Ukuaji wa lugha ya Kiswahili: Neno Mbashara

Ok asante lakini limekua likitumika kama kiungo hivi linawekwa kwenye kila sentensi ndio inanichanganya
Ni kweli neno libamaanisha "live" kutofautisha na "recorded"
Lakini matuizi yake sio yote ni sahihi. Kama vile neno la kiingereza live linavyotumika vibaya mfano "nimeshuhudia live wakigombana", "nataka nikutane naye live", "nimemuona Diamond live akisakata mziki"mataka nikashuhudie mechi live sio kusimuliwa" nk.
Neno "live au mubashara halina maana kama upo kwenye eneo la tukio. Mfano mtu ambaye yupo uwanjani haangalii mchezo "live au mbashara" kwa kuwa yupo kwenye eneo la tukio.
Mbashara au live lina maana au kutumika pale mtu anapoangalia tukio kwenye tv au kusikiliza redio ambapo kuna mbadala wa kuangalia au kusikiliza tukio lililorekodiwa. Kama hakuna option ya kuangalia/kusikiliza tukio liliorekodiwa basi matumizi ya live/bashara yanakuwa hayana maana.
 
Katika hayo maneno uliyoyataja kiukweli mtaani siyasikii hii inamaana kiswahili kinachagua au nikigumu
 
Hili neno bana linaleta ladha flani ukilitamka pekeake ukiliunganisha na maneno mengine sasa linaleta maana unaelewa lakini huwa halivutii
Mimi naona ladha yake ndio inatukosha ila linatumika isivyo
 
mh. unaishi kijijini?
Hili ni neno la kiswahili na linatumiwa na wote wamjini na kijijini af so far Tanzania hii ni wap utapaita mjini ujitofautishe na wengine? Hii nchi mimi binafsi naona mjini na kijijin tofuti ni jina labda
 
Maana yake ni moja kwa moja au live in English ila unatujua watanzania kwa kuchakachua, hata mabasi ya mwendokasi yalileta mapenzi ya mwendokasi, wanja wa mwendokasi, pozi LA mwendokasi n.k inabidi utuzoee watz.
 
Mubashara maana yake ni,,,,live.
 
Hili ni neno la kiswahili na linatumiwa na wote wamjini na kijijini af so far Tanzania hii ni wap utapaita mjini ujitofautishe na wengine? Hii nchi mimi binafsi naona mjini na kijijin tofuti ni jina labda
ok nimekupata
 
Hebu leo niliseme hili, jamani vyombo vya habari kabla ya kundika neno basi wawe na uhakika nalo na kuelewa matumizi yake.

Kuna neno liitwalo MBASHARA ambalo maana yake inayorushwa moja kwa moja au kusikika au kuonwa kwa waakti huohuo. Mara nyingi kupitia matangazo ya redio au televisheni.

Yaani kama vile unaangalia mpira muda huohuo unaochezwa hii ni mbashara, kwa kingereza inaitwa 'LIVE', kipindi chochote kitakachooneshwa moja kwa moja ni Mbashara. Hii ndo maan halisi ya neno hilo.

Ila hivi sasa nashangaa kuna makundi ya watu wameibuka na neno MUBASHARA badala ya MBASHARA sijui wamelitoa wapi hili, vyombo vya habari wanalitumia hilo kwa maana tofauti. Yaani chombo cha habari kutumia neneo jingine kinyume na neno halisi tena kinyume na muktadha wake.

Si uharibifu wa lugha huu?
 
Katika Neno la Wiki hii na eno mbashara na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Onni Sigalla anazungumzia maana ya neno mbashara ambapo anasema, ni kipindi kinachorushwa hewani moja kwa moja na kusikika au kuonwa kwa wakati huo huo aghalabu kupitia matangazo ya redio na televisheni matumizi yake unaweza kusema, Kipindi mbashara cha televisheni kitarushwa saa moja usiku.
 
hilo neno ni 'mubashara' sio 'mbashara' na limetoholewa kutoka arabuni wao wanatumia 'mubasher'
 
Hao BAKITA nao wamejichokea kabisa. Bado tunatohoa maneno ya Kiarabu mpaka karine hii!? Nilidhani kwa usomi wao wa Lugha pamoja na tafiti mbalimbali za lugha zetu za asili wangeweza kupata neno safi na tamu kutoka kwenye asili yetu. Sijui hawa wasomi wetu vipi.
 
Habari zenu wana jamvi?
Kama kichwa kinavyo jieleza hapo juu, kwanza ningependa kutoa pongezi za pekee wa taasisi zinazojihusisha na ukuaji na ueneaji wa kiswahili Cc TUKI & BAKITA
Lalamiko langu kuu ni maana ya neno mubashara na matumizi yake maana imekuwa kero sasa kila kitu ni mubashara kuna kituo kimoja maarufu cha luninga hapa nchini kimekuja na kampeni katika msimu huu wa wapendanao wanaiita MAPENZI MUBASHARA
Nadhani neno mubashara lina maana ya LIVE kwa lugha ya kwa malikia
Unaposema mapenzi mubashara unakuwa una maanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…