Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,157
Bi Mrembo, sasa upeo wa akili ya mtu wewe unaupimaje? Kwa kuangalia shule alizosoma, madaraja aliyopata kwenye mitihani ya taifa, au shahada alizonazo?
Manake si wengine ambao hatuna shahada yaweza ikawa ndo imekula kwetu hivyo. Tunachokiona mbele ni doom and gloom tu.
Hapana siangalii elimu yake kwa maana ya digrii ngapi amezipanga au vipi kama umenisoma toka mwanzo, naangalia uwezo wake na upeo wake kwenye 'practical problem solving skills'.
Ikawa bahati akawa na elimu kubwa nitaangalia je elimu yake ameitumia na ameiapply vipi nje ya ajira ya kuajiriwa? kwa ufupi siangalii madigrii, japo elimu japo ya form six ili nitakapokuwa na code mix na ku code switch anielwe vyema isijetokea lugha gongana akaona kama nimemtukana bure.
Hhhaha maisha bwana nilishawahi kutana na mkaka mwenye hela chafu(ni femasi sana mkoa fulani sitautaja kwani mdogo wake pia ni JF member) lakini na akili yake kwenye maisha ilikuwa inachanga hasa lakini la saba ambae hata sidhani kama alimaliza hlo la saba, kweli alinipenda saaaaaana na mie nilimpenda. Sasa ishu ikaja kwenye lugha gongana. Basi siku mie nkaamua kumpima tu kuona kama lugha zitaendana , nikawa nachanganya lugha kwa makusudi huwezi amini akawa anaona namtukana na ananung'unika kuona eti kwasababu hajasoma mie namtukana kwa kingereza...haya siku ingine nikamwambia basi dear kule chuo kuna theory ya sociology tunatakiwa tuchangie kuinunua ili tufundishiwe. Mkaka akaingia mfukoni akatoa hela bila hata kujua nini anakitolea hela. Nikajua hapa siko sehemu sahihi
Lengo la mfano wangu ni kuweka sawa kwamba elimu itakuwa ya muhimu kwa sababu tu ya kuondoa ile inferiority kati yetu hasa kwa upande wake yeye ila si kama kigezo cha kupima upeo wake.