Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Anamaanisha badilisha mtazamo wako. Yafukiri maisha kwa ubongo mpana zaidi. Badilisha namna unavyowawazia wengine.

Kuna watu wanadhani kuishi kijijini au mkoani basi wwni mtu uliyefeli maisha au huna vha kufanya na huna ujualo.
Umeelewa vizuri sana Uzi wangu.👏👏
 
Sio lazima uwe na Mishe,wengne ni wazawa washazoea maisha ya Daslam,mioyo yao hujaa Amani wakiwa DSM,Nna rafiki zangu wawili walipata kazi (gvt) mikoani hawakwenda,kupanga ni kuchagua,linda amani ya nafsi yako,maisha ni yako,ishi vile roho yako inataka...
Sahihi
 
Watu wa Daslam wameyapatia sana maisha kwenye kujua Aziz Ki jana alipikiwa nini na yule mwanamke aliemuoa juzi (jina lake nimelisahau)

Wameyapatia sana maisha kujua Diamond atamuoa zuchu au anamchezea.

Wanajua sana maisha kuwa mechi ijayo ya Simba na Yanga refa gani asichezeshe hiyo mechi maana kahongwa.

Wanajua sana wasafi Media ni ya Diamond au siyo, Crown Media ni ya kiba au siyo

Wewe wa mkoani unajua nini bana?
Hahaa.....Na kubet wanaongoza

Milo yao sasa Mihogo kila asubuhi
 
Yaani Haya Maisha Bwna.

Yanaweza kuwa yamekupiga Chenga ila bado ukawa unaamini umeyapata.

Hasa hasa kama una ishi Dar kuna kaimani kanakujia kichwani kwamba huko Mbeya hakuna kitu, kuna kasumba inakupumbaza kichwani kwamba huko Mtwara kumejaa maskini tu na hakuna hela. Yaani Kichwa kinajaa na kuvimba kabisa kwamba wanaoishi Singida au Nzega Tabora ni watu wenye hali duni.

Tena kuna kitu kinakujaa kabisa unaamini watu wa Tanga wanakula bata gani bwana? Kuna nini cha ajabu Tanga? Kwanza kule Rami yenyewe ya magumashi.

Kumbe Hapo Dar ulicho nacho ni Geto la Chumba Master, Sebule na Jiko, TV ya Nchi 50, Saboofa la Aborder na Mademu kama wawili hivi wa kubadilisha badilisha na wanakugombania.

Huku Mkoani Nachingwea, Dumila, Handeni na Rufiji Vijana wana miliki Mamilioni ya Fedha na Miradi kadhaa isiyohamishika yenye thamani mpaka 200M.

We mali zako hazifiki hata 10M na hilo Duka lako la Mpesa, Tigopesa, halopesa etc.

Huku watu wanakula Bata si la Nchi hii. Wana Majumba mazuri, watoto wa kwenda.

Magari ya kufa mtu ya kifahari hata kama hayafiki 50M lakini hizi za 15M, 18M, 20-25M hadi 45M zipo za kumwaga.

Wewe unajidai mademu wawili wamejaa Enjoface na Macream huku watu wanapiga hadi 8 Kuku wa Kienyeji.

Kwenye Biashara ndio usiseme. Mshindo mmoja tu unatoboa maisha.
Mi naishi Jijini Mwanza, ila watu wa mikoani tunapenda sana kuijiliwaza. Tutafute pesa tule maisha. Mambo ya kuwasemasema vibaya watu wa Dar tuache! Mwisho wa siku, Dar ndio kila kitu Tanzania hii!!
 
So Kwamba wenye hela hawapo, wapo ila asimilia kubwa ya watu wa hili jiji wana life la kuunga unga, na vijana wakitoka huko peripheral kuja uku hukutana na kitu ambacho ni tofauti na walichosikia, lengo la kuanzisha nyuzi adimu kama hizi ni kutoa elimu
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom