Ukraine: Mataifa ya magharibi yanatuangalia kwa mbali, njooni mtusaidie

Ukraine: Mataifa ya magharibi yanatuangalia kwa mbali, njooni mtusaidie

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Volodymyr Zelensky ametoa ombi jingine kwa washirika wa nchi za Magharibi kuisaidia Ukraine na kukomesha mashambulizi ya kikatili ya Urusi.

"Leo asubuhi tunalinda taifa letu peke yetu. Kama jana, majeshi yenye nguvu zaidi duniani yanatazama kutoka mbali," Zelensky alisema katika hotuba yake kwa taifa asubuhi ya leo.

"Je, Urusi ilishawishika na vikwazo vya jana? Tunasikia katika anga yetu na kuona kwenye ardhi yetu kwamba hii haitoshi."

Kiongozi wa Ukraine amethibitisha mashambulio mengi ya makombora yaliyoripotiwa alfajiri ya leo.

Zelensky alisema mashambulizi hayo yalianza saa kumi asubuhi kwa saa za huko Ijumaa.

Ameongeza kuwa mashambulizi ya Urusi yalilenga maeneo ya kijeshi na ya kiraia. Urusi hapo awali ilisema hailengi raia.

Lakini kama tulivyoripoti hapo awali, mji mkuu wa Kyiv umeshuhudia milipuko asubuhi ya leo, ikiwa ni pamoja na kile kinachoonekana kuwa shambulizi lililolenga jengo la makazi.

BBC Swahili
 
Madhara ya kuchagua viongozi wa sio na akili , kila kitu anafanya masiala na vichekesho mpaka kwenye maisha ya watu
Kumbe hata Ulaya huwa wanafanya huo upumbavu?

Hivi USA atakubali kweli kuruhusu RUSSIA kuweka kambi zake za kijeshi jirani na nchi zinazoizunguka USA kama Mexico na Canada[emoji848][emoji16]

Putin yuko sahihi.

USA ni mnafki sana, ni sawa na ule ujinga wa kuonea vidagaa visitengeneze silaha za kujihami za nuclear bombs ilihali yeye anazitengeneza.

Ndiyomaana Kiduku(Rais wa North Korea) alimkomalia alizitungulia hapo hapo USA toka Korea Kaskazini na kuachwa aendelee kutengeneza maana aliona USA ana unafki mwingi sana [emoji38]
 
Kuna mmoja aliandika jana eti mataifa kama Russia ni haki na halali yawepo ili ^kubalansi shobo^ za Mmarekani! I can't agree more! 🙂
 
Anae jua kazi ya UN please [emoji81][emoji81]au ndo pambo kama the league of nations
Kwani yale matamko makali-makali hukuyasikia? Ndiyo kazi yao imeishia hapo. Sana-sana wanangoja mshahara mnono unaotokana na kodi zetu.
 
Back
Top Bottom