KERO Ukiwa na mkopo Songesha hupati mkopo benki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
How do I check my status huko Credit bureau ni Database
 
Mikopo ya Tanzania imekaa kiuni huni ndio maana watu wanashindwa kulipa mikopo,riba z mikopo Tz zipo juu sana haziendani na hali ya uchumi wa Nchi.
 
Wewe weka unavyoona. Watu tume deal na credit scores zaidi ya miaka 25, tunajua how it works. Tz ndio imeanza hivi karibuni baada ya bank kuumizwa sana. Kazi yake basically ndio hii tunayosema kuiweka bank aware na status ya mkopaji.
 
Miaka sita? Hii ngumu kutekelezeka labda ipo kwenye maandishi tu. Kumbuka benki bila wakopaji faida yake ni ngogo
 
CRDB ndo wameanza kuwanyima watu mikopo mkuu.
CRDB ni miaka karibu 2 sasa wana shida katika kutoa mikopo sio tu wa wafanyabishara hata ya Watumishi.watu wanakwenda wanakaa mwezi ndii wanapewa mikopo,ni kama CRDB imeanza kufulia.
Nenda NMB unapata mkopo siku hiyo hiyo.
CRDB ni bank ya kishamba sana,sijui kwa nini unakuta mtu smart anatumia CRDB-bank ya hivyo sana huduma mbovu sana.
 
Umenichekesha sana, kwamba hiyo computer imefanyaiwa programming na robot au binadamu? Kwamba 1000 unayodaiwa ndiyo izuie mtumishi wa umma mwenye uhakika wa dhamana ya serikali ndo benki ikose 15,000,000 ya faida.
Wewe mtumishi wa umma bank haiwezi kukuacha. A cash cow, kwako wana uhakika utalipa kwasababu mdhamini wako ni serikali hata usipolipa wanasubiria pension yako. Wanakupa 15m unalipa 45m nani ataacha deal kama hio na serikali imekuwekea dhamana.
 
Laini akipewa mtu mwingine huwezi kudaiwa?
Lain ikishakuwa na deni hatapewa mtu mpaka ijulikane mmiliki aliyesajili mwanzo akakopa bila kulipa alikoenda.

Ni kusema hata ipite miaka kumi haitabadilishwa usajili ila siku mmiliki aliyekopa kwa kujua au kutokujua akijitokeza kwenye masuala ya mikopo kwenye taasisi nyengine atakutana na mkwamo mpaka alipe deni na riba yao.
 
Kaka hii business na hili ni soko hulia,hakuna mtu au taasisi ikaona una uwezo wa kulipa wasikupe mkopo watakuuliza mkopo a.b.c kwa nini hujalipa na majibu utawapa wakiridhika nayo watakupa pesa.
Bank zote biashara yao kuu ni mikopo,wasipo uza hiyo mikopo watajiendeshaje?? Achana na story za vijiwe.
 
Wewe weka unavyoona. Watu tume deal na credit scores zaidi ya miaka 25, tunajua how it works. Tz ndio imeanza hivi karibuni baada ya bank kuumizwa sana. Kazi yake basically ndio hii tunayosema kuiweka bank aware na status ya mkopaji.
Bank gani kubwa hapa Tz iliwahi kuumizwa na mikopo ikapelekewa kufungwa?? usije ukasema M-bank hii ilifungwa kwa sababu za kisiasa.
Kwa miaka karibu 10-15 hakuna bank imewahi fungwa sababu ya kufirisika kutokana na madeni,na hii inatokana na kuwa kwa Tanzania banks nyingi zinaoata supernormal profit kwa kuwa riba za mikopo zipo juu sana.

Kapitie financial statements za bank hata 4 kwa miaka 3 mfululuzo uangalie zinavyopata faida kubwa.achana na story za vijiweni.
 
Wewe nawe mwehu unapopata hivyo vishiringi vya mchongo unafikiri wote wa hovyo kama wewe, mkopo Kwa Mtumishi ndio unafanya aendele
mkopo unamkandamiza mtumishi angalia wote wanaopewa mikopo mara ya magari mara ya nyumba za kusihi ni ujinga mtupu na cha ajabu watumishi hawastuki..... kopa fanya biashara ikibuma pambana uanze tena sio unakopa unanunua gari na huna kitega uchumi cha ziada gari ikizingua inapaki na mkop bado unahitaju rejesho
 
Shida unaenda kuomba wewe kama wewe nenda kama kampuni uone kama watakubania. Yaani songesha ya elfu 20,000 ndio iwe kikwazo kwa mimi kupatiwa mkopo wa milioni 20+ na zaidi? Si nakopa nawapa kaela kao, hebu waache upumbavu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…