Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Mzee Bongo Zozo kashavuta yake na anapeta mtaani hebu watu tuchukue mamuzi.magu tuhudumiane wenyewe,ziletwe gari zipigwe bei tusisubiri wapika pilau la clean energy waje kutusaidia hili jambo.I swear the problem isn't over yet.
 
Mie nilikuwa na mix, kuna sehemu maeneo ya Tanga nilikutana na Mvua.. so nikashuka mpk 60-70kph pia gari ipo chini sana hivyo kuna sehemu natembea na 80-90 (Just in case).

Kuna kipande cha kuitafuta Makanya hapo katikati ndio nilitembea 150-170kph mpk unaskia harufu ya petrol iliyochemshwa..😌

Ni kweli, ukanyagaji unachangia mafuta kupungua kwa kasi. Maana unavuta mafuta then breki unavuta tena breki..

Natumia Manual, so Rpm nilikuwa nacheza na 2.5k -3k natia gia. Nikiboost nabadiri gia nikiwa ktk high Rpm 7-8-9k.. (Redline shifts).
 
Wachache watazimiliki tesla kwa sababu pia ya gharama za matengenezo. Tesla kama iPhone anajaribu kukaba kila kona kuanzia matengenezo hadi vipuri akuuzie yeye mwenyewe.
Sasa kimbembe betri lizingue, bei yake ni sasa na nusu ya gari jipya.
Labda wachina waokoe jahazi. Mafundi wetu wa ilala warudi shule wajiandae na mabadiliko.
 
Upo Sahihi kabisaa mkuu...Sisi tunasubiri used tutakoma kwenye kubadilisha battery
 

Uko vizuri na uzoefu wa kutosha Mkuu, hongera.

Kuna kipande cha Mwanga barabara sio rafiki sana.
Mie sio mtu wa masafa uzoefu Mdogo sana, gari ikifika 200 sisikii harufu ya petrol ila nasikia jasho langu japo sitoki jasho na nimepaka deodorant.

Faida nyingine niliyonayo sihofii traffic...
 
Halafu services yake ni nzuri sana si gharama wala ya mara kwa mara.
 
Obviously ww ni poti
 
Kwa kuanza, wangejaribu ata kupunguza kwa miaka kadhaa.

Ila huu ushirikiano ulipo kati ya TZ na CN maybe unaweza fanya mapinduzi.

Sijui kwanini ushuru wa kuingia magari unakua juu sana.
Tusubirie mapitio ya ushuru kama yataangazia hili eneo la magari tupate unafuu.

Shida ipo kwetu hata sio huko yanapotoka au kutengenezwa, tuna sera mbovu sana za Kodi.
 
Unataka kuniambia charging process ni 100% efficient?

Unahitaji umeme 1kWh kujaza battery 1kWh?
Hapo nafikiri Kuna vigezo na masharti havijazingatiwa. Kuna suala la matumizi na kuanza kuchoka pia, battery zitapunguza ufanisi kutokana na muda zilizotumika. Niliona mahali zinatakiwa zibadilishwe ndani ya miaka 10 au umbali wa 100,000 km.

Na pia najaribu kuwaza charging Kwa nyumbani na kwenye charging station, units ni zile zile tofauti ni muda tu?

Nnavyoelewa charging station ni kama fast charger ya simu, unaweza muda mfupi battery imejaa.
 

Mchina anatengeneza EV za hatari. Kwa Sasa magari yake yamekua tishio US. Ameingia makubaliano na Volvo kutengenezwa EV ikijumuisha Hybrid. Wale jamaa watatuokoa sana.
 
Unataka kuniambia charging process ni 100% efficient?

Unahitaji umeme 1kWh kujaza battery 1kWh?
Direct Current Super Charger (Level III) zina efficiency ya 99-100% wakati za nyumbani Level I zina efficiency ya 90 na Level II zina efficiency ya 95 kwenda juu. Zote tested under extreme condition.
 
mkuu sisi wauzaji wa oil/lubricants na filter tutakufa njaa hizo gari zikiteka soko la Tz.

Hapana Mkuu, hizo EV kutrka soko itachukua muda sana. Ila ni vizuri kuanza kuangalia zinahutaji vitu gani vidogo vidogo na matengenezo yake yakoje.

Baadhi ya nchi za Ulaya wameweka ukomo ifikapo 2030 magari yote yawe ya kutumia umeme. Huku kwetu bado sana kiongozi.

Ila na nyie kwanini baadhi yenu wanatupiga na oil fake?
 
Sasa kilometa 400,000 ni leo? Mimi nimenunua gari 2017 na ninaitumia kila siku kwa mizunguko yangu ya mjini. Niliinunua na km 67,000 leo iko 138,000.

Kilometa 400,000 ni miaka angalau 10 - 15 kwa matumizi ya kawaida.
Tena ayo sio ya kawaida. Ni makubwa. Kilometa 100k tu ni nyigi kinoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…