Ukraine sasa iko katika vita kamili vya kujikomboa

Unaeshangilia rais zelenski wa ukraine ni sawa na unashangilia mauaji ya Adolf Hitler wa ujerumani kwa waisraeli tofauti na Ukraine kuna misemo na vitendo vya kinazi kama vile “glory to the nation death to the enemy” pia “Ukraine above all” hii ni misemo inayotekelezwa kufanya mashambulio katili kwa warusi waishio Ukraine kabla ya anguko la U.S.S.R. Pia mmarekani na vyombo vyake vya western kwanini hawataki kusema ukweli kuhusu upande wapili? Kwanini wanawaangalia tu wa Ukraine na wala sio warusi wa toka enzi za USSR?
 
Kijeshi au kivita, Mrusi kapoteza zaidi kwa askari wengi na vifaa vingi (vifaru + ndege) kuangamizwa.

Ukraine imepoteza zaidi kwa miundombinu, majengo mengi kubomolewa, raia wengi kuuawa na kukimbilia uhamishoni.
Mnatumia nguvu nyingi sana kuficha hasara aloipata na anayoendelea kuipata UKRAINE kwakila angle
UKRAINE wanaangamia
 
Mkuu una akili ya kufikiria mbali . asante sana
 
Russia alikuwa anatoa vifaa chakavu store....
hajaanza kutumia silaha zake za kisasa
kwa kifupi Russia alikuwa anatafuta shimo la taka akatupe uchafu......
Sidhani mkuu Yaani aone wanajeshi wake wanakufa eti dump. La taka
 
Ni mwisho wa madikteta, Zelensky tokomeza madikteta, ukimalizana na huyo afuate dikteta wa Belarus baadae Africa.
 
Jidanganye
It’s of no consequence to me. Hata hivyo zingatia kuwa Putin (sio Urusi) anapambana na dunia. Hakuna ushindi hapo. Watamtembeza hadi aishiwe na kuachia ngazi. Ukraine wataijenga upya chap chap.

Kama walivyoua uchumi wa kikomunisti basi na tawala za kikomunisti (state dictatorship) zinahitaji akili kubwa kuzidumisha. Akajifunze kwa wajanja Xi Jinping na Kim jong un. Sio anavyojiexpose kwa jazba huko Ukraine.
 
Ukraine ni uwanja wa mapambano tu lakini vita ni vya nato na marekani dhidi ya Russia
 
German, UK, France n.k zimemuacha mbali kiuchumi Russia. Na si tu kiuchumi, hata kiteknolojia. Product za Ulaya sio za kitoto kabisa.

Ukiondoa Manuclear, tukisema zichapwe kawaida tu, UK au German au France, wanaingia mpaka Moscow mapema sana.
Hawawezi kukuamini hawa.. Russia Ameonesha weakness kubwa
 
Atajijengaje wakati maeneo yake muhimu itachukuliwa na warusi mpaka bahari yaani Kwa kifupi Ukraine inaenda kugawanywa.
 


Nasema tena; kuvamia kwa nia ya kujilinda ni HAKI, mimi siungi mkono kuvamia kwa madai ya udanganyifu kama alivyofanya George Bush kule Iraq nk.
 
Nasema tena; kuvamia kwa nia ya kujilinda ni HAKI, mimi siungi mkono kuvamia kwa madai ya udanganyifu kama alivyofanya George Bush kule Iraq nk.
Kuvamia (kama ilivyo kwa kubaka) ni kuvamia tu. Haijali kafanya nani wapi.

Iwe Amini, Bush, Putin, NATO, Sirro nk. Ukivamia wewe ni mwovu tu.

Mpenda haki yeyote asipokemea hilo na astaafu tu. Atakuwa hana jipya!
 


Ni sababu tosha kwani ngome pekee kwa usalama wa Russia upande wa Magharibi ni Belarus na Ukraine (neutral ground), mojawapo ya hizo ngome ikijiunga na NATO ni hatari kwa Russia na hiyo itapelekea hatari kwa usalama na amani ya dunia kwani kilichokuwa kinaendelea ni juhudi za US kuteza nguvu za Russia (super power) kupitia NATO ili hatimaye duniani kuwe na mbabe mmoja US. Hizo nchi zingine hakubali US atumie ardhi zao kama base za kijeshi, Zelensky ni pro US tofauti na Yule mtangulizi wake waliyemfurusha kwa hila madarakani kwa msaada wa US.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…