Ulichosema ni ukweli mtupu,,japobaadhi hawataelewa. Kwenye suala zima la kuzaa mwanamke ndio mwenye maamuzi.
Ukienda Ustawi wa Jamii kesi nyingi za matunzo ni za wanawake nyumba ndogo. Mapenzi yakiisha basi mwanaume haangaiki na kulea mtoto. Na wengi wanaingia kwa madai kuwa wanapendwa.Na wanawake wengi wanajua kuzaa ndio garantee yabkupata fedha au ndoa kwa mwanaume kiti ambacho wala hakina ukweli kwani mwanaume akikupenda hata kama huna kizazi ata stiki na wewe.
Wanawake wengi wanakuwa wahanga sababu ya kujipa upofu wa maneno mazuri wanayopewa wakati mapenzi yapo moto moto. Wanawake wenyewe ndo tunaweza kujikomboa katika hili. Tufanye maamuzi ya kuzaa kwa sababu tunahifaji lkn sio kwa sababi ya tamaa,, fedha au ndoa kutoka kwa mwanaume.
Sent using
Jamii Forums mobile app