Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Wazazi/Walezi/Walimu/Viongozi wa dini wajitambue na kulichukua jukumu la malezi serious,Serikali pia ihusike kwa namna moja ama nyingine.
Hapo ndo tatizo linapozidi,tatizo la jamii sio la kiserikali wala kidini,wala wazazi.Tatizo la maadili ni jukumu la mwanajamii Kwa nafasi yake anatakiwa kulivalia msuli
 
Mwanajamii ni nani? Wazazi.Walezi.viongozi wa dini wao sio wanajamii?
 
......mi binafsi huwa najiuliza mabinti wa leo kuzaa zaa ovyo ovyo sijui wanajisikiaje, sijui wazazi tumefeli wapi. Binti mdogo kabisa anabeba mimba tena niseme isiokua na baba, mzazi nae atashiriki kumuandalia baby shower shame!! Shame!! Akikaa kidogo kaenda tena kuzaa na mwingine, yani kawaida sahivi kila mtoto kuwa na baba ake.
Ila bora hvyo mkuu....Embu fikiria bint wa 2000s labda awe na umri wa miaka 20 apo awe amechoropoa mimba 3 adi 4....huyo tayri ana ile nguvu ya ujasiri wa kufanya uovu wowote coz kashaua nafsi zisizo na hatia,

Na watu kama hawa wanakuwa sio waaminifu kwenye jamii...
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?
Zamani hata kabla hujatoa single(wimbo)ilikuwa lazima mashairi yahaririwe ..Leo hii Kwa nyimbo za kina wasafi etc. usitegemee maadili..Zamani hata mke wa mtu alikuwa anazini Kwa Siri mno,Leo hii mke wa mtu anakuomba namba ya simu..
 
Andiko zuri, chanzo kikubwa ni malezi na mfumo mbovu wa kulinda maadili ya mtanzania. Tumeona Arusha wakiweka mfano wa mfumo wa mavazi, watu wamezodoa... Ila kile wanachotaka kufanya ni kujenga mfumo wa kulinda maadili, hapa si semi kuwa ndio mfumo njia bora but at least wameonesha nia.
Sasa Kam serikali inge weka mfumo huo kwa kufundisha Mashuleni, kutoa kama by laws ktk ma shule mitaani tangu zamani, tungeweza Linda kwa kiasi kikubwa maadili yetu.

Elimu Nido msingi mkubwa ktk malezi ya maadili mema. Serikali iweke mkazo ktk eneo hili.
Binafsi naamini mambo ambayo tunayaona madogo madogo sanana ya kawaida tu, kama uliyoyasema ya"mavazi" na mengineyo mengi sana, ni mlolongo wa mambo maodgodogo ambayo tunayachukulia ni kawida tu kumbe si kawaida na ni kichocheo kikubwa cha ukosefu wa maadili.

Mavazi kuanzia utotoni, inabidi Watanzania tusichukulie mavazi kwa watoto wadogo ni kitu cha kawaida tu na anaweza kuvalishwa vyovyote tu. Pia unayovaa sisi na tunayowavalisha wajukuu zetu, kwa wengine watoto zetu, iwe nyumbani au nje ya nyumbani, ni muhimu sana.

"dress codes" za kiheshima ni muhimu sana a'all across".Haijalishi wapi na nani, mavavi yetu ni moja ya kichocheo cha ukosefu wa maadili.

Nakumbuka "historia ya ukweli kabisa" Nyerere alipoanza maisha ya Kisiasa jijini Dar alikuja na vazi ambalo kwa siku hizo ni "fasheni", kaptura, na likivaliwa sna na wazungu, alipoanza kutambulishwa kwa wazee akaambiwa hilo vazi sasa wachana nalo, wazee hawatakuelewa, wewe unapigania kuwaondowa wakoloni basi usivae kama wakoloni ambao wazee wanachukulia kinyume cha maadili yao.

Nyerere hakubisha akawacha kuvaa kaptura katika harakati zake.

Siku hizi imekuwa kawaida eti kumkuta mtu kavaa "bukta" nyumbani kwake mbele ya wanawe au watoto wadogo wa kike na wakiume na mbele ya mama zake na baba zake na watu wazima, wengone ndiyo mpaka nje.

Juzi hapa tukaona kundi la watanzania wakivalishwa bukta zilizokunjwa mpaka kuonesha tupu zao na kupakwa mafuta mmeremeto na moosefu wa maadili mmoja, na mijinga, wanawake kwa wanaume wakafata na wengine wanaiga mpaka leo mitaani.

Tumekuwa taifa la ajabu sana.
 
Mzazi anaweza kuwa drunker Ila mtoto wake akawa sio mtumiaji wa vilevi this is what my parentsdid to me

Kilichopo wamtumikie Mungu tu hapo Maisha ya kiroho ndo kila kitu

Nina 26 yrs
Sinywi pombe
Sivuti sigara Wala bangi
Sifanyi Uzinzi na sijawahi

Namtumikia Mungu Sana na nafurahia Maisha vizuri
Utakuwa na mbuyu wako mkuu....tena ukouko unapomtumikia Mungu....
 
20231029_092215.jpg
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?
Umeongea ukweli mtupu FaizaFoxy najisikitikia mimi na vijana wenzangu ambao hatujaoa.Mungu atuongoze.
 
Kwani uislamu hauna majibu ya haya?
 
Kuiga. Vijana tunapenda kuiga maisha ya watu wa magharibi wanaona ni ujanja kumbe ni ushamba na ujinga hasa vijana wa kike kuvaa vinguo vifupi na nguo za kubana , umalaya kwao wanaona ni ufahari, sasa hivi wanashindana kudanga.

Tukirudi kwa vijana wa kiume nao ni hivyo hivyo kuiga ujinga, mfano kunyoa viduku huu ni uhuni, kuvaa mlegezo, kuvuta bangi, madawa ya kulevya yote haya ni kuiga kutoka west.

Ushauri wangu kwa vijana: Be unique that's mean you are the only one. Usipende kuiga bali kuwa mfano kwenye jamii yako kwa kuigwa. Hakuna kitu ninachopenda kuwa tofauti na vijana wengi wa nyakati hizo. Am so proudly for being myself

Being mudi
Being mtalebani
 
Kizaz hiki cha zuchu,dear x singeli amapiano maadili sifuri kabisa

Ova
 
Unategemea maadili kwenye jamii masikini?
Maadili kwenye jamii isiyotaka elimika?
Maadili kwenye jamii ambayo watoto wanajilea wenyewe ?
Maadili kwenye jamii inayolelewa na msaidizi wa kazi?
Maadili kwenye jamii isiyo na hofu ya Mungu?
Maadili kwenye jamii inayosikiliza nyimbo hamasishi za ngono, ulevi, uvutaji?

Maadili kwenye kuishi uswahilini ambapo kila mtu ana ndevu kama kambale?

Ili tuwe na maadili kila mtu aangalie mtoto wake na kumtunza vizuri kwa ajili ya kesho.

Turudi makanisani na misikitini

Tuondoke uswahilini

Tuzuie nyimbo zote za Singeli

Tuwazuie Kina Diamond

Tuzuie Tiktok
Naunga mkono hoja

Ova
 
Haohao wa nje ndo wanatuharibia maadili
 
Mwanajamii ni nani? Wazazi.Walezi.viongozi wa dini wao sio wanajamii?
Ni wanajamii pia ila jukumu la kukemea maadali mabovu hayawezi kuishia kanisan/msikitini pekee na wala hayawezi kuishia majumbani kwetu.

Kumbuka sio wote wanahudhuria kweny nyumba za ibada hayo mazingatio na mafundisho watayasikia/kuyafahamu wapi? Au hao viongozi wa dini wanawafikiaje?

Serikali yenyewe corruption imekithiri ndo useme tuitegemee kuboresha maadili?

Wazazi kila mtu yuko busy na familia yake akitoka nje hana hata habari na watoto wajiran wachache saan wanajitahidi

Mabadiliko ya jamii yanaanza na ww binafsi hakuna kuatafuta mchawi
 
Bila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozido miaka 40 watanielewa.

Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".

Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikiuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.

Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.

Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana na cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunayoyaona kuwa ni maadili mema.

Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.

My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi ndiyo tulikosea?
We pambana na maadili yako na to some extent utakavyowalea wanako; hutoweza kamwe kufanya maadili yako 100% yawe ya kila mtu 100% na pia iyo cjui TZ ilikuwa ivi cjui ivi? Jaman utandawazi unayafanya mengi yaonekane ila sio mapya chini ya jua na pia unafki mwingi unafanya watu wengi waonekane watakafitu.
 
Back
Top Bottom