Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
UKIZAA NA MUME WA MTU, JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LAKO MWENYEWE!
Anaandika, Robert Heriel
Unajizima Data sio!
Ati ooh! Alinidanganya Hana MKE, ooh! Sikujua kama kaoa. Wanaume ni Umbwa Koko!
Kama alikuambia Hana MKE si ungemuambia Ukoe wewe sasa ili uwe Mke wake. Mwambie apeleke posa nyumbani, taratibu za kindoa zifuate, iwe ndoa ya kimila au kiserikali au kidini. Kimila utaratibu ni simple Sana. Ukishaenda kutoa posa ukakubali tayari hiyo ni Ndoa.
Binti yangu epuka kujizima data. Mabinti WA siku hizi wengi ni wale wa liwalo na liwe. Wanayachezea Maisha yao kijinga.
Wengi wanajua kabisa Fulani ni mume wa mtu lakini kwa tamaa ya Pesa wanajilengesha Makusudi, na kujibebesha mimba, kisha baadaye wanaanza kusumbua Watu.
Acheni ubinafsi, eleweni kuwa mnawatesa Watoto wenu. Mtoto wako hawezi kulingana kihadhi na mtoto wa kwenye Ndoa. Hawezi kupata thamani kama angezaliwa ndani ya Ndoa. Mtoto wako utakayemzaa badala ya kuwa baraka anakuwa mleta tafrani Duniani.
Kwa nini usitafute Mwanaume wako akakuoa ndipo upate mtoto, uone jinsi ilivyoraha mtoto kulelewa na Baba na Mama. Wewe unazaa na waume za Watu alafu kama chizi ATI unasema ATI alinidanganya hana MKE. Hana MKE ulienda kwao akakutambulisha na Akaja kwenu kutoa Mahari ili useme alikudanganya. Wewe ndiye ulijidanganya.
Jukumu la KULEA MTOTO uliyempata Kwa Mume WA MTU ni jukumu lako ewe Binti yangu.
Hakuna Mwanamke yeyote mwenye Akili, MKE kamili atakayekubali Mume wake akuhudumie wewe au huyo mtoto wako. Na hiyo ipo Naturally ili ujutie Makosa uliyoyafanya, sasa Kwa nini umtese mtoto wako kisa ujinga wako. Ni Bora ukaacha kuzaa na waume za Watu.
ATI ili mtoto wako ahudumiwe ni mpaka vikao, sijui kupelekana Mahakamani, sijui kutukana na mume WA MTU. Kwa nini ujipe Shida? Yaani mpaka Mwanaume apate Pesa ya ziada ndio akupe wewe Pesa ya matumizi ya Mtoto. Lakini mtoto wako hayupo kwenye hesabu za Baba yake kisa Baba anafamilia Kuu anayoiangalia.
Binti yangu, epuka kuzaa na mume WA MTU kama unataka mtoto wako apate mapenzi kamili ya Baba na Mama.
Mke anayomamlaka na Haki zote kumzuia mume wake kutotoa Pesa yoyote nje ya familia. Sio ajabu Wake wakiona Waume zao wanawatoto nje wakapandisha gharama za Maisha ndani ya familia kama kuwapeleka Watoto shule za gharama na matumizi mengi yawe juu kusudi mtoto wako akose kabisa Pesa ya mume wake.
Sarah alimshawishi Ibrahimu kumfukuza Hajiri na mtoto wake waondoke katika nyumba. Ibrahimu Baba wa Imani Kwa mujibu wa Dini ya Uyahudi, uislam na Ukristo akamfukuza Hajiri na mwanaye. Kama Hicho kisa haujapata picha jinsi Hali ilivyo endapo utazaa na Mume WA MTU basi utakuwa unamatatizo.
Acha kuharibu Maisha yako. Acha kuharibu Maisha ya mwanao utakayemzaa. Zaa na Mwanaume wako.
Acha kuvuruga nyumba za Watu. Usiwe Mkosi na janga katika Maisha yako.
Epuka kuolewa MKE mwenza, hakuna kitu kama Hicho. Ni kujidanganya tuu. Ni tamaa zetu wanaume na ubinafsi wetu. Hakunaga mambo ya hivyo. Ni kuharibu Maisha tuu.
Ni Bora uwe mvumilivu na subira. Mpaka mume wako atakapofika ndio ufanye Maisha na kuanzisha familia Naye. Dunia ya sasa sio lelemama.
Ukivunja Kanuni za asili hata ungeunda sheria Kali vipi lazima mambo yazidi kuwa magumu.
Hakunaga msamiati usemao alinidanganya hana MKE. Huo ni Uongo mkubwa. Ulithibitishaje maneno yake.
Mwanaume yeyote kama upo serious naye na unahitaji awe Mumeo sharti umpe Kanuni zako kupima Nia yake. Mwambie afanye hima akuoe.
Elewa kuwa Mwana mpumbavu ni mzigo Kwa Mamaye, na hii inatokana na sababu kuwa Mama ndiye amebeba dhamana ya mtoto.
Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam