Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Hadithi ulizoweka haziko wazi kuonyesha siyo sahihi, sababu ya kwanza nilikuuliza kwani Mtume ameswali sala ya Khofu mara ngapi ?

Lakini, uchambuzi wako wa hadithi sio sahihi sababu hujachambua sanadi tujue kweli maneno hayo ni ya swahaba Abuu Huraira au la. Lazima turudi kwenye asili kwanza.

Kwanza thibitisha ya kuwa hayo maneno aliyasema Abuu Huraira, ili iwe ameyasema chambua sanadi kwanza.

Kwenye hadithi haionyeshi ya kuwa alisema aliswali hiyo Sala mwaka wa 5. Ndio maana nikakuuliza je Mtume aliswali mara ngapi swala ya Khofu ? Hujajibu hili swali.

Siyo kwamba naogopa bali Abuu Huraira hawezi kusema uongo, ndio maana nataka uchambue sanadi kwanza kabla ya matini. Usiruke hatua za uhakiki wa habari.

Unachokifanya wewe uko nje ya misingi ya elimu ya Hadithi, na hizi tabia wanazo sana Mashia katika kuwatusi maswahaba wa Mtume.

Umejuaje kama hazina shaka na haujafuwekea uchambuzi wa sanadi hiyo, kwa kitabu ulichokuwa nacho, kimekata sanadi Sasa tafuta chenye sanadi utuchambulie kwa mujibu wa elimu ya Hadithi usahihi wa sanadi hiyo.
 
ila Kuhusiana na utaalamu wa Hadith basi Imam Abu Ahmad Al Hasan bn Abd Rahman Ibn Khalal Al Farsy Al Ramhurmuzi ambae ni mtaalamu mkubwa wa mfumo wa makundi ya I’lm ya Hadith anasema kua ‘Abd Ar Rahman Ibn Al Mahdi amesema kua:
Sio "Ramhurmuzi" sahihi ni "Ramahurmuzi".
 
Sasa uliposema Imam Bukhari hajafikia level za Taqlid ulimaanisha ?
 
Ni kweli dini zipo tofauti lakini Chimbuko la dini za ukristo na uislam ni imani za simulizi za wayahudi ambazo Yesu na Muhammad walikuja kuzifanyia remix

Kwa miaka mingi wayahudi wamekua na simulizi za imani yao kupitia mababa zao wa imani
Kimsingi ni kwamba AGANO LA KALE ni simulizi za mapokeo ya kiimani ya wayahudi ambazo zinapatikana kwenye vitabu vyao TANAKH

Alipo kuja Yesu hakuanzisha dini yake from the scratch, alitumia Agano la kale la Wayahudi kuhalalisha yeye ni Masiha aliyetabiriwa kwenye Agano hilo.
Wayahudi wakamkataa wakamuua, wafuasi wake wakakusanya habari zake zikawa AGANO JIPYA(ndani kuna Injili)
UKRISTO ukazaliwa rasmi ukitumia AGANO LA KALE na AGANO JIPYA

Alipokuja Mohammed alikua amezungukwa na wayahudi na wakristo ambao walikua wanampinga, akaona ili awapate ni lazima atumie sehemu ya Imani yao kwa kuwatambua mababa wa imani zao
Akaanza kukopi hekaya za kwenye Agano la kale na kuzifanyia mabadiliko kwa madai kwamba vitabu VIMECHAKACHULIWA ila version ya hekaya zake ndio sahihi
Akaja na kwa Wakristo na Agano Jipya(injili)akamtaja Yesu tu ila aka twist kiaina plot ya hekaya nzima ya Yesu

Na ndio maana Mohammed kwenye hekaya zake za Quran aliwataja Mitume 26 tu na katika hao 26 mitume 23 aliwakopi kutoka kwenye Ngano za simulizi za Wayahudi kutoka TANAKH na Yesu akamkopi kwenye Injil ila aka twist plot kuhalalisha utume wake
 
Sheikh Usimbilie Ushia Mimi sio Shia wala sunni wala ahmadiya wala Yeyote kati ya hao..
Nilichotaka kukuonyesha kiko wazi..

Unataka Nikuchambulie Sanadi kwenye Hadithi iliyowekwa Tayri kwenye Sahihi Bukhari na kupewa Daraja La Sahihi?

Uko serious Kabisa?

Najua Unachosema ni sahihi kuwa Sanadi ni Muhimu sana katka Dini..

Kama Abd Allah Ibn Al-Mubarak alivyosema:
Yule atafutaye I’lm kuhusu dini bila ya Isnad hua ni sawa na anaetaka kupanda juu ya paa bila ya ngazi’.

Na Sufyan Ath Thawri pia alisema:
Isnad ni silaha ya Muumin. Jee Mu’umin atajilinda vipi pale anapokua hana silaha?’

Lakini Je,Unatilia shaka Sanadi ya Al-Bukari??
usisahau Sahihi Bukhari ni Miongoni mwa Sihah al Sittah au al Kutub al Sittah..
kilichokusanywa na Imam Muhammad Ibn Ismai’l Al Bukhari..


Na pia Je unasahau kuwa Hata sanadi Hutungwa na watu..Nitakupa mfano..

Miongoni mwa watu waliotunga Sanadi na hadithi walikuwemo kama kina Abd ul Karim Ibn Abi Al Awja, Muhammad Ibn Said Al Shami na Al Harith Al Kadhab Abd Rahman Ibn Udays ambae alijitangazia kua yeye ni Mtume na kupewa adhabu ya kifo na Khalifah Abdu ul Malik Ibn Marwan.

Abd ul Karim Ibn Abi Al Awja alienda Damascus na baada ya kugundulika kua ni mzushi alikamatwa na kupewa adhabu ya kifo, baada ya kukamatwa kwake alikiri kwa kusema kua: ‘Nimezusha takriban Hadith 4000, ambazo kutokana nazo nimekufanyeni mfunge wakati si siku za kufunga, nimekuhalalishieni vile visivyokua halali, na kuharamishieni vilivyokua haram.

Amesema Al Khatib al Baghdadi katika kitabu chake cha Al Kifayah, kuwa siku moja Umar Ibn Musa alikuja Homs, Syria.
Watu wakamzunguka msikitini na akasema: ‘Tumepata habari kutokana kwa Shaykh wenu kua kuna Hadith isemayo kadhaa wa kadhaa’.

Alipoendelea kuzungumzia Hadith hiyo, Afiir Ibn Midan akamuuliza Umar Ibn Musa: ‘Jee unamzungumzia Shaykh wetu gani huyo? Tutajie jina lake ili tupate kumjua’.

Umar Ibn Musa akasema: ‘Ni Shaykh Khalid Ibn Midan’.

Afiir akamuuliza: ‘Jee ni mwaka gani ulikutana nae?


Amir Ibn Musa akajibu: ‘Nilikutana nae mwaka 108 Al Hijr’

Afiir akamuuliza: ‘Jee ulikutana nae wapi?’.
Amir Ibn Musa akajibu: ‘Nilikutana nae katika vita vya Armenia

Hivyo Afiir akasema : ‘Muogope Mola wako, na usiseme uongo, kwani Khalid Ibn Midan alifariki mwaka 104 Al Hijr lakini wewe unasema kua ulikutana nae miaka minne baada ya kufariki kwake, wacha nikukumbushe kua hakupigana tu katika vita vya Armenia bali pia alipigana katika vita vya Byzantium (Warumi)

(simulizi hiyo ipo kwenye Al Kifayah fii I‘lm ir Riwaayah).


Kwa kusema hayo naomba twende kwenye Uchambuzi Tuanze na Sanadi tumalizie na matini kama Unavyotaka


Na nitaanza na Hadithi namba 4137 Juzzu ya 7 ya Sahihi Albukhari ...



Kama hadithi inavyosema..
Amesimulia Abu az-Zubayr kutoka kwa Jabir ibn Abdullah,

Sasa Hadithi kwa Urefu zaidi ni Hii hapa chini..kwenye Riwaya..

narudia Tena Concern yangu Hapo chini Ukisoma Utagundua Ni vita gani inayotajwa na Ilifanyika Vipi na vita hiyo kipindi inafanyika Abu huraira bado Hakuwa Muumini..

Usiniulize tena Vita gani Unless Hukusoma Tarekhe bhasi nitakusaidia kujibu

Narudia tena Swali Abu huraira kadanganya??
usije sasa na Blah blah za uchambuzi jikite kwenye swali
 
Mtoa mada ungefananisha
Ukatoriki na Uislamu ndio dini zinazo fanana.

Ukatoriki - Uislamu
Rozali - Tasbihi
Roma - Maka
Jumapili - Ijumaa
Sanamu - Jiwe Jeusi la Maka(aswadi)
Maria - Uzza, Lutta na Manata
Kwaresma - Ramadhani
Papa - Hadija mke wa mtume
Katekisimu - Qurani, Al-Yassin
Malaika - Majini
Liturujia - Kumpiga mawe Shetani.
Tehorani - Ahera, Kuzimu.
Kubatiza vitoto - Kusilimu.
Papa - Waraqa bin Naufal
Kilatini - Kiarabu
Kanzu - Kanzu
Kanisa - Msikiti
Kengele - Azana
Sadaka - Sadaka
Zaka - Zaka
Msalaba - Mwezi na Nyota
Bikira Maria - Muhammadi
Kupiga magoti - kusujudu
Njia ya Msalaba- Kudhikiri

Nk. Nitavitaja vingi tu nikitulia.

Ukristo hauna hizo mambo.
 

Naam sahihi kabisa, na ndio maana mpaka kesho wanachuoni wanaendelea kuzahakiki na kuzipitia ndio maana kukapatikana hadithi dhaifu katika sahihi al-Bukhari. Unafikiri walijuaje wanachuoni kama Kuna hadithi dhaifu kwenye sahihi Bukhari ? Sababu walizihakiki.

Kuchambu sanadi ni jambo la lazima katika hadithi, sababu katika sanadi ndio utamjua nani amechukua habari kwa nani ?
 
Ndio maana nataka ulete sanadi huenda hizo hadithi ulizoziweka zote zimetungwa kuanzia sanadi mpaka matini.

Lakini ajabu naona ubazunguka zunguka. Kingine nilichokiona kwako huna hivyo vitabu zaidi ya soft copy tu pekee.
Nina Hardcopy na softcopy kabatini..
MImi ni msomaji mzuri sana na Collector (Mkusanyaji wa Vitabu)
 

Hii ndio shida ya kutokuwa na elimu juu ya kile unachokijadili.

Swali langu, la je Mtume aliswali mara ngapi swala ya Khofu hujalijibu. Umeacha kujadili sanadi unerudi kwenye tarekhe. Maliza kitu kimoja kwanza.

Lengo langu mwisho nije nikufundishe namna gani hadithi zinacuambuliwa na kuhakikiwa.

Abuu Huraira hajadanganya, sababu ni muadilifu. Ili iwe amedanganya kweli kwanza chambua hadithi hiyo kuanzia kwenye sanadi.
 
Sheikh Usimbilie Ushia Mimi sio Shia wala sunni wala ahmadiya wala Yeyote kati ya hao..
Nilichotaka kukuonyesha kiko wazi..

Huenda ukawa Mshia wewe, au umecopy toka kwa Mashia, haya ndio mapito yao. Na mtihani walio pewa Mashia ni kutokuwa na elimu ya Hadithi.
 
Amesimulia Abu az-Zubayr kutoka kwa Jabir ibn Abdullah,

Kingine hii sanadi haijakamilika mzee. Mpaka kufikia kwa Abuu az-Zubayr Kuna wapokezi umewaacha. Waweke mpaka masimulizi yatokee kwa Imam Bukhari.

Ndio maana nasema hivi, wewe una soft copy za vitabu ambavyo vimeondolewa sanadi.
 
Kwakuwa umetaka nichambue ok sawa Ngoja nikuchambulie..

Kwanza nitaanza na Tarekhe ambayo Umeikwepa..
Kwa sababu ninaamini ndyo shida haswaa kubwa ulonayo...

Kwanza Hii ndiyo hadithi Haswa tunayoijadili kabla hatujaenda kwa nyingine..




وقال أبو الزبير، عن
جابرٍ: كنا مع رسول الله ﷺ بِنخْلٍ
فصلى الخوفَ، وقال أبو هريرةَ:
صليتُ مع النبيِّ ﷺ في غَزوةِ نَجْدٍ
صلاةَ الخَوْفِ . وإِنَّما جَاءَ أَبُو هُرَيْرَةَ
إلى النَّبِيِّ ﷺ أَيَّامَ خَيْبَرَ [راجع: ١١٢٥ صحيح البخاري، ٤١٣٧]​

Inatamkwa hivi..

Wa qāla Abū Zubayr, ‘an Jābirin: Kunnā ma‘a Rasūlillāhi ﷺ bi-Nakhlinfa-ṣallā al-khawfa, wa qāla Abū Hurayrah:ṣallaytu ma‘a an-Nabiyyi ﷺ fī Ghazwati Najdinṣalāta al-khawf. Wa inna-mā jā’a Abū Hurayrahإلى an-Nabīyyi ﷺ ayyāma Khaybar [rāji‘: 1125 Sahih al-Bukhari, 4137]


Sasa Tuendelee kwa kuwa Kuna matukio kwemye Matini Yametajwa tuyaangalie..

Swala alKhawfa umeuliza zilifanyika Ngapi Jibu ni Nyingi ila swala ya Hofu iliyofanyika "Nakhl"...Iko moja tu...

Nakuuliza Tena unakumbuka Swala ya Hofu iliyofanyika Nakhl Ilifanyika lini??

NA pia Bila kusahau Vita ya Najd (Ghazwati Najdin) ilo moja Tu na swala ilifanyika Moja tu hapo...

Na Vita Ya Khaibar inafahamika Kuwa ilifanyika lini na ni Moja tu Kipindi cha mtume..

Kwa matini hizo unafahamu Abu huraira amesilimu Lini??

Je hizo vita zilizotajwa zimemkuta abuhuraira akiwa Muislamu?
Au Abu huraira kasilimu kazikuta hizo vita??
Ni swali ambali nilitaka Uniambie ila unachenga sana kulijibu..

Ooh Swala ya khofu imeswaliwa Mara nyingi sasa nimekupa Hizo.specific Battle...

Turudi kwenye isnad Ili nikuachie Al-Jarh wa l-Ta'dil fi Jābirī wa Bukhārī Sanadī...

Hadithi Hiyo chain yake Ni Jabir ibn ‘Abdullah ambaye Ni Swahaba Mmojawapo aliyeshuhudia Tukio Hilo, akaja Abu Zubayr ambaye ni Tabi'i aliyepokea, Imam Bukhari alirecord hadithi hiyo toka kwa Zuberi..
 
Hadithi Hiyo chain yake Ni Jabir ibn ‘Abdullah ambaye Ni Swahaba Mmojawapo aliyeshuhudia Tukio Hilo, akaja Abu Zubayr ambaye ni Tabi'i aliyepokea, Imam Bukhari alirecord hadithi hiyo toka kwa Zuberi..
Huu uzi lazima utaukimbia, ni Zubeyr au Abu Zubeyr ?

Kati ya Imamu Bukhari mpaka kwa Abu Zubeyr Kuna miaka mongapi ?

Tuendelee ...
 
Swali langu rahisi hujalijibu, sababu matini inaonyesha maswahaba walikuwa wanaelezea tukio kulingana na muhusika alivyo lidiriki.

Hapa achana napo patakuumiza na hauwezi kutoboa.
 
Swali langu rahisi hujalijibu, sababu matini inaonyesha maswahaba walikuwa wanaelezea tukio kulingana na muhusika alivyo lidiriki.

Hapa achana napo patakuumiza na hauwezi kutoboa.
SIo pataniumiza ni kwamba Huna uwezo wa kupazungumzia na Nahisi ndo kikomo.chako maana huwezi kueleza zaidi ya hapo maana unaogopa kudanganya na Unaogopa pia kumkosea Adabu Swahaba kwahyo uko Dilema...😅😅
 
Swali langu rahisi hujalijibu, sababu matini inaonyesha maswahaba walikuwa wanaelezea tukio kulingana na muhusika alivyo lidiriki.

Hapa achana napo patakuumiza na hauwezi kutoboa.
Na nimelieleza Tukio kwa Mara Tatu sasa Na zote hizo Abu huraira hakuwa Amesilimu bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…