Uko tayari? Dar es Salaam mpya inakuja. Serikali kutwaa eneo la mita za mraba 233,000. Maeneo ya Sinza, jirani na Mlimani City, Boko, SIMU2000 kuguswa

Ume assume mengi sana ambayo sijasema.

Ume assume nimesema kila mwekezaji wa dunia nzima aje kupewa ardhi hapo. Sijasema hili.

Ume assume nataka wananchi waondolewe hapo. Sijasema hilo.

Ume assume nataka walipwe fidia isiyo market value. Sijasema hilo.

Ume assume sijui kuwa kuna masuala mengine ya uchumi yanayotakiwa kufanyiwa kazi. Sijasema hilo.

Kote humo ume assume wrong.

Mimi Bibi yangu alikuwa na nyumba hapo Sinza si mbali na Mlimani City. Kuna mjomba wangu karithi yupo mpaka leo.

Ukivunja nyumba kama zile tano na kujenga ghorofa 25, halafu pale chini ghorofa ya chini kabisa kukawa na nyumba tano za wale uliowavunjia nyumba wabaki palepale, ukawalipa fidia ya kuvunja nyumba zao (ya sentimental value)halafu uwaache wawe pale ghorofa ya chini wapangishe watu au kutumia kama nyumba au biashara, hapo unahitaji kuwahamisha waende wapi tena?

Huoni kwamba kuwa hapo si tu hujawahamisha, bali pia umewaongezea value sehemu hiyo itakuwa inavutia biashara zaidi, wanaweza kuzidisha rent na wakiamua kufanya biashara wanaweza kufanya biashara kubwa zaidi?
 
Kwa ulichoandika bongo hii Ni hasara tu, maghorofa mengi marefu hayana wapangaji. Ukiongeza watatoka wapi?

CAG kwenye report yake ya 2021-2022 alilizungumza hili mashirika mengi yenye maghorofa makubwa hayana wapangaji

Pspf towers mule ndani kweupe mwaka wa ngapi huu

Posta inaanza kugeuka kuwa ghost town.

Hapo sinza tu PSSSF tower haina wapangaji. Pamoja na uzuri wote ule, location nzuri nk
 
Ndoto hizo. Hayo ili yafanyike yanahitaji pesa na muda mrefu. Hiyo pesa ipo wapi?
 
Hamna kitu. Ujinga mtupu na uchochoro wa kuiba hela unaandaliwa.
Nchi kubwa hii. Serikali Ina uwezo mkubwa wa kujenga mji MPYA kabisa let say Bagamoyo ambapo mapori mengi wanafuga wamasai na wamang'ati...... Hiyo hela ya fidia inatosha kufidia maeneo makubwa zaidi bagamoyo na kuweka miundombinu......
 
👏👏👏
 
Maghorofa mengi hayana wapangaji kwa sababu rent zimewekwa juu artificially. Pia hizo nyingi ni commercial properties nyingi si residential apartments.

Pia, rent inakuwa juu kwa kufuata sheria za demand and supply. Ukijenga maghorofa mengi kukawa na apartments nyingi, rent zitashuka tu, kwa sababu kutakuwa na supply kubwa itakayoshusha bei kwa kanuni kwamba bei inapatikana kutokana na nguvu za demand and supply.

Ukiweka rent zinazoendana na vipato vya watu, apartments za kukaa watu hazikosi watu, watu wako wanatafuta nyumba, tatizo ni rent kuwa juu artificially tena kwenye commercial properties. Mimi naongelea apartments za kukaa watu, tena ikibidi ziwekewe hata government subsidies kwa watu wenye kipato cha chini wapate makazi bora.

Mpaka nchi za kibwpari kama Marekani zina schemws kama hizi za Section 8.

Serikali ikiwa na mipango mizuri inaweza kuoanga hivi na kuwainua hawa watu kiuchumi mpaka wakaweza kuzinunua hizo apartments.
 
Mkuu ni kwajili ya stendi ya mwendokasi na karakana zake pia,sio maghorofa ya anasa
 
Umeambiwa Jiji linaboreshwa
 
Kwa sasa ni 8 milion only in Daresalaam
 
Kwa sasa ni 8 milion only in Daresalaam
By 2040 hiyo inakuwa 16 million.

Ni kama unaongeza Dar nyingine ndani ya Dar.

Bila kujenga kwa kwenda juu tutabanana sana.

Pia itabidi tufanye kazi masaa 24, karibu kila ofisi iwe wazi masaa 24, watu wagawane shift, wengine usiku, wengine mchana.
 
Wala sababu sio rent. Wapo wanalipa rent kubwa chini kuliko ambayo ipo kwenye hizo sky scrappers.

Maghorofa yapo mengi posta na hayana watu, Hilo la demand na supply na kuleta unafuu wa rent mbona bado hakuna watu?

Ukiwa unazungumza haya unapaswa kujua unazungumzia Tanzania ambayo 50% ya population cant afford three meals.

Hilo la government subsidies liondoe maana ni wazo ambao uhalisia wake haupo. NHC wamefanya projects na husema wanaweka subsidies gharama nafuu but still two bedrooms apartment inacosr around mil 200. Nani wa ku afford kulipa mil 200 kwa room mbili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…