Ukiwa unaweka mafuta full tank inapunguza ulaji wa mafuta kwenye gari?

Hii ndio huwa tunaita over thinking. Enzi zile tuko tuko shule kwenye Math unakuta mtu amekokotoa karatasi nzima halafu kapata 2/10.

Kitaalam haya mawazo uliyotoa tunaweza kusema UMECHOPEKA.

Hebu tukuulize
Kwa mfano IST FULL TANK ni lita ngapi?? Convert hizo lita kwa kg, halafu linganisha na uzito wa mtu mzima mmoja Tuambie kama huo uzito ukiamua kupunguza nusu yake utaokoa mafuta kiasi gani?

Usilinganishe load ya mafuta ya ndege na ya gari. Ndege inaweza kubeba mafuta yenye uzito mkubwa unaweza Kufikia 1/3 ya uwezo wake wa kubeba mzigo. Lakini hakuna gari inayoweza kubeba mafuta yake yenyewe yenye uzito wa 1/3 ya uwezo wa gari.
 
Mkuu kwa kuuliza kuwa full tank ni lita ngapi inaonyesha wazi kwamba umekuja kubisha bila kujua hata haya mambo ya magari. Unabisha tu kwa kuwa una nafasi ya kufnya hivyo. Full tank capacity za magari zinapishana kwa kila aina ya gari, kwa hiyo kuuliza full tank ni lita ngapi haina lojiki.

Labda tuanzie gari kama Nissan Patrol. Inachukua lita 90 kuwa full tank, ambazo kwa kiasi ni kama Kg 90. Njoo BMW. Lita kama 7o, kilo 70. Halafu hizi IST labda full tank litre 45 sana na karibu kilo 45. Sasa unaniambia huo uzito si hoja?

Halafu, kama umesoma hii thread, umeshapewa hadi reference ya watu walifanya utafiti tasmi juu ya hili, wewe unakuja na point zako yeboyebo hapa.
 
Masikini!!

Nadhani wewe ndio huna uzoefu wa magari kabisa, you just talking from uncorrelation theories. Unachukua theories za ndege unaleta kwenye gari kweli 😂😂😂

Ingekuwa unachokiongea ni sahihi tusingekuwa na sababu ya kujaza full tank kwenye mabasi yetu yanayotoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Ndege inabeba tones of litres, gari kubwa linalobeba 30 tones linabeba litre 200 tu. Sasa 200kg kwa 30 tones wapi na wapi??? Yaan hata ukizidisha mzigo kwenye mzani huwezi uka opt kupunguza mafuta ili ubalance uzito wa mzigo.

Ungekuwa unajua unachokiongea kwenye hiyo hesabu yako ungefanya hivi: Baada ya zile hesabu zako za ndege Unge sample gari moja halafu halafu ukatupatia hesabu zako. Ungetuambia kabisa ukiweka 45/90 tutasave mafuta kiasi gani kwa Km moja.
 
Wewe poyoyo sana! Eti ndege inabeba tani 30 za mafuta na gari kubwa lita ishirini tu. Sasa kama ungekuwa na akili kama unavyodai, ungeelewa kwamba kama ukikubali hii theory ni kweli kwa ndege basi ni kweli kwa magari. Unachotakiwa kufanya ni kuingiza factor ya uzito wa ndege kwa uzito wa gari, na kutumia hiyo ratio katika kuangalia fuel capacity ya ndege kwa fuel capacity ya gari. Yaani scale down the the aircraft weight to fuel capacity ratio to the vehicle weight to fuel capacity ratio and see what you get.

Lakini kwa sababu ulikimbia shule huwezi kuelewa utabisha tu kipoyoyo
 
Mkuu Jitahidi kusoma vizuri ili uelewe. Itakusaidia kuwa staha kwa wenzio.

Hakuna sababu ya kutumia maneno yasiyo na staha.

Kama umesoma kwa ufasaha ni wapi nimesema ndege inabeba tones 30, ni wapi nimesema gari inabeba ishirini.

Halafu bora nikimbie shule kuliko kwenda hii shule uliyoenda wewe.
 
Una trivialize hoja. Iwe umesema ndege inabeba mafuta tani 30 au 10 za mafuta au ngapi sio hoja kuu hapo, suala ni kwamba mfano wako ni wa kipoyoyo na uliutoa ili kunionyesha mie sijui na unastahili jibu nililokupa. Shule yangu ni UDSM. Sasa kama uliikimbia na kwenda "equivalents" nadhani hapo ndio tatizo lako lipo.
 

Dah....wabongo bana...mleta mada kauliza swali rahisi kuhusu ujazo wa tenki la mafuta unavyoleta athari kwenye utumiaji wa mafuta kwa gari... wewe umeleta stori nyingi zisizo na ushahidi wa kisayansi....
Uhusiano wa injini kupoa na ujazo wa mafuta kwenye tanki ukoje?
Performance ya gari ni nini?
Ili mafuta yaunguzwe ndani ya injini hewa pia lazima iwepo. Unafahamu mifumo ya uchomaji mafuta ndani ya injini? (Kabureta, EFI, Tabo chaja nk)?
Kwa kifupi mafuta ni nishati. Nishati ni uwezeshaji wa kufanya kazi. Uzito na misuguano vina athari kubwa kwenye matumizi ya nishati...
Usikariri....elewa [emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Uwezo wako wa kusoma na kuelewa ni mdogo kama wa kuandika pia.

Kwa kifupi wewe ni mjinga.
 
Nataka nikuulize swali wanaposema gari hii fuel consumption yake ni 8km/l from factory je hapo wanapiga hesabu gari ikiwa robo tank nusu tank? Full tank je wanapiga hesabu ikiwa na full load capacity au least load capacity?
 
Nataka nikuulize swali wanaposema gari hii fuel consumption yake ni 8km/l from factory je hapo wanapiga hesabu gari ikiwa robo tank nusu tank? Full tank je wanapiga hesabu ikiwa na full load capacity au least load capacity?
Hiyo ni average consumption unapewa, na mara nyingi minimum consumption na katika ideal conditions. Kataika matumizi ya kawaida lazima utakula zaidi ya wanavyosema
 
Asante Sana blaza
 
Daaah![emoji119][emoji119][emoji119][emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah...unaijua construction ya tenki mkuu ?
 
case closed. Hili ndo jibu. Kama mtu hajakuelewa hapa basi ana shida kichwani.
 
Usifananishe ndege na ndege na magari Boss.

1. Airbus A380 ina uzito wa 360,000Kg na ina uwezo wa kubeba 103,000Kg za mafuta.

2. Range Rover Vogue L405 ina uzito 2500Kg na uwezo wa kubeba 70Kg tu za petrol sababu ndio full tank yake.

Kama unajua hesabu ukipiga ratio hapo utaona utaona utofauti uliopo.
 
We jamaa ni mweupe tayari mpaka hapo. Hilo swali lako namba moja linakuaibisha.

Hivi unajua petrol inakuwa vapour katika joto lipi?

Katika joto la -40° C petrol inaweza kuevaporate.

Unajiabisha.
 
I am sorry. Hapa umeandika ugoro tupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…