Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Ukizaa na mume wa mtu, jukumu la kulea mtoto ni lako mwenyewe!

Kwenye suala la ngono hakuna mwanaume anayejitambua.
Wanawake lazima waelewe kuwa Sisi wanaume tunapofanya ngono tupo Kwa lengo la kuridhisha Nafsi zetu.

Jukumu la mahusiano na ndoa lipo Kwa Mwanamke.

Tunachoangalia ni uhalisia bila kujali sheria zinatungwa vipi. Sheria haziondoi uhalisia.

Nimewashauri Wanawake waache kuzaa na wanaume waliooa Kwa uhakika wa Watoto wao kutunzwa ni asilimia 1% zilizobaki watahangaika wenyewe. Na huo ni uhalisia kwenye jamii na dunia yetu.

Wewe kama umeona ninahamasisha wanaume wasilee Watoto waliozaa nje ni Sawa Kwa sababu umeamua kuelewa hivyo.

Ila mada inajieleza.

Kwanza Baba Hana muda wa kuwafikiria Watoto wa nje hiyo ipo automatically.

Mwanamke gani atakubali azae na Mwanaume ambaye hafikirii mtoto wake?
"Kwenye suala la ngono hakuna mwanaume anayejitambua".

Sikujibu tena kwa kuwa hujitambui, bado hujakomaa akili.

Kwa heri.
 
"Kwenye suala la ngono hakuna mwanaume anayejitambua".

Sikujibu tena kwa kuwa hujitambui, bado hujakomaa akili.

Kwa heri.

Wewe ndio hujitambui,
Kama ungekuwa umekomaa Akili usingeshindwa kulijua Jambo Hilo kuwa Sisi wanaume Mbele ya ngono hatuna ujanja, hatujitambui.

Kila la kheri, ukienda kujifunza Jando maana unaonekana hukupita huko
 
UKIZAA NA MUME WA MTU, JUKUMU LA KULEA MTOTO NI LAKO MWENYEWE!

Anaandika, Robert Heriel

Unajizima Data sio!

Ati ooh! Alinidanganya Hana MKE, ooh! Sikujua kama kaoa. Wanaume ni Umbwa Koko!

Kama alikuambia Hana MKE si ungemuambia Ukoe wewe sasa ili uwe Mke wake. Mwambie apeleke posa nyumbani, taratibu za kindoa zifuate, iwe ndoa ya kimila au kiserikali au kidini. Kimila utaratibu ni simple Sana. Ukishaenda kutoa posa ukakubali tayari hiyo ni Ndoa.

Binti yangu epuka kujizima data. Mabinti WA siku hizi wengi ni wale wa liwalo na liwe. Wanayachezea Maisha yao kijinga.

Wengi wanajua kabisa Fulani ni mume wa mtu lakini kwa tamaa ya Pesa wanajilengesha Makusudi, na kujibebesha mimba, kisha baadaye wanaanza kusumbua Watu.

Acheni ubinafsi, eleweni kuwa mnawatesa Watoto wenu. Mtoto wako hawezi kulingana kihadhi na mtoto wa kwenye Ndoa. Hawezi kupata thamani kama angezaliwa ndani ya Ndoa. Mtoto wako utakayemzaa badala ya kuwa baraka anakuwa mleta tafrani Duniani.

Kwa nini usitafute Mwanaume wako akakuoa ndipo upate mtoto, uone jinsi ilivyoraha mtoto kulelewa na Baba na Mama. Wewe unazaa na waume za Watu alafu kama chizi ATI unasema ATI alinidanganya hana MKE. Hana MKE ulienda kwao akakutambulisha na Akaja kwenu kutoa Mahari ili useme alikudanganya. Wewe ndiye ulijidanganya.

Jukumu la KULEA MTOTO uliyempata Kwa Mume WA MTU ni jukumu lako ewe Binti yangu.

Hakuna Mwanamke yeyote mwenye Akili, MKE kamili atakayekubali Mume wake akuhudumie wewe au huyo mtoto wako. Na hiyo ipo Naturally ili ujutie Makosa uliyoyafanya, sasa Kwa nini umtese mtoto wako kisa ujinga wako. Ni Bora ukaacha kuzaa na waume za Watu.

ATI ili mtoto wako ahudumiwe ni mpaka vikao, sijui kupelekana Mahakamani, sijui kutukana na mume WA MTU. Kwa nini ujipe Shida? Yaani mpaka Mwanaume apate Pesa ya ziada ndio akupe wewe Pesa ya matumizi ya Mtoto. Lakini mtoto wako hayupo kwenye hesabu za Baba yake kisa Baba anafamilia Kuu anayoiangalia.

Binti yangu, epuka kuzaa na mume WA MTU kama unataka mtoto wako apate mapenzi kamili ya Baba na Mama.

Mke anayomamlaka na Haki zote kumzuia mume wake kutotoa Pesa yoyote nje ya familia. Sio ajabu Wake wakiona Waume zao wanawatoto nje wakapandisha gharama za Maisha ndani ya familia kama kuwapeleka Watoto shule za gharama na matumizi mengi yawe juu kusudi mtoto wako akose kabisa Pesa ya mume wake.

Sarah alimshawishi Ibrahimu kumfukuza Hajiri na mtoto wake waondoke katika nyumba. Ibrahimu Baba wa Imani Kwa mujibu wa Dini ya Uyahudi, uislam na Ukristo akamfukuza Hajiri na mwanaye. Kama Hicho kisa haujapata picha jinsi Hali ilivyo endapo utazaa na Mume WA MTU basi utakuwa unamatatizo.

Acha kuharibu Maisha yako. Acha kuharibu Maisha ya mwanao utakayemzaa. Zaa na Mwanaume wako.

Acha kuvuruga nyumba za Watu. Usiwe Mkosi na janga katika Maisha yako.

Epuka kuolewa MKE mwenza, hakuna kitu kama Hicho. Ni kujidanganya tuu. Ni tamaa zetu wanaume na ubinafsi wetu. Hakunaga mambo ya hivyo. Ni kuharibu Maisha tuu.

Ni Bora uwe mvumilivu na subira. Mpaka mume wako atakapofika ndio ufanye Maisha na kuanzisha familia Naye. Dunia ya sasa sio lelemama.

Ukivunja Kanuni za asili hata ungeunda sheria Kali vipi lazima mambo yazidi kuwa magumu.

Hakunaga msamiati usemao alinidanganya hana MKE. Huo ni Uongo mkubwa. Ulithibitishaje maneno yake.
Mwanaume yeyote kama upo serious naye na unahitaji awe Mumeo sharti umpe Kanuni zako kupima Nia yake. Mwambie afanye hima akuoe.

Elewa kuwa Mwana mpumbavu ni mzigo Kwa Mamaye, na hii inatokana na sababu kuwa Mama ndiye amebeba dhamana ya mtoto.

Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
AHsante Taikon
watajitetea hapa
kuna watakaoleta emotions hapa. umenena vema sana.

KWANN KWENYE NYUMBA ZA IBADA WANGEANZA HIYO KAMPENI kuelimisha watu (dini zinahalalisha hili tatizo) ,
 
-hujui sheria kiongozi, Mimi ni mwanaume sio mwanamke, Mimi naongea kwa mtazamo wa kisheria, Kwa kutumia Sheria ya Mtoto, local customery law declaration order

Mimi naongea Kwa Mtazamo wa kiuhalisia.
Sheria haziondoi uhalisia.

Ni Sawa na sheria za dini ya Kiislam zinaruhusu mwanaume kuoa wake zaidi ya wanne. Ila kiuhalisia mwanaume Hana uwezo wa kuoa wake wanne Kwa sababu hakuna Mwanamke anayetaka kuolewa MKE mwenza.

Mimi nazungumzia uhalisia wa Mambo.

Mapenzi ya Mama na mtoto yapo automatically.
Mapenzi ya Baba na mtoto yamekonektiwa mara nyingi na Mama.
Yaani inategemea na mahusiano baina ya Baba na Mama.
 
AHsante Taikon
watajitetea hapa
kuna watakaoleta emotions hapa. umenena vema sana.

KWANN KWENYE NYUMBA ZA IBADA WANGEANZA HIYO KAMPENI kuelimisha watu (dini zinahalalisha hili tatizo) ,

Balensiaga amesema anaongelea kisheria, lakini anasahau sheria zimetungwa na watu, na sheria hazibadili chochote kwenye uhalisia.
 
-tatizo Taikun hajui Sheria, yeye anaongea anavyoona kwake ni sawa.
kusema kweli mkuu ROB yupo sahihi sana sana.
hizo sheria wameziweka tu regulate tatizo nakupunguza madhara.
Aliyoyanena Rob yataondoa kabisa tatizo,
 
Balensiaga amesema anaongelea kisheria, lakini anasahau sheria zimetungwa na watu, na sheria hazibadili chochote kwenye uhalisia.
Kwamba atakae zaa na mume wa mtu kwa kujua au kutokujua itambidi aonje consequences za hiyo maamuzi aliyoyafanya.
 
-Kwa mujibu wa sheria zetu jukumu la kutunza mtoto ni la baba, ndiyo maana mwanaume akimpa mimba binti Ili amkomboe mtoto ni lazima alipe gharama zote za Matunzo ya mtoto, au amuoe hiyo ni Kwa mujibu wa Tamko la Kimila la serikali that is to say Local customery law declaration order
- na Ili apate Matunzo ya mtoto Mama wa mtoto itabidi ampeleke mwanaume kwenye Mahakama ya watoto, na akipinga kwamba huyo mtoto sio Wake Mahakama itatoa Amri ya kwenda kwenye DNA test, na DNA results zikionesha kuwa ni mtoto wake mwanaume utawajibika kumtunza huyo mtoto hata Kama una mke
-
Hili ndio jibu sahihi na la kitaalamu. Tofaauti na wababaishaji wanaotaka kumlaumu tu.
 
Usiwashtue tunataka ongezeko la singo maza liongezeke ili na wao waupate moto wa kutafuta kwa jasho huku wakibweka kwenye status
 
Usiwashtue tunataka ongezeko la singo maza liongezeke ili na wao waupate moto wa kutafuta kwa jasho huku wakibweka kwenye status

Mimi nawashtua Kwa sababu nawapenda.
Ila wao wenyewe wataona ninachuki nao Kwa kuwaambia ukweli.

Sifurahii ongezeko la single mother kwani sio tuu linawatesa Dada zetu Bali pia linaumiza Watoto.

Watoto wanakua pasipo ulinzi na upendo wa Baba
 
Kwamba atakae zaa na mume wa mtu kwa kujua au kutokujua itambidi aonje consequences za hiyo maamuzi aliyoyafanya.

Yaani sop itabidi, Jambo Hilo lipo automatically.
Hata iwekwe sheria ipi, Jambo Hilo lipo hivyohivyo.

Ni vizuri Tuwafundishe mabinti zetu maadili maana wao ndio wahanga wakubwa.
Hatuwezi kujidanganya kisa tumetunga visheria ndio tukadhani madhara yatokanayo na mmomonyoko wa maidili yatawakuta kijana na Binti Kwa kiwango sawa
 
Back
Top Bottom