Ukiwa unaweka mafuta full tank inapunguza ulaji wa mafuta kwenye gari?

Pump huwa inapata moto. Mafuta yakiwa mengi yanasaidia kwenye cooling ya pump.
 
point. nawashangaa sana wanaofananisha gari na ndege.
 

Ist petrol lita 45 iwe karibu kg 45?

Hii ni hesabu ya wapi?

Nani kakuambia petrol ina density sawa na maji?

Acha hizo bhana.
 
Hapa umeandika upupu mwingine. Ndege na gari hazifanani. Narudia tena.
 
Jamaa anaandika vizuri.. lakini kiongozi unaandika kikorofi Sana..sio poa
 
Ist petrol lita 45 iwe karibu kg 45?

Hii ni hesabu ya wapi?

Nani kakuambia petrol ina density sawa na maji?

Acha hizo bhana.
Density ya petrol 0.71–0.77 kg/L, density of water karibu 0.91 kg /L

Sasa unajua maana ya kusema litre 45 ambazo ni karibu na Kilo 45?

Na wewe acha kubisha kipoyoyo
 
If you know, you know
 
Kumbe ndio maana tunanyimwa lift kwakuwa tutatumia mengi?
 
Hiyo hiyo ya petrol... embu angalia pump location ya escudo. Ipo juu ta tank...

View attachment 1823432
Mkuu hata kama pump iko juu ya tenk sio tatizo. Angalia hizo pipe mbilitoka kwenye pump zimeenda hadi chini kabisa ya tenk. Moja itakuwa ya kuvuta na nyingine ni return. Kwa hiyo hata mafuta yawe nusu au yamejaa sio tatizo. Na unaona ziko chini sana ndio maana unaambiwa sio vizuri kuendesha gari hadi mafuta yakauke kabisa kwenye tenki na gari izimike
 
Safi Sana injinia
 
Density ya petrol 0.71–0.77 kg/L, density of water karibu 0.91 kg /L

Sasa unajua maana ya kusema litre 45 ambazo ni karibu na Kilo 45?

Na wewe acha kubisha kipoyoyo
Kwa kukusaidia chukua hiyo hiyo 45 zidisha mara 0.7 halafu ukipata jibu jishike kifuani sema kwa sauti kuu "MIMI NI POYOYO"
 
Jibu nikweli kabisa hata Pikipiki ukijaza full tank mafuta hayaendi kabisa hasa ukiwa nasafari ndefu.
Mkuu, ngoja nikueleweshe wewe na wake wanaodhani ukijaza tenki gari au pikipiki hautumii mafuta kwa kasi. Ni kwamba tenki nyingi za magari na hata pikipiki zina namna ya shepu ambayo juu ni kubwa na chini ni ndogo. Kwa hiyo ukijaza mafuta na geji ikaenda hadi juu kabisa, utaona inachukua muda mrefu sana geji kushuka hadi kufikia nusu. Ni kwa kuwa eneo la tenki la juu ni pana kuliko la chini, kwa hiyo geji inaenda taratibu ikianzia juu kabisa.

Ukishafika nusu tenki, eneo la chini la tenki mara nyingi ni jembamba, hivyo geji itaonekana inaenda kasi kuelekea empty tenki. Ndio maana watu wanadhani ukiweka nusu tenki gari inatumia mafuta mengi na yanaisha haraka na ukiweka full tenki mafuta hayaishi haraka! Shape za tenki za mafuta mara nyingi ziko hivi kama michoro hapo chini, na ushukaji wa geji mafuta yakiwa yamejaa unakuwa wa taratibu, na yakiwa chini ya nusu tenki geji inashuka kwa kasi kwa sababu mara nyinki tenki ni nyembamba chini. Lakini bado ujue pamoja na geji kushuka taratibu ukiwa na full tank, gari inatumia mafuta zaidi kuliko ukiwa na half tank kwa sababu ya factor ya uzito kama nilivyoeleza hapo juu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…