Ukristo ni Uzungu na Uislamu ni Uarabu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Najaribu kuwaza ni kwa nini watu wengi wanaonesha kuwa ili uwe muislam mzuri ni lazima utumie mambo mengi ya kiarabu kuanzia kuvaa mpaka kuongea kwa lafidhi ya Kiswahili cha Kiarabu.

Lakini pia Wakristo wengi nao ili ionekane wewe ni mteule wa mungu uzungu ni lazima uwe ni sehemu ya maisha yako. Siku hizi kila anayejiita "Nabii" au "Mtume" ni lazima pia ajitahidi kuhubiri kwa Kiingereza au aweke mtafisiri wa Kiswahili kwenda Kiingereza.

Hivi huwezi kuwa Mkristo safi bila ya kuitwa Silvanus, Tarchistus, Moses, Jenipher, Peter au Magdalena? Na majina ya Mohamed, Hussein, Jumah, Hidaya, ndiyo alama ya Uislamu. Hivi mtu akiitwa CHANDIMU hawezi kuwa muislamu au mkristo?

Hivi Uislamu ni Uarabu na Ukristo ni Uzungu??
 
Imani ya wafuasi wa Yesu Kristo ililetwa na Yesu mwenyewe, myahudi. Aliendeleza imani ileile ya wayahudi tangu enzi za Abraham.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…