Unafuatilia huu mpambano unavyokwenda au unakielezea kile unachokielewa kwa kile unachokiona kuhusu huu mpambano?
Kwa ufupi umeachwa nyuma kwa taarifa nyingi sana! Au pengine uruhusu kuwasikiliza wajuzi wa mbinu za kivita kama wengine tunavyofanya, na hili ni bora zaidi kwako na kwa wengineo wenye mfano wa kwako.
Kuizingira miji mfano wa Kieve ni mbinu ya kivita ndivyo wataalamu wanavyosema. Huo ni mji mkuu wa nchi hivyo utalindwa kwa gharama yoyote ili usianguke. Msafara wa jeshi la Russia kuonekana unaelekea Kieve ukawafanya sehemu kubwa ya jeshi la ukraine kuuhami mji wao kwa gharama ya namna yoyote. Sehemu nyengine za nchi zikabakiwa na idadi ndogo ya jeshi kukabiliana na Russia.
Alichokifanya Russia ni kuuzunguka mji wote. Mianya yote akaiziba. Hii ikawa ni faida kwa sehemu nyengine za Ukraine zenye majeshi kuteketezwa kwa urahisi kwa sababu upinzani ulikuwa mdogo.
-Nukta nyengine ni kwamba mkutano wa uliyofanyika baina ya Russia na Ukraine ya amani uliyofanyika nchini Turkey moja miongoni mwa guarantee walizokubaliana nazo kwa kukubaliana baadhi ya matakwa ili kuiendea amani kwa mustakabali wa pande zote mbili ni Russia kuondosha sehemu za majeshi yake baadhi ya sehemu za Ukraine. Ndiyo maana Russia akaondoa majeshi yake Kieve na kwengineko ili kuonyesha kuwa yupo serious na anaheshimu makubaliano.
Hotuba ya rais wa Russia ipo wazi na kama mdau wa juu
Mokaze alivyowasilisha huu mgogoro una historia. Naam, tutamlaumu Putin kwa alichokifanya ila kuulewa huu mgogoro zaidi inakubidi uutumie muda wako kusoma majarida mbalimbali ya uhasama baina ya NATO na Russia(Soviet).
Maazimio ya kile Rais wa Russia alichokiita Special military operation ni yaliyojikita kwa usalama wa Russia na usalama wa raia wa majimbo yaliyojtangaza kujitenga Ukraine ambayo ni:
1)Kupunguza nguvu jeshi la Ukraine na kuondoa NAZI.
2)Kuyakomboa majimbo yaliyojitenga nchini Ukraine dhidi ya uonevu wa jeshi la Ukraine.
-Nukta ya kwanza ambayo kwa mujibu wa Russia tayari wameshaitekeleza. Ikiwa kama kweli unafuatilia hii vita utaona tangu siku ya kwanza jeshi la Russia lilikuwa likilenga kambi za jeshi, maghala ya kuhifadhia silaha, maghala ya kuhifadhia mafuta, yaani miundombinu yote ya kijeshi kwa ujumla. Hii ndiyo demilitarization. 90% ya jeshi la Ukraine limeharibiwa na hili limethibitishwa na msemaji wa Ikulu ya Ukraine.
-Phase 2 ambayo Russia wameitangaza ndiyo hiyo ya kuikomboa hiyo miji kutoka mikononi mwa jeshi la Ukraine ambapo mpaka jana taarifa zinasema kulikuwa na idadi ya 6000 ya wanajeshi wa Ukraine.
Mpaka sasa taarifa ni kuwa: "The cleanup of Mariupol continues. As of April 7,2022, the allied army of the DPR and Russia liberated Novogrigorovka (Volodarsky district), Pannovka, Suzhenka, Lugovoye, Sadovoye, Fedorovka, Kalchinovka, Nazarovka, Ukrainka, Republic, Ksenovka, Novoromanovka, Sergeevka, Starchenkovo, Peremoga, Priazovskoye, Shevchenko (Pershotravnevy district), Ilyichovskoye, Rybatskoye, Chervonoye..."
Short situation report: Mwendo huo huo ndiyo wanaokwenda nao:•
-Kherson-Nikolaev.
-Odessa.
-Zaporozhye.
-Ugledar-Velika Novoselka
-Maryinka.
-Avdiivka.
-Izyum.
-Kharkiv—Sumy.
Ukraine ameshapoteza kwenye huu mpambano pakubwa sana!