Ukiwa na mkeo jizuie kupepesa macho

Ukiwa na mkeo jizuie kupepesa macho

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,436
Natumai hamjambo wananzengo.

Wakuu leo nilikua nimetoka na wife, after kushuka kwa gari mbele yetu alipita dada mwenye figure yake ukweli nilijikuta nimegeuka kumtizama, kumbe wife kile kitendo hakikumpendeza akaninunia hadi tumerudi home.

Tulipofika home akaanza kunisomea "yaani upo na mkeo unamkosea heshima na kugeuka kutizama wanawake wengine, je ningefanya hivo kwa wanaume wapitao ungependezwa? sio siri umenikwaza sana"

Ilinibidi nijishushe na kuomba samahani yaishe, nawaasa nanyi wakuu muwapo na wake zenu jizuieni kupepesa macho msije wakwaza bure.
 
Nilikuwa na huyu babe nilimzoea sana, nakuwa huru sana nikiwa nae.., tukiwa misele nikaona mdada ana mshepu wake uwa namshtua namwambia aangalie uumbaji wa sir God.....basi anacheeeka mwenyewe, sometimes ananitania nikamuombee namba na mimi namtania kausha kuna UTI sugu pale 😆😆

Macho hayana pazia, lakini muwe mnajitahidi kutuliza shingo zenu hizo muwapo na wenzi wenu...
 
Ha ha wengine tunauliza mama, niangalie ama nikaze mwendo...anasema "pixel unahitaji maombi", namuambia hata hivyo siyo mambo yangu, fahari ya macho tuu zigo kama hilo na hiki kitambi hatuwezani, anacheka siku imeisha
 
Mkuu ulitakiwa kutufunza jinsi ya kuangalia bila kua noticed na wapenzi wetu, kuna siku nilikua na mpenzi wangu pale stand ya kivukoni, magari ya tegeta kivukoni yanapopaki, kuna dada mmoja hivi nafikiri alikua hayuko sawa kichwani, niliambiwa tu mpenzi wangu mambo aliyokua anafanya na na baadhi ya maneno nilisikia aliyokua anaongea aisee nilishindwa kugeuka nyuma kabisa japokua akili ilikua inaniambia angalia uone.
 
Naongezea
Ukiwa na wife/mpenzi wako epuka au kuwasifia wanawake wengine mbele yake.
Kuna jamaa yangu aliachwa kisa hii tabia, yupo na mpenz wake lakini akikutana na marafiki zake wa kike ni kuwasifia”umependeza” wakati alietoka nae nyumbani hata hajamsifia.
 
Nikinuna we ninunue kwa hela, niwekee hela kwenye matiti na kitovu, ntakupa tabasamu na vingine. Ila ukirudia tena kunifanya ninune, bei ya kuninunua inaongezeka... kazi kwako.
sintorudia kipenzi
 
Back
Top Bottom