Ukosefu wa maadili unatisha kwa kasi unayoporomoka Tanzania

Nakazia hapa[emoji419][emoji375]
 
Ugumu wa maisha ukosefu wa kazi kipato huchangia sana maadili kuyumba. Maana watu ili mkono uende kinywani wanafanya vitu kinyume na maadili mfano umalaya nk.
Hivi naninkasema zamani maisha yalikuwa marahisi...
 
Yalikuwa na afadhali sana kuliko maisha ya leo. Zamani ukimaliza elimu yako unapewa form ya kuchagua kazi. Sio siku hizi.
Mkuu napinga ukiegemea kwenye cheti na ajira nitakushangaa sana.
Zamani kidato Cha nne walikuwa wanashinda 3-7 tu halafu la Saba wanaweza faulu wanafunzi 9 darasa Zima hata chini ya hapo. Je wale wengine walikuwa Wana ajiliwa na nani hasa walio feli?


Story ni nyingi hasa Kwa wazee wetu wanakuambia Mimi nimesoma na fln na pengine ndo Dr, mwalimu mstaafu Kwa Sasa,Askari nk mbona walibaki na maaadili?
 
Huo ni mfano mdogo nimekupa. Ipo mingi tu hata matibabu yalikuwa bure sio siku hizi.
 
Zamani hata kabla hujatoa single(wimbo)ilikuwa lazima mashairi yahaririwe ..Leo hii Kwa nyimbo za kina wasafi etc. usitegemee maadili..Zamani hata mke wa mtu alikuwa anazini Kwa Siri mno,Leo hii mke wa mtu anakuomba namba ya simu..
Na ukimnyima anakununia balaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hali ni ya hatari sana mpaka kufika 2030,2035 huko watoto watakuwa wamechakaa

Ova
 
Ulitaka nieneze chuki za upagani?


Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.

Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?

CCM haifunzi maadili kwani??
 

Wazazi wa hiyo miaka uliyoitaja ndio wameshindwa kulea hawa watoto unaowaona leo hawana maadili.

Wazazi wenye maadili huzaa na kutoa watoto wenye maadili. Nyoka hawezi zaa jongoo.
Mbona kuna watoto wenye maadili, kumaanisha walilelewa na wazazi kimaadili.

Mzizi wa wa matatizo yote ni wazazi walioshindwa kutimiza majukumu yao. Ndio walioharibu hiki kizazi.
Jukumu la mzazi ni malezi kwa mtoto. Mtoto unavyomlea ndivyo anayokua.

Kusema sijui mambo ya utandawazi ni uongo na kisingizio cha kipuuzi cha wazazi walioshindwa majukumu yao.

Mtoto anajilea mwenyewe tangu akiwa mdogo unategemea nini?

Unakuta mzazi hajazeeka, hata miaka 60 haijui na haumwi ati anamtegemea mtoto amtunze, mtoto anitafute, upuuzi tuu.

Kila siku nasema hapa, lakini wapumbavu wanateteana na kuona kama nakosa adabu.
Nitakuwaje na adabu na watu waliokimbia majukumu yao?
 
Maadili yanayotolewa katika nafasi tofauti hasa katika malezi toka kwa watu wa karibu na namba moja ni wazazi na ili kuelekeza vijana/mtoto atende vile inamjenga vizuri yeye kuzunguka jamii hivyo wazazi na walezi ikiwa ndio namba moja katika maadili ya mtoto ukiona yuko kinyume na maadili mema bhas wa kulaumiwa wa kwanza ni mtoto ndipo itafuata mabadiliko hayo mengine kama ya utandawazi n.k

Nje kidogo ,😉😉 na mimi nitafutie mchumba wa kitanzania lakini zingatia maadili.
 
Sasa watoto wadogo wanaona vibao kata huku mitaani unategemea nini
Wasaz wao wenyewe wanashiriki vibao kata huku wanajumuika na watoto zao
Baba mama mkononi wameshikilia smartgean

Ova
 
Ugumu wa maisha ukosefu wa kazi kipato huchangia sana maadili kuyumba. Maana watu ili mkono uende kinywani wanafanya vitu kinyume na maadili mfano umalaya nk.
AlhamduliLlah, katika umri wangu nimejaaliwa kuishi na kutembelea nchi mbali mbali nje ya Tanzania.

Cha kushangaza, Tanzania niionavyo kukosa kazi kunachangiwa sana na maisha yetu tunavyoishi. Utakuta tumewazowesha vijana "kula kulala" wanapokuwa hawana kazi za kufanya bila kulipia kiaina hiyo" kula kulala".

Utakuta kijana anaweza kwenda kuishi kwa shemeji, mjomba, shangazi, ma mdogo, ma mkubwa au ndugu, jamaa na marafiki akala akalaa bila wasiwasi hata chembe. Na "ukoo" upo adhi kabisa kumpokea na kumweka hata miaka. Mifano hai ni mingi sana.

Hayo hutoyakuta nje ya Tanzania kwa kiwango cha Tanzania, tunajenga au tunabomoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…