KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa waweke hiyo bureau iwe wazi sio kutuvizia. Shida ya watanzania vitu bayana wataficha, vya kuficha watatangaza. Upuuzi over upuuzi.
 
How do I check my status huko Credit bureau ni Database
Huwezi binafsi wanaoruhusiwa kuingia huko ni taasisi za fedha zinazokopesha tu

Wewe kujua status Yako jiangalie tu mikopo uliyokopa je huwa unalipa na kwa wakati mliokubaliana kwenye mkataba?
 
Unachosema kama ujawahi kukutana nacho utasema uongo ila nakuambia ukweli mtupu.

Nilibisha kama wewe ila ukienda pale Victoria pale Credit info utajua. Nilikosa mkopo wa biashara zangu wa mamilioni ya pesa kisa laini nilimsajilia mdogo wangu kakopa elfu 20 SONGESHA akulipa miaka mitatu nikaelekezwa niende pale FINCA HQ karibu na hao Credit info, nililipa ila niliambiwa taarifa zangu zitafutika automatically baada ya miaka 6.

Mkopo wa SONGESHA umeandikwa WRITTEN OFF
 
Huwezi binafsi wanaoruhusiwa kuingia huko ni taasisi za fedha zinazokopesha tu

Wewe kujua status Yako jiangalie tu mikopo uliyokopa je huwa unalipa na kwa wakati mliokubaliana kwenye mkataba?
Anaweza kupata taarifa zake sio zaidi ya 1000
 
Zinazo
 
ukilipa ukachukua clearance form kutoka credit bureau ukaenda nayo bank bado watakataa kukupa mkopo
 
ukilipa ukachukua clearance form ukaenda nayo bank bado watakataa kukupa mkopo
Mkuu shida siyo clearance form, shida inakuwa umeshachafua rekodi yako kama mkopaji maana inarekodi siku ulizopitiliza na kuweka marks kama vile WRITTEN OFF, HIGH RISK na kadhalika.

SONGESHA inamilikiwa na FINCA

MPAWA inamilikiwa na BOA Bank

Hizi kampuni za simu kama watu wa kati tu
 
ndio maana hata nmb mshiko fasta wameniblock wakat sijawai kiwacheleweshea inawezekana wameangalia iyo songesha maana nina miaka 3 sijawalipa 40000
 
Kwako wewe kuumizwa bank ni mpaka bank ifungwe? Financial statements zipi wakati bank kubwa ni mabingwa wa kupika vitabu? Inawezekana wanapata faida ila faida ingekuwa kubwa zaidi kama sio hizo NPL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…