Nashukuru kwa kunielemisha. Lakini tukubali ukweli mmoja kuwa maneno ya lugha nyingine huingia na juanza kutumika kwenye lugha nyingine kurokana na mazoea. Sio kwa kulazisha neno la lugha nyingine ambalo halitumiki popote na kulifanya neno rasmi.
Kutokana na ujio wa luninga, na kuanzishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga na kwa sisi uelekeo wetu na mazoea ni kiingereza na neno la kiingereza linalotumika na tunaloliona ni LIVE, na kwa kuwa neno hili lina tafsiri rasmi ya kiswahili, HAI. Basi ingekuwa rahisi tu kugeuza neno LIVE na kuwa HAI. Kwa mfano ni rahisi kusema "tunawaletea matangazo hai ya mpira kutoka uwanja wa Kirumba..." kuliko kusema ".....matangazo mubashara..."
Kunyumbulisha tafsiri kutoka maneno ya lugha nyingine ambayo hayakuzoeleka kwa kiswahili ni kukifanya kiswahili kuwa kigumu zaidi.
Kutokana na hili ndio maana sio vituo vingi vinatumia neno hili.