Ukuu wa Dollar ya Marekani umefika mwisho?

Ukitka kununua MRI toka USA utatumia pesa ya Saudia? Dola ina nguvu kwa sababu ya industrial productions ambazo zinahitajika duia nzima.
Ndo wangekuwa wanasumbuka na Russia ,China,Iran,Cuba,Venezuela na North Korea?Embu weka taarifa yako vizùri.
 
United States has a significant supply of fuel, It is one of the world's largest producers of crude oil and natural gas.
 
labda tuiweke hivi ....Kama mauzo ya bidhaa kwa dollar itapungua ndo kusema thamani yake itakuwa ileile kama 1970.
 
Tatizo lako umekaririri soga za maskani...
Libya na Iran hatakama wasingeuza mafuta kwa Dollar,still wangehitaji hazina yake kwa manunuzi ya Vipuli ya Sekta hiyo ya mafuta,delta ya Kompyuta, aviation na Mashine kubwa ambapo USA bado ana dominate.
 
Tatizo lako umekaririri soga za maskani...
Libya na Iran hatakama wasingeuza mafuta kwa Dollar,still wangehitaji hazina yake kwa manunuzi ya Vipuli ya Sekta hiyo ya mafuta,delta ya Kompyuta, aviation na Mashine kubwa ambapo USA bado ana dominate.
Daah
 
Hakuna nchi inayopangiwa aina ya fedha ya kutumia...ila bila kuwa na one currency kama world reserve, ina maana...
  • Nchi zetu ziwe na akiba ya pesa zaidi ya tano au kumi.
  • Na nchi zenye kutegemea viwanda zitaanguka kiuchumi...
Ujifunze kuhusu uchumi wa dunia unavyoenda acha story za mtaani..
 
Bado unasafari ndefu kujua mambo yanavyoenda. Hapa siyo nani ana mafuta mengi, hapa ni pesa ipi inatumika kununulia hayo mafuta.

Na hao wanatumia nini kununua vitu toka USA? China ni biggest exporter toka 2009, USA comes in 2nd story hizi hizi zilianza ila hadi Leo dollar ipo pale pale, what's new now?

Nenda kaangalie kama kuna mkopo wowote umeandikwa kwa yuan ulete majibu. China wenyewe wanataka dollar.
 
Bado unasafari ndefu kujua mambo yanavyoenda. Hapa siyo nani ana mafuta mengi, hapa ni pesa ipi inatumika kununulia hayo mafuta.
SA ana mikopo? Anailipa kwa kutumia sarafu gani?
 
Kufa kwa dollar kupo palepale Sababu dunia inabadiika watu au njia zilizokuwa zinatumika kuiimarisha dollar Enzi hizo kadri siku zinavyoenda zinapugua na zingine zinakosa nguvu mambo mengi yanabadilka kwa maana hyo USA Alishasoma mchezo kuwa haya makaratasi dollar kuna siku yatamuangusha ss akaja ni mbinu mbadala ndo hii kitu inaitwa BITCOIN ni mbadala wke na ameshafanikiwakwa hilo lkn kuna vitu kwenye bitcoin havijakaa sawa kuna mbadala mwingine tena unakuja kwa mfumo wa Bitcoin unaitwa Pi networks hyo yote kuhakikisha anaendelea kuwa juu
 
Kilichopo ni kuwa Saudi Arabia imekubaliana na Marekani kuuza mafuta yake kwa Dollar. Ndiyo maana huoni watu wakitafuta pesa yao kwenda kununua mafuta. Lakini leo wakisema wanauza mafuta yao kwa Riyal unafikiri ni wangapi wataanza kuisaka hiyo pesa?
Saudi Arabia sio mzalishaji pekee wa mafuta duniani kwa sasa. Mexico, Canada, Iraq, UAE na Brazil ni wazilishaji wengine muhimu sana kidunia.
 
Saudi Arabia wanasita kusaini mkataba wa Petro dollar. Kuna harakati nyingi sana za watu kutaka kuachana na dollar.
Hakujawahi kuwa na mkataba uliosaniwa wa petrodollar kati ya Marekani na Saudi Arabia. Achana na fictions na porojo.
 
Kitendo cha akiba ya dollar za Russia kuwa frozen kimewafanya watu wengi waanze harakati za kuikimbia dollar.
Ni bora huko Marekani ambapo waki frozen akiba unaona utaratibu wa kitaasisi uliofuatwa kufikia hayo maamuzi. Sasa jichange ukaweke akiba zako za fedha Russia au Saudi Arabia ambapo mtawala anaweza kuamka tu amegombana na mke wake akazikomba zote.
 
Wew umeshaawahi kuona mlalahoi ananunua dawa kutoka usa au ulaya ..cipro ya denk inauzwa kati ya 3600-4000 ya kwetu inauzwa 200 .
 
zote ni underlicence ya USA , kama hujui jua hilo maana patents bado ni za USA, ndio wagunduzi huwezi kuzitengeneza bila ruhusa yao kimataifa.
I stand to be corrected!
Siyo kila kinachotengenezwa kutoka viwanda vya china ni underlicence ya USA vinginevyo hukusoma kabisa au umeamua kujizima data
 
keep on dreaming
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…