NABII MTARAJIWA
JF-Expert Member
- Sep 11, 2024
- 425
- 609
Hilo Andiko halihusu ukristo. Linawahusu Wayahudi. Wayahudi wana dini yao iitwayo Dudaism. Wao wanafuata Agano la kale. Wakristo tunaishi kwa mujibu wa Agano Jipya. Na kanuni ni hii:Ukisoma biblia, kutoka 21, 10. Inasema
"kama huyo bwana akioa mke mwingine, lazima aendelee kumtosheleza mkewe wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zake za ndoa."
Ukisoma toka mwanzo utagundua kuwa utagundua hapa yamezungumziwa mambo ya kuachia watumwa.. Sipingi hilo, lakini kitendo tu cha kusema kama AKIOA MKE MWINGINE, yule wa awali AENDELEE KUMPA HAKI ZAKE ZA NDOA,
huu ni uthibitisho tosha ndugu zetu mnaruhusa ya kuoa mke wa pili.
Au mimi ndio nimetafsiri hovyo.
Hii ni kwa wale wanangu wa kikristo waliokuwa wanalalamika mambo ya mke mmoja.
Jambo lolote lililoelezewa ktk Agano la kale na Yesu akalisemea tofauti au akatoa Agizo tofauti basi lile la Yesu ndilo linasimama. Yesu ndiye alitoa Agizo kuwa ndoa ni ya mume na mke mmoja tu. Mengine ni dhambi na maovu ndio yansukuma watu. Na wanaofanya hivyo wasahau kurithi ufalme wa Mungu.