shida ni unaziwekaje pesa bank cash na ukatoa justification? usiwe na kichwa cha kama cha mbuzi. ili ufanye online purchase ulaya, pesa yako inatakiwa kuwa kwenye bank. sasa pesa zipo home cash, atalipaje online payment china au kokote? na atazipelekaje bank kama hana justification, itabidi abaki nazo tu home, wazungu wameweka pin kila kona ili kuondokana na money laundering? kwa wale waliofika ulaya, yapo baadhi ya maduka au niseme yaliyo mengi, ukienda kununua kitu kwa cash wanagoma, zinatumika credit cards, waswaipu tu kwenye card na pesa yako itajikata kwenye bank yako ziwe zipo au utadaiwa na hiyo bank n.k. hivyo ukiondoka na begi lako la pesa ukapeleka bank, cha kwanza itabidi ueleze zimefikaje mikononi mwako hizo cash wakati sio desturi mtu kukaa na cash ndefu hivyo, kama una justification hapana shida, ila kama hauna, hautatoka pale kwasababu utaitiwa polisi, tena ukiwa mweusi ndio wanafikiri unauza unga. sasa pesa zako zipo kwenye salfeti, utanunuaje bidhaa online china au kokote? na ukipeleka bank ndio suspecion inaanzia hapo. wale mnaowaona wanasambaza mipesa kwenye vitanda mfano wacheza ndondi etc, wana justification na hata wakipeleka mzigo bank inajulikana, sasa wewe una kazi gani ulaya inayokufanya ulipwe cash pesa yote hiyo, na kodi unatakiwa kuwa umelipa. kuna mengi.