Ukristo ni kutukuza utamaduni wa watu weupe, tujitafakari sana

Acha hoja ya kipuuzi, hakuna mwafrika anayetukuza uzungu, waafrika still wanaabudu dini zao za asili. Kama wazungu walieneza mifumo yao afrika kuna ubaya gani wakati tunatumia teknolojia zao?
 
Jiwe walilo likataa waashi ndo limekua jiwe kuu la pembeni kwa walio okolewa ukristo wanautambua vyema wewe bado
 
Screenshot_20241117-112953.jpg
 
Screenshot_20241117-193653~2.png
Kwa wale ninaowaambia kuwa ziko Qur'an zaidi ya 30 hapa nimewaonyesha hizi 2 tu, Hafs inayotumiwa na wengi na Warsh inayotumiwa zaidi kaskazini magharibi hasa Morocco! Je, tafsiri ni sawa?
 
Ukristo uliingizwa na wazungu Afrika kwa mara ya kwanza katika karne ya 1 AD Misri na Tunisia na baadae kuenea kaskazini. Karne ya 4 AD Ethiopia iliufanya ukristo hata kuwa dini ya kitaifa chini ya mfalme Ezana kwenye himaya ya Aksumite.

Lakini umeenea zaidi Afrika Chini ya jangwa la Sahara ikiwemo Tanganyika kwenye karne ya 15 chini ya wamisionari waliokuwa wanakuja kututawala, kututumikisha na kutuibia mali zetu ikiwa ni njia nzuri ya kutubadilisha kisiasa, kifikra na kitamaduni( wakati wa ukuaji wa himaya ya kirumi), kuenezwa ktk njia zote zilizokuwa zinafanya biashara pamoja na za watumwa.

Machifu na viongozi wetu walikumbatia ukristo kwa sababu ya kujenga urafiki na wazungu au kwa nguvu lakini lengo la wazungu likiwa ni kutubadilisha tuwe na imani kama yao ili tutawaliwe kirahisi kifikra na kiuchumi, biblia wakiishikilia mkono mmoja lakini bunduki mkono mwingine ukifanya masihara nao aliyefanya masihara na hao watakatifu, basi jua kwako imeenda!

Ambacho hakikubadilika ktk ukristo wa leo ni kutawala na upigaji. Mchungaji yuko juu ya kila mtu na hata juu ya familia za watu. Wakiamua wachungaji baba mwenye familia jua kwako imeenda Utakalolisema kama ushauri kwa mkeo atakuchenjia ndani mpaka utakoma hata kama ukiuliza mbona hela zote za familia unapeleka kanisani. Zitapelekwa, mchungaji ataambiwa unakatalia hela na hakuna kuongea na wewe wiki nzima.

Mahubiri mengine ya kitapeli na yanajulikana kabisa huu ni utapeli lakini inahalalishwa na watu na serikali inakaa kimya kabisa watu wakiibiwa, na hata kuingilia maamuzi ya kiafya katika familia za watu kwa maombi yasiyokuwa na miguu wala mikono. Kwa utawala huu walionao leo wananunuliwa magari ya kifahari, wanalishwa mahotelini kifahari, watoto wao wanasomeshwa shule za maana na wengine wanajengewa nyumba za kifalme kutoka kwa waumini wao ambao wengi hata mlo mmoja kwa siku ni shida.

Ukristo kama ilivyokuwa nia ya wakoloni kuja kutupiga na kuzineemesha kiutajiri nchi za ulaya, leo wakati nchi hizo zimeshakuwa matajiri, wachungaji na viongozi wa kidini wamekuwa ni wapigaji wa wananchi tena bila huruma au aibu. Baadae tutakuja kuona wakitosheka kwa kula na kusaza wachungaji ndio watakuwa maraisi wa nchi zetu baada ya mafisadi kuchoka maana ndio wenye hela.

Kwa hiyo mtu asinidanganye kunisomea kifungu hiki cha neno ktk bibilia kinasema hili au lile. Nawajua.
Mnapambania kutukuza utamaduni wa watu weupe niwaamini ili mnitawale kiuchumi na kifikra.

Na mara nyingi hata serikali nyingi za Africa zunajua tunapigwa, ila wanazisaidia serikali nyingi "KUTUNZA AMANI, ILI MAFISADI NAO WAENDELEE KULA KWA AMANI" na sio kwa maslahi ya falimia yoyote. Kama unabisha nitafutie kanisa lolote lili kubwa kama utaona mzee wa kanisa ni muuza mchicha. Cheo chako kanisani kitategemea kitita cha hela kilichoko mfukoni mwako na ndiye utakayekuwa na sauti kanisani.

Wanaitwa mihimili ya kanisa. Wachina wanawapa watoto wao majina ya kichina, wahindi ya kihindi, wajapani ya kijapani lakini usipompa mtoto wako jina la kikoloni basi utaitwa mpagani, neno ambalo nia yake ni kudhalilisha imani za wazazi wetu ili upuuzi wao uendelee kushika mizizi wa kutuibia fikra na mali zetu. Walitutenganisha na wazazi kuwapeleka utumwani bila kujali familia zao zitaishije huko nyuma na leo wachungaji wengine ndio vinara wa kuvuruga familia za watu. Yaleyale. Mvimbishie kichwa mchungaji uone! Kudadeki. Atakuhibiri mpaka masiko yako yang'oke kichwani. Kisa umtii tu. Simtii yoyote!

Kwa leo Ukristo ni kitu kinachosikitisha kukiona!
Ukristo hquna shida, wala kutumia majina ya kizungu sio shida, Taiwan wanatumia ukristo huo huo, na wapo mbali kiuchumi! Tatizo waafrika,dini kwetu ndio suruhisho LA kila kitu, kila tatizo tunataka liombewe!
Ilibidi iwe hv, soma dini, baada ya hapo, ingia kitaa, kufanya kazi, innovation, sayansi, AI nk
 
Nakubali
 
Umeandika stori za vijiweni..nilitegemea ungekuja na vifungu ambavyo ni mapotofu,lakini hujafanya hvyo,badala yake umeandika mambo ambayo ni too general..
 
Mtu mweupe na mwarabu nani bora. Maana kuna mmoja anaishia kujenga misikiti akijitahidi ataweka kisima cha maji kwa ajili ya kutawadha. Lakini kuna mwingine amejenga mashule, mahospitali na vyuo nchini kwetu. Nasubiri Jibu ndugu yangu ?
Hivi wewe umesoma kweli kilichoandikwa au umekimbilia hili swali lilibiased kihisia? Hivi unafahamu kwamba umeshajijibu mwenyewe?

Wote hawana tofauti yoyote, kama ni vizuri iga lakini Dini zao haziwafai wala hazina faida kwa Waafrica.
 
Huu uzi ni evidence tosha kwamba plan ya wakoloni imekuwa successfully kupita viwango. Ukisoma comments za hawa watu ni unabaki kusikitika na kutingisha kichwa tu.
 
Umeandika stori za vijiweni..nilitegemea ungekuja na vifungu ambavyo ni mapotofu,lakini hujafanya hvyo,badala yake umeandika mambo ambayo ni too general..
Vifungu vilivyoandikwa na hao watu anaowapinga? Hivi umesoma hata ulichoandia?
 
Hivi wewe umesoma kweli kilichoandikwa au umekimbilia hili swali lilibiased kihisia? Hivi unafahamu kwamba umeshajijibu mwenyewe?

Wote hawana tofauti yoyote, kama ni vizuri iga lakini Dini zao haziwafai wala hazina faida kwa Waafrica.
Hawana tofauti kivipi huku Ujerumani watu hawaendi makanisani lakini kuna sikukuu nyingi za kikristo. Hoi nchi imejengwa kwa tamaduni za kikristo. Ukiangalia Tanzania kuna mahospitali, shule na vyuo vinavyoendeshwa kwa misaada ya wakristo.
 
Vifungu vilivyoandikwa na hao watu anaowapinga? Hivi umesoma hata ulichoandia?
Nimesoma vyema,huenda wewe ndiye hujaelewa nilichokiandika.
Ukristu hauhusiani na uhuni mnaotaka kuuweka Pamoja nao..
Ukristu siyo Utamaduni wa mtu mweupe, never....
Kama ni msomaji mzuri wa Biblia utagundua kwamba Kristo Yesu alikuja hapa Duniani kutuletea ufalme wa Mbinguni, yote aliyoyazungumza yanapingana kabisa na tamaduni za kizungu,rejea nyaraka za Mtume Paulo zote...alikuwa akiwaonya,kila uchao,kila nyaraka zilikuwa na ole..ikimaanisha kwamba tamaduni za kimataifa haziendani na UTAMADUNI WA UFALME WA MUNGU.
 
Jiwe walilo likataa waashi ndo limekua jiwe kuu la pembeni kwa walio okolewa ukristo wanautambua vyema wewe bado
Limekuwa a stumbling block ( jiwe likwaalo) kwa wale wote wasiotaka kumfuata Mungu , naona kabisa unabii huu ukikamilika kwa jamaa wanaompinga Yesu na Ufalme wake aliouleta hapa Duniani.
Neno la Mungu ni hai,na linadumu milele.
 
Hawana tofauti kivipi huku Ujerumani watu hawaendi makanisani lakini kuna sikukuu nyingi za kikristo. Hoi nchi imejengwa kwa tamaduni za kikristo. Ukiangalia Tanzania kuna mahospitali, shule na vyuo vinavyoendeshwa kwa misaada ya wakristo.

I see, self awareness is a lost ability.
Hawana tofauti sababu intentions za kuleta dini Africa zilikuwa kujifaidisha wao. Wanaita assimilation. Na dini ni product ya culture husika.

Kama ulisoma hii thread ungegundua haiongoelei nani bora kati ya hao mbuzi wawili na dini zao. Bali madhara ya fanaticism kwa Waafrica. Lakini wewe genius umeenda straight kufanya comparison.
 
Nimesoma vyema,huenda wewe ndiye hujaelewa nilichokiandika.
Ukristu hauhusiani na uhuni mnaotaka kuuweka Pamoja nao..
Ukristu siyo Utamaduni wa mtu mweupe, never....
Kama ni msomaji mzuri wa Biblia utagundua kwamba Kristo Yesu alikuja hapa Duniani kutuletea ufalme wa Mbinguni, yote aliyoyazungumza yanapingana kabisa na tamaduni za kizungu,rejea nyaraka za Mtume Paulo zote...alikuwa akiwaonya,kila uchao,kila nyaraka zilikuwa na ole..ikimaanisha kwamba tamaduni za kimataifa haziendani na UTAMADUNI WA UFALME WA MUNGU.

Yeah? Christianity ni utamaduni wa nani then kama sio Europeans? Unafikiri kwanini yesu ni mweupe na wewe ni mweusi?
 
I see, self awareness is a lost ability.
Hawana tofauti sababu intentions za kuleta dini Africa zilikuwa kujifaidisha wao. Wanaita assimilation. Na dini ni product ya culture husika.

Kama ulisoma hii thread ungegundua haiongoelei nani bora kati ya hao mbuzi wawili na dini zao. Bali madhara ya fanaticism kwa Waafrica. Lakini wewe genius umeenda straight kufanya comparison.
Ndugu yangu huku ujerumani ukitoka nchi ya kiislamu una-report uhamiaji kila miezi eita wanakufanyia security check up. Waislamu wa kitanzania wanashukuru kuwa nchi yetu siyo ya kiislamu. Mimi bila ukatoliki wangu nisingefika hapa nilipo. Mimi nongea facts kuna dini ina faida na sisi na zna ubinadamu na kuna dini yenye matabaka hadi huko inakotoka.
 
Usidanganye ujerumani hamna hicho kitu , mimi nimefika mara zaidi ya ishirini tokea 1986
 
Back
Top Bottom