Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Kwa kuanza, wangejaribu ata kupunguza kwa miaka kadhaa.

Ila huu ushirikiano ulipo kati ya TZ na CN maybe unaweza fanya

Kwa Tanzania ni suala la muda tu, tutegemee wachina kuanzisha kiwanda cha magari ya umeme cause malighafi tegemezi ya betri yaani graphite ynapatikana wilayani Rungwa, Lindi, na uchimbaji Karibuni utaanza
 
Itabidi kuja na fundi wako
 
kila kona ya dar naona ujenzi wa vituo vya mafuta ya diesel and petrol. najiuliza kwa nn hawa matajiri wasijenge hata vituo vya kujazia gesi kwny magari yanayotumia gas (CNG)? pale Temeke na ukonga kuna folen ndefu sana ya magari & bajaj znazoenda kujaza gas, najiuliza hv matajiri hawaoni kama hii ni fursa?
 
Kwa Tanzania ni suala la muda tu, tutegemee wachina kuanzisha kiwanda cha magari ya umeme cause malighafi tegemezi ya betri yaani graphite ynapatikana wilayani Rungwa, Lindi, na uchimbaji Karibuni utaanza
Ikitokea gari zimefika, charging stations zitakuja tu.
 
Ikitokea gari zimefika, charging stations zitakuja tu.
kwani lazima charging stations lazima ziletwe na serikali? vp mtu akinunua mfano ww au mimi nimenunua EV nikaleta na power station yake naifunga nyumbani kwangu natumia mwenyewe au mjini kwa ajili ya biashara yeyote mwenye EV yake alete vp inaruhusiwa au mpaka uwe na kibali maalum.? na hizo power zinauzwa shiling ngapi kwa level tofauti.
 
Swali la msingi sana.

Charging stations zipo za level kweli na wameziweka kwenye level 3, yaani level 1, 2 na 3 ambazo zinachotofautiana ni umeme (current).

Level 1
Hii ipo slow, kwa wastani inaweza kuongeza kama kilometa 6 hivi ya range kwa saa 1 utakalochaji.
Mara nyingi zinakua installed majumbani na nzuri kwa kuchaji overnight unavyolala.
Hii sio lazima iwe charging station, inaweza kua ata umeme wa nyumbani unaotumia kuwasha TV na friji ukatoa tu waya nje ukachaji chuma.


Level 2
Hii ipo katikati kwa wastani unapata kilometa 30 hivi za range ukichaji kwa saa 1.
Hii pia inaweza kua installed nyumbani au kazini, pia baadhi ya public charging stations.


Level 3
Hii ndio fastest inaweza kuongeza hadi kilometa 30 kwa kila dakika unayochaji. Mara nyingi chini ya saa 1 unakuta uamechaji gari from 0 to 100%!

Hii sometimes inaitwa DC Fast Charging u akuta baadhi ya watu wameimprove inaitwa Super Charger na utaikuta mara nyingi katika public stations mfano ikawekwa Mlimani City ukishuka unaweka chaji we unaingia supermarket ndani ya 30 minutes utazofanya shopping unakuta gari imejaa from 30 to 90% mfano.

Sasa tukaja kwenye maswali yako, Yes mtu anaweza akainstall izo charging stations yoyote nyumbani kwake au ofisini au popote kwa matumizi binafsi au biashara, yaani assume kama tu kituo cha mafuta.

Majumbani wengi wana level I kwasababu inatumia voltage za majumbani 120V so hauitaji ufundi mwingi.

Kuhusu gharama:
Mara nyingi ukinunua EV unapewa chaja (mobile chaja). Yaani kama umenunua simu mpya tu.
Mfano Tesla, unakuta hii mobile chaja.


Ambayo sio gharama sana ni kama $600 kama unavyoona. Na zipo alternative, yani Kama unavyotumia iPhone lakini chaja ukatumia Oraimo au kichwa cha Tecno.

Kwahiyo kuhusu bei za chaja unless ununue tu kama umepoteza maana vichwa vinafanana kama simu.

Mfano simu zina Type C, type B sijui na zile za iPhone basi na EV zina connector za aina mbalimbali kutegemea na region na DC au AC (ila lazima ziwe mbili za AC na DC)

Usiogope pia kwasababu gari lako litakua na port mbili kama hivi:


Sasa utajiuliza tena vipi kama charger yangu itakuja tofauti na port za gari langu, usijali kuna adapter pia:


Kwahiyo kaka sijaona sababu ya kutonunua EV achana na PureviwZeiss uyo Mjapan hapendi Wachina.

Kwahiyo mtu unaweza nunua yako home ukawa unatumia umeme wako ghetto.

PS: Kuchaji kwenye public stations sio bure unalipia, na point ya kununua EV ni home charging, kama lengo kusave hela. Ukiwa unachaji kila siku kwenye public bora ubaki na ICE.

Research walizofanya wenzetu, wameona kuchajia kwenye public ni expensive 15-20 times more kulikoa kuchajia home.
 
asante sana kwa elimu hii..
 
Juzi nimeenda kwenye maonyesho viwanja vya sababa nikakutana na huyu mwamba amebadilisha gari kutoka kwenye mafuta ameweka mfumo wa umeme
 
Aqua ni cc1300 hybrid.

Volvo cc 2000, ukitembea zaidi ya 100km/h turbo zinafunguka unapepea balaa. Shida ni hapo kwenye mwarabu tu.
Mmh turbo inafunguka mapema tu sio hadi ufike 100 sio kweli,hata ukipaki ukiikanyagia utaisikia tu.
 
Mkuu hapo ni telsa model 3 ya 2020
Sasa Mimi natafuta ndiga za akina BYD,Zeeker,Cherry,NIO,EXpeng, hazipo kwenye portal ya TRA
Ukiona gari haipo ukienda wanaikadiria manually. Ingawa risk ya rushwa inakua kubwa.
 
Juzi nimeenda kwenye maonyesho viwanja vya sababa nikakutana na huyu mwamba amebadilisha gari kutoka kwenye mafuta ameweka mfumo wa umeme
Tatizo za EV ya kubadirisha inakua challenge range. Unakuta full charge inaenda kilometa 70.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…