Ukuaji wa lugha ya Kiswahili: Neno Mbashara

Hii yako ulitakiwa useme naangalia mpira wa miguu matangazo " mubashara" huku nikiwa tufaa na sharubati mkononi.
Angesema "naangalia mpira wa miguu mubashara huku nikinywa sharubati ya tufani".

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Mpulukio=>ushoroba katika uwanja wa ndege ambapo ndege hupuluka
 

Hapo neno jipya ni "nywila" tu. Kwa Waswahili hayo mengine tumeyakuta na yapo enzi na enzi.

Hujasikia, mbashiri? Basi hata kina Bashiri? Au kubashiri? Yote hayo yanahusiana na neno mbashara.

Sharubati halina upya wala tofaha halina upya ni upunguani wako tu.
 
Neno "mubashara" ni jina la kiarabu la msichana likimaanisha "mleta habari njema". Matangazo ya moja kwa moja kwa kiingereza ni "live broadcast" ambapo ukifasiri kwa kiswahili ingefaa kuwa "matangazo hai".
Wewe ndio miongoni mwa watu mliotafsiri Central Police kama Kituo cha kati cha polisi badala ya Kituo Kikuu cha Polisi
 
Wikipedia wanasema Mubashara na sio Mbashara, yupi yupo sahihi!?
 

Attachments

  • Mubashara - Wikipedia, kamusi elezo_ - https___sw.wikipedia.org_wiki_Mubashara.png
    34.5 KB · Views: 60
Msimbo=code

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio miongoni mwa watu mliotafsiri Central Police kama Kituo cha kati cha polisi badala ya Kituo Kikuu cha Polisi
Tatizo lako ni kwamba unajizuia kufikiri ndio maana umekimbilia kutia maneno kinywani mwangu.
 
Tatizo lako ni kwamba unajizuia kufikiri ndio maana umekimbilia kutia maneno kinywani mwangu.
Sorry mkuu kama nimekukwaza au nimeandika kwa lugha ambayo imekuumiza lakini kusudio langu lilikuwa ni kwamba sio lazima neno litafsiriwe kwa neno kama yaani "live broadcast" iwe matangazo hai ndo nikatoa mfano wa wale waliotafsiri Central police kuwa kituo cha kati badala ya kituo kikuu...otherwise ni majadiliano tu mkuu na sifa yetu wanadamu ni kutofautiana mawazo lakini mwisho wa siku kinapatikana kilicho bora..samahani kwa mara nyingine tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…