Wapi tunakosea? Nini kifanyike?Maadili yanayotolewa katika nafasi tofauti hasa katika malezi toka kwa watu wa karibu na namba moja ni wazazi na ili kuelekeza vijana/mtoto atende vile inamjenga vizuri yeye kuzunguka jamii hivyo wazazi na walezi ikiwa ndio namba moja katika maadili ya mtoto ukiona yuko kinyume na maadili mema bhas wa kulaumiwa wa kwanza ni mtoto ndipo itafuata mabadiliko hayo mengine kama ya utandawazi n.k
Nje kidogo ,😉😉 na mimi nitafutie mchumba wa kitanzania lakini zingatia maadili.
Tumshauri nini waziri wetu wa ustawi wa jamii? Maana masikini ya Mungu, ndiyo kwanza plan ya wizara yake ipo kwenye kuandikwa. Wanayoiandika anafahamu mwenyewe ni akina nani.Wazazi/Walezi/Walimu/Viongozi wa dini wajitambue na kulichukua jukumu la malezi serious,Serikali pia ihusike kwa namna moja ama nyingine.
Hilo nalo neno.Sasa watoto wadogo wanaona vibao kata huku mitaani unategemea nini
Wasaz wao wenyewe wanashiriki vibao kata huku wanajumuika na watoto zao
Baba mama mkononi wameshikilia smartgean
Ova
Ukitaka kujua maadili yamekua ya hovyo kwa vijana, tembelea Arusha, usikie kiswahili chao, uone mavazi yao, na namna wanavyo jifananisha ktk kitu wasicho nacho, unaona wazi kabisa tunakoelekea ni kubaya sana sana kwa vizazi, wakidhani kupokea watalii watakua ni kama hao watalii ktk maisha yao, kumbe wako Arusha ktk Africa, na mtalii atarejea kwao kuendelea na utamaduni wakeBila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.
Tanzania yetu iliyokuwa inasifika ndani na nje ya nchi kwa maadili na nidhamu imeenda "arijjojo", wale waliowahi kucheza na vishada (kites) watanielewa nikisema "arijojo".
Nakumbuka miaka ya nyuma, kuna vijana nilikuwa nawasiliano nao sana US, wakati huo nami naishi nje ya Tanzania, akanambia kuna rafiki yake anatafuta mchumba nimtafutie, nikamwambia mbona wachumba wapo wengi na vijana siku hizi hakuna anaetaka kutafutiwa, akanambia hujanielewa, hataki mchumba tu, anataka mchumba kutokea Tanzania. Akanielewesha nikamuelewa, nikamuunganisha na watu Dar., Nafurahi kusema akapata mke na mpaka sasa wanazeeka pamoja, watoto zao wameshafikia umri wa kujukuu, kama bado, sina mawasiliano nao ya mara kwa mara.
Hiyo siyo point yangu bali ni mfano tu. Kama hayo yalikuwa mengi sana si kutokea Ulaya tu, hata nchi za jirani walitamani kuoa mwanamke wa Kitanzania, sababu kuu ikiwa ni maadili.
Leo hayo kukutana nayo ni nadra sana, sisemi yamekwisha kabisa, lakini yameporomoka kwa kiwango kikubwa sana. Ni nini kilichotufikisha hapo? Nafahamu wengi sana maisha wanayokutana nayo ndivyo yalivyo, hawatoweza kunielewa kabisa, kwani hawana cha kulinganisha nayo hayo, sisi wa zamani tunaoyaona kuwa ni maadili mema.
Wewe unayenisoma, maadili mema kwako ni yepi? Tutajie japo moja tu. Inawezekana kabisa nnavyoviona mimi kuwa si maadili mema, kwako ikawa ni ajabu kwanini hilo hayo si maadili mema.
My take; Maadili mema hayafundishwi tu, bali huanzia kwa kuigwa, je ni wazazi na walezi ndiyo tulikosea?
Wewe unazungumzia maadili ya dini yako?Ulitaka nieneze chuki za upagani?
Kama wewe huna dini unataka wote tusiwe na dini? Kukosa dini ndiyo chanzo kikuuu cha ukosefu wa maadili.
Kama huna dini hayo maadili utajifunza kutokea wapi?
Umeainisha matatizo, hilo ni la kwanza. Linalofatia ni kila tatizo tulichukulie kulitatuwa kwa falsafa ya "Resilience", tuligeuze kuwa fursa.Wazazi wa hiyo miaka uliyoitaja ndio wameshindwa kulea hawa watoto unaowaona leo hawana maadili.
Wazazi wenye maadili huzaa na kutoa watoto wenye maadili. Nyoka hawezi zaa jongoo.
Mbona kuna watoto wenye maadili, kumaanisha walilelewa na wazazi kimaadili.
Mzizi wa wa matatizo yote ni wazazi walioshindwa kutimiza majukumu yao. Ndio walioharibu hiki kizazi.
Jukumu la mzazi ni malezi kwa mtoto. Mtoto unavyomlea ndivyo anayokua.
Kusema sijui mambo ya utandawazi ni uongo na kisingizio cha kipuuzi cha wazazi walioshindwa majukumu yao.
Mtoto anajilea mwenyewe tangu akiwa mdogo unategemea nini?
Unakuta mzazi hajazeeka, hata miaka 60 haijui na haumwi ati anamtegemea mtoto amtunze, mtoto anitafute, upuuzi tuu.
Kila siku nasema hapa, lakini wapumbavu wanateteana na kuona kama nakosa adabu.
Nitakuwaje na adabu na watu waliokimbia majukumu yao?
Sielewi kama kuna "dini" ambayo haifundishi maadili mema. Ikiwepo hiyo itakuwa ni ya Kishetani, maana ushetani siku hizi umejaa.Wewe unazungumzia maadili ya dini yako?
Wewe ni kama unasema hakuna maadili ya kiafrika tofauti na hayo yaliyoletwa na wageni.Sielewi kama kuna "dini" ambayo haifundishi maadili mema. Ikiwepo hiyo itakuwa ni ya Kishetani, maana ushetani siku hizi umejaa.
Kabisa tena, mimi nazungumzia maadili niliyojifunza kwa mafunzo ya Kiislam.
Una wasiwasi na mafunzo ya Kiislam kimaadili?
Umeainisha matatizo, hilo ni la kwanza. Linalofatia ni kila tatizo tulichukulie kulitatuwa kwa falsafa ya "Resilience", tuligeuze kuwa fursa.
Tuitafute fursa ya namna ya kuokoa jahazi na kurekebisha tulipokosea ili tusitatuwe kosa kwa kufanya makosa zaidi.
Suala muhimu linalotukabili, ni nini kifanyike kwa kila tatizo tulilonalo linalotuathiri kumomonyoka kwa maadili kijamii?
Hao watalii wenyewe wanatushangaa sisi kuliko wanyama wanaokuja kuwaona.Ukitaka kujua maadili yamekua ya hovyo kwa vijana, tembelea Arusha, usikie kiswahili chao, uone mavazi yao, na namna wanavyo jifananisha ktk kitu wasicho nacho, unaona wazi kabisa tunakoelekea ni kubaya sana sana kwa vizazi, wakidhani kupokea watalii watakua ni kama hao watalii ktk maisha yao, kumbe wako Arusha ktk Africa, na mtalii atarejea kwao kuendelea na utamaduni wake
Mji huu unaongoza kwa maadili machafu hapa nchini
Naam nimesema hivyo. Labda tunachotofautiana ni uelewa wa neno "dini".Wewe ni kama unasema hakuna maadili ya kiafrika tofauti na hayo yaliyoletwa na wageni.
Kumbuka umesema “bila dini hakuna maadili”
Hilo siyo kweli.
Hayo majukumu ya wazazi ndiyo yepi? Tuwe specific, maadili huwezi kuya "generalize."Chakufanya ni kuwa kila mtu afanye wajibu na majukumu yake.
Mtoto hana wajibu wa kujilea wala kulea wazazi wake.
Unampa mtoto jukumu la kujilea unajiondolea haki na wajibu wake wa kukuheshimu.
Mtoto akutunze umeshafikisha miaka 60 kuendelea.
Lakini sio kuendekeza uvivu na kumpa majukumu mtoto huyo ni uhuni na Sisi tutausema siku zote. Hilo nimeliona sana.
Angalia watoto wengi waliokosa maadili utagundua asilimia 90% wazazi wao wamekimbia jukumu la malezi.
Nenda kaangalie Malaya, nenda Bara, angalia Wadada wa majumbani, nenda kwa machokoraa.
Vijana wanajitutumua kufanya kazi zozote ilimradi wawatumie WAZAZI (wabinafsi) pesa za kuwatunza.
Alafu huyo mzazi mwenyewe unakuta nguvu anazo, umri haujaenda, kuumwa haumwi. Hiyo ni akili au matope.
Acha mambo yaende jinsi yalivyo. Hiyo ndio namna ya kuisadia dunia. Acha mambo yaende vile yaendavyo.
Hiyo ndio maana ya kizazi cha nyoka.
Unazaa watoto, alafu watoto wanajilea wenyewe
Hayo majukumu ya wazazi ndiyo yepi? Tuwe specific, maadili huwezi kuya "generalize."
Ndipo niliposema, unaloliona wewe silo, mzazi mlezi mwengine analiona ndilo bora.
Kizazi cha 2000+ kina laana...[emoji28]......mi binafsi huwa najiuliza mabinti wa leo kuzaa zaa ovyo ovyo sijui wanajisikiaje, sijui wazazi tumefeli wapi. Binti mdogo kabisa anabeba mimba tena niseme isiokua na baba, mzazi nae atashiriki kumuandalia baby shower shame!! Shame!! Akikaa kidogo kaenda tena kuzaa na mwingine, yani kawaida sahivi kila mtoto kuwa na baba ake.
Jukumu la mzazi ni kuhakikisha anamlea mtoto mpaka atakapojitegemea, kwani hao wazazi wanashindwa akili na wanyama?
Tatizo chama cha mambuziBila ya shaka, wengi wa wale wenye umri iliozidi miaka 40 watanielewa.