SWALI
Zinaa ni nini?
السؤال: ما الزنا؟
JAWABU الجواب
➡Zinaa ni neno lenye maana ya kitendo cha:
"Mwanaume baaleghe kuingiza utupu wake katika utupu wa mwanamke ambae si halali kwake"
الزنا لفظ يدل على معنى: " إدخال رجل بالغ ذكره في فرج امرأة لا تحل له"
➡Na zinaa inazingatiwa kuwa ni zinaa mara tu atakapoingiza kichwa cha dhakari yake katika utupu wa mwanamke asie halali kwake.
والزنا يعتبر زنا بمجرد إدخال الرجل حشفة ذكره في فرج امرأة لا تحل له.
➡Na zinaa ni katika maasi makubwa na ni njia mbaya.
والزنا من كبائر المعاصي وساء سبيلا.
➡Na uharamu wake umethibiti katika Qurani na Sunna na Makubaliano ya Maulamaa wote.
وتحريم الزنا ثبت بالقرآن الكريم والسنة النبوية وإجماع العلماء كافة.
➡Amesema Allaah sw:
(وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا)
[Surat Al-Isra 32]
Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.
➡Na Mwenye kupinga uharamu wa zinaa au akatia shaka katika uharamu wake, atakuwa amekufuru kufruru kubwa.
ومن أنكر حرمة الزنا أو شك في حرمته، فإنه يكون بهذا قد كفر كفرا أكبر.
➡Muisilaamu anatakiwa kuamini uhalali wa aliyo yahalalisha Allaah sw, na uharamu wa aliyo yaharamisha.
المسلم يجب عليه أن يؤمن بحل ما أحله الله سبحانه وتعالى، وحرمة ما حرم الله سبحانه وتعالى.
➡Ndio maana ameamrisha Allaah sw kuwapiga vita wale ambao wanakwenda kinyume na hilo, na akawaita kuwa ni makafiri.
ولهذا أمر الله سبحانه وتعالى بمقاتلة من يخالف ذلك، وسماهم كفارا.
➡Amesema Allaah sw:
(قَاتِلُوا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَا بِالْيَوْمِ الْآخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ الْحَقِّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حَتَّىٰ يُعْطُوا الْجِزْيَةَ عَنْ يَدٍ وَهُمْ صَاغِرُونَ)
[Surat At-Tawba 29]
Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.
➡Na mwenye kumchezea kwa utupu wake mwanamke ambae si halali yake, basi amefanya maasi makubwa, na anastahiki kutiwa adabu na kadhi.
ومن عبث بذكره في بدن امرأة لا تحل له فقد فعل معصية كبيرة، ويستحق التعزير من قبل القاضي.
➡Pia mwenye kuwachezea watoto wadogo, wa kiume au kike miili yao kwa utupu wake, anatiwa adabu na kadhi mpaka akome tabia hiyo.
وكذلك من يعبث بذكره في الصغار من البنين أو البنات، يستحق التعزير من قبل القاضي.
➡Na hata kama atamchzea kwa kutumia vidole au ulimi, pia atapata hukmu kama hiyo.
وحتى لو عبث بهم بأصابعه أو لسانه لحق به نفس الحكم السابق.
➡Na akijichezea utupu wake kwa mkono wake mpaka akajitoa manii atakuwa amefanya dhambi pia.
وإذا عبث بذكره باستعمال يد نفسه حتى أنزل المني، فقد قارف إثما عظيما أيضا.
➡Na akimtazama mwanamke asie halali kwake kwa matamanio mpaka akatokwa manii pia amefanya maasi, na analazimika kufanya toba kwa Allaah sw kutokana na yote hayo.
وإذا نظر إلى امرأة لا تحل له شهوة حتى نزل منه المني فقد عصى، وعليه التوية إلى الله تعالى في ذلك كله.
➡Muumini anatikiwa awe na sifa ya kuhifadhi utupu wake kutokana na yote ambayo haya kuhalalishwa na Allaah sw.
يجب على المؤمن أن يحفظ فرجه من كل ما لم يحله الله تعالى.
➡ Amesema Allaah sw:
(وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ)
[Surat Al-Mumenoon 5]
Na ambao wanazilinda tupu zao,
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.
[Surat Al-Mumenoon 6]
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ
Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.
[Surat Al-Mumenoon 7]
➡Namuomba Allaah sw atuongoze katika kuijua haki na kuifuata na kuifikisha.
أسأل الله تعالى أن يهدينا إلى معرفة الحق واتباعه وتبليغه.
ALLAAHU AALAM الله أعلم
➡Jawabu kutoka kwa
SH. SHAABAN AL BATTAASHY.