Huo msemo wa Dar na mikoani naomba muufute kwa maana Dar ni mkoa.
Jiji Tanzania ni moja tu Dar kwingine kote ni mikoani
 
Maisha yapo hivi,

Kwa mfano mtu asiye na Ajira anaamua kutokuja Dar, yaani jiji linakuwa na walioajiriwa tu

Nani atachimba shimo la taka,

Nani ataangusha miti,

Nani atafyeka kiwanja chako,

Nani huyo wa kuzibua vyoo vikijaa,

Nani huyo msomi aliyeajiriwa akuoshee passo yako,

Nani atatumwa kazi ili alipwe 5000 hadi 3000.

Nani atatembeza vitu unavyonunua ukiwa kwenye foleni.

Mungu anajua ndiyo maana hao uliowataja wapo mkoani na wengine wapo Dar na umasikini wao
 
Sasa hayo maisha mbona hawayapati..wanaishi kama wanyama. Mtu anakimbizana na magari kwenye jua kali kwenye barabara anauza maji au karanga ni mateso
Mtu anayekuja Dar es Salaam usiku na kuondoka mchana ni ngumu sana kuona kuwa Dar kuna fursa na Changamoto.Dar wako wanaoishi peponi na wanaopata shida.Ukienda mbeya hivyo hivyo,Morogoro hivyo hivyo,Arusha hivyo hivyo tena pale vijana wako loose loose.Kikubwa tafuta pesa usaidie wengine kwenye jamii yako usijikite kujilinganisha na rafiki yako anayeishi Dar.
 
Umeongea pumba
 
sio rahisi hivyo kama unavyodhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…