Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Hii ni hatari na nusu. Ngoja niufyate ila wametuweza
 
Huenda wanaweka mradi mkubwa hapo, najua pana barabara ya mwendokasi pia. Kosa lilifanyika kuipanga Dar linaendelea kufanyika hata katika yale maeneo mapya yanayopimwa kwa sasa.
 

Tanzania haikuumbwa kwa ajili ya kila mwekezaji dunia nzima kuja kupewa ardhi hapa.

Hao wananchi unaoshabikia wanyang'anywe ardhi zao uelewe maisha yao ya kiuchumi na kijamii yamefungamanishwa na mahali hapo wanapotaka kuhamishwa. Hivyo kitendo cha kuwaondoa hapo tu hata kama wanalipwa fidia kwanza hiyo fidia sio market value na haiwawezeshi kupata naeneo mengine yenye hadhi sawa na hapo hivyo watarudishwa nyuma kiuchumi na mfumo wao wa maisha utavurugika. Mtu aliyekuwa anapangisha nyumba yake sinza na kuingiza kipato tayari anerudi katika umaskini mkubwa.

Pili hao watu wanaohamishwq wanaenda wapi na kwa gharama za nani?

Kinachofanya makazi yawe duni ni hali za kiuchumi za wananchi hivyo hata majengo ya kisasa, yakijengwa bado kama mtu hana kipato kikubwa hataweza kupanga na kuishi.

Hii sheria ya ardhi inayoruhusu mwananchi kunyang'anywa ardhi yake kwa manufaa ya umma ilipaswa kubadilishwa.
 


Basi serikali ina hela. Kwa ukubwa huo italipa mpaka basi. Si rahisi kihivyo maana gharama ya fidia si ya kitoto.
 
Watawala wameamua kujigawia maeneo sio?
 


Huwa linaanza tangazo kama hili ili michakato hiyo uliyosema iwe halali kisheria
 
Mkuu hilo ni eneo dogo sana, sio la kuleta mabadiliko makubwa kiasi cha kuifanya Dar-es-salaam iitwe Dar-es-salaam mpya. Hizo ni ekari 47 tu.
Mkuu usistushwe na ukubwa kwa mita za mraba. Ukubwa huo ni mdogo sana maana mita za mraba zilizotajwa hapo ni sawa na ekari 47 tu ambazo pia hazipo pamoja.

Mkuu, ukilinganisha na ukubwa wa mji wa Dar-es-salaam ambao una ukubwa wa ekari 285,714, hizo ekari 47 hazina impact kiasi hicho!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…