Kiufupi ni mfumo wa kutuma pesa sehemu mbali mbali ulimwenguni uliojikita katika mazingira ya Uaminifu baina ya pande mbili zinazoaminiana. Washiriki/mawakala wa mfumo huo hujulikana kama Hawaladar kwa mfano unataka kutuma hiyo pesa hapa bongo kinachofanyika ni unatafuta Hawaladar X wa nchi uliyopo unampatia taarifa za muamala ikiwa ni pamoja na taarifa za mpokeaji kisha mtakubaliana gharama ya kufanikisha zoezi hilo, mkishakubaliana Hawaladar X atamtaarifu Hawaladar Y wa nchi na eneo unalotaka pesa ifike, hawaladar Y akithibitisha kuwa na Kiasi kinachotakiwa kutumwa atapatiwa taari za anayetakiwa kupewa pesa hizo then anayetakiwa kupokea kiasi hicho cha pesa atajulishwa na kwenda kukichukua kwa Hawaladar Y, jinsi Hawaladar X na Y watakavyomalizana wanajua wao wenyewe, cha msingi pesa yako inakuwa imefika sehemu husika bila jicho wala mkono wa Serikali ama benki.