Ukuu wa Dollar ya Marekani umefika mwisho?

Uliuliza kama kuna nchi zinajaribu kuachana na dola kwa sasa nikakujibu. Hujalitilia maanani jibu, umequote unachojua wewe. Inaonekana wewe ndiyo unataka ubishi, huwezi kusoma majibu na kuelewa au ujuaji tu.

Tukirudi kwenye mada. Hizo nchi umetaja hazijawahi kujaribu kuachana na Dollar. Baada ya WWII Marekani alihakikisha Ujenrumani na Japan zinakuwa imara kichumi ili ziiserve dollar kwenye maeneo yao, yaani Ujerumani Ulaya(Kumbuka Ujerumani "Ndiyo EU") na Japan Asia. Hizo nchi hazijawahi taka kuachana na dollar. Waliojaribu walau ni Ghaddafi na Saddam Hussein. Na tunajua kilichowapata. Kazi kubwa ya jeshi la Marekani ni kuilinda Dollar.

Kwa sasa harakati za nchi kutaka kuachana na dollar zina nguvu sana, nimekuwekea harakati hizo hapo juu(Sijui kama umesoma).

Unaweza kutuambia kwa nini dollar ni reserve currency ya dunia pamoja na manyanyaso yote ambayo dunia inapitia?
 
Ni factors gani zingine zinazofanya dollar iwe na nguvu?
 
Amekumbuka shuka kumekucha. Ameanza kujenga miji iwe kama Dubai kwa kupanic. Mara Noem, Mara The Cube nk nk.
 
Ni factors gani zingine zinazofanya dollar iwe na nguvu?
1. Uchumi: Marekani ina uchumi mkubwa na wenye nguvu zaidi duniani. Ukubwa wa uchumi huu unafanya dola kuwa fedha ya kipaumbele katika biashara za kimataifa.
2. Marekani ina masoko makubwa ya fedha kama vile soko la hisa la New York (NYSE) na soko la Nasdaq. Haya masoko yanavutia wawekezaji kutoka kote duniani, na hivyo kuongeza mahitaji ya dola.
3. Benki kuu za nchi nyingi duniani zina akiba kubwa ya dola kama sehemu ya akiba yao ya fedha za kigeni hivyo inafanya dola kuwa na mahitaji makubwa na kubaki kuwa imara.
4. Marekani ina historia ya utulivu wa kisiasa na kiuchumi ikilinganishwa na nchi nyingine. Hii inaongeza imani ya wawekezaji na nchi nyingine kutumia dola kama fedha ya akiba.Hili nalo ni muhimu sna.
Na pia Marekani ina mfumo mzuri wa kisheria unaolinda haki za mali za wawekezaji. Hii inawafanya wawekezaji wengi kupendelea kutumia dola kama fedha ya kipaumbele.
Kuna vipengele vingi tu pamoja na hicho cha mafuta.. Jaribu hata ku-Google utapata picha halisi kwa upana zaidi..
 
Ndio. zipo nyingi kwa sasa zinazo punguza matumizi tofauti na awali hii ni dalili ya miaka ijayo nini kitatokea.
 
Ukitka kununua MRI toka USA utatumia pesa ya Saudia? Dola ina nguvu kwa sababu ya industrial productions ambazo zinahitajika duia nzima.
Industrial products hazipatikani U.S.A pekee kwanza U.S.A sio industrial powerhouse kwa sasa duniani hiyo nafasi imechukuliwa na China miaka mingi iliyopita labda ulete sababu tofauti na hii.
 
Hiyo 1-3 ni matokeo ya pesa yao kuwa pesa ya dunia, si mambo yaliyofanya pesa yao kuwa pesa ya dunia. 4 ni kweli inautulivu wa kisiasa lakini si salama kwa mali za wawekezaji, ndiyo maana imefreeze pesa za Urusi. Imefreeze pesa za Taliban. Na haya ndiyo yanafanya watu wengi waharakishe kuikimbia.

Sababu kubwa ya kuifanya pesa ya nchi fulani iwe pesa ya dunia ni nchi hiyo iwe na trade surplus(Yaani iuze sana bidhaa duniani huku ikinunua kidogo tu) Marekani ilipoteza sifa hiyo miaka ya 70. Tokea hapo dollar imebaki kuwa reserve ya nchi nyingi kwa sababu ya ujanja ujanja na ubabe tu.
 
Aisee ndyo nyie tuwaitaji kweny nch zetu syo hawa kama mleta mada ajui power ya 💵 anakurupuka tu ebu mkuu wape elimu hao watt wa mama ezakuwa ajui biashara sasa mmarekan yy kwa waza miaka 400 alaf unakuta mtu kavmbiwa makande anakurupuka kutowa mada ajui hata kwann dollar ipo dunian kote
 
Industrial products hazipatikani U.S.A pekee kwanza U.S.A sio industrial powerhouse kwa sasa duniani hiyo nafasi imechukuliwa na China miaka mingi iliyopita labda ulete sababu tofauti na hii.
Industrial products ya chna iz zakna vunja bei au ip mkuu unazozungumzia ?
 
Namba 3 na 4 kuna mtikisiko mkubwa hapa sikubaliani na wewe kwa sasa.

Namba 1 na 2 kuna uimara
 
Kama unaangalia mambo namna hii, tena kwa kupingana na sababu za kitaalam kabisa, basi una haki ya kuja na conclusion kama uliyoainisha kwenye thread yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…