Haujanibana kwa hoja, umeongea tu points za kukariri, unachosha hata kukujibu.
Unadhani watu wanatumia dollar kwa hiari yao? Pesa yako kuwa pesa ya dunia kuna faida kubwa sana. Ndiyo maana Marekani anahakikisha anapambana na yeyote anayehatarisha hilo. Libya, Iraq, Iran na Venezuela walikataa kuuuza mafuta exclusively kwa dollar ndiyo maana US anawasakama.
Kuanzia miaka ya 1970 ukubwa wa Dollar unasababishwa hasa na matumizi yake kama pesa pekee ya kuuzia mafuta. Ndiyo maana kuna neno petrodollar. Toka US alipoacha kuwa muuzaji zaidi duniani na alipoachana na gold standard njia pekee inayoisimamia dollar yake ni petrodollar.
Unafikiri Marekani hazalishi mafuta? Hapa si kuzalisha au kutozalisha mafuta, ni kuwa hayo mafuta yananuliwa kwa sarafu ipi. Hilo ndilo la msingi kama unataka kuelewa hoja iliyopo mezani.
Hoja zako nyingine kama mikopo kuwa kwa dollar ni matokeo ya nguvu ya dollar na si sababu zinazofanya dollar kuwa na nguvu.
Kinachotafutwa na wengi si mbadala wa dollar kama sarafu-akiba. Kwamba pesa ya China ibadili kuwa sarafu-akiba. Kinachotafutwa ni uhuru wa kutumia sarafu zingine. Mfano Iraq, Iran, Venezuela, Saudi Arabia nk nk waweze kuuza mafuta yao kwa Euro, Renminbi, Rupia nk nk. Au kupatikane sarafu ambayo haiwi issued na nchi moja na hivyo kufanya inyonye zingine.