Hili andiko linatoka kutoka na hizo ni Sheria za Musa, ukisoma torati utagundua mambo mengi yalikuja kuwekwa sawa na Yesu hapo baadae, kwahiyo torati ni kama haitoshi hivi kukupa jibu la mwisho hadi urudi uone Yesu alisemaje juu ya jambo hilo.
Na kwenye hiko kipengele kilikuja kuwekwa sawa na Yesu.
"Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja" (Mathayo 19:5-6). (Hii ni kama Sheria kwa maana imesemwa na Yesu)
Ila pia kuna bwana mmoja wa kuitwa Paulo ambae alikua mtume nae aliwahi kutoa mapendekezo na kuweka msisitizo wa mtu kuwa na mke mmoja, ingawa yeye alijikita zaidi kwa viongozi wa makanisa (hii sio Sheria ya kimungu ila ni mapendekezo kama hayo ya Musa uliyoyaona kwenye kutoka).
Kwahiyo kabla ya Yesu watu walikua wanaoa watu wengi, kuna mwamba alio wake mia saba na michepuko mia tatu 🤣🤣🤣🤣, na ikumbukwe mimba ya huyu mwamba alitungwa baada ya Daud kumkula mke wa askari wake, kwahiyo ni uzinzi juu ya uzinzi.