Uchaguzi 2020 Ukweli ambao wana CCM hawataki kuusikia: Magufuli hatashinda Urais Uchaguzi Octoba 2020

Uchaguzi 2020 Ukweli ambao wana CCM hawataki kuusikia: Magufuli hatashinda Urais Uchaguzi Octoba 2020

Niwaambie tu kuwa hata Mobutu alisifiwa sana kwenye utawala wake , waliomsifia walikuja na sababu lukuki.
Huenda Magufuli amefanya mengi mazuri kuliko hata Mobutu.

Hata yule aliyekuwa Rais wa Malawi walimsifia sana na wapo walioamini kuwa aliyoyafanya yatampa kiti tena kwa mara ya pili.

Mifano ni mingi, muda ni mchache. Kama vile waliomfyatulia risasi Tundulisu walijua tayari kinachofuata ni mazishi tu lakini ikawa tofauti.

Ile nguvu iliyomfanya Lisu awe hai pasi watesi wake kutarajia, the same power ndio itakayomkalisha Lisu madarakani kwenye uchaguzi ujao.

Tutaukumbuka utawala wako Mhe.
Kujenga barabara , kujenga flyover na madaraja sio kabisa kigezo cha kuchaguliwa kuwa rais na wananchi , wakoloni walifanya mambo makubwa zaidi ya hayo...Walichokosea wakoloni walikuwa hawawapi uhuru wananchi ,waliwatesa ,walipewa ajira za kitumwa(kulima plantations) etc

Wananchi wanataka uhuru ,kwasasa uhuru hakuna watu wanaogopa kuandika chochote kwenye mitandao ya kijamii maana kuna sheria kibao za kumziba mwananchi mdomo waliojaribu kusema waziwazi tumeona kina lissu walivyopigwa risasi 38 huku 16 zikiingia mwilini ,tumeona wapinzani walivyofungwa etc

Kutawala bila kufuata katiba/sheria:- Tumeshuhudia mtu firani akitoa maneno ambayo yanaenda kinyume na katiba kuzuia mikutano ya kisiasa kwa wapinzani huku chama chake kikifanya siasa saa 24 huku kikilindwa na dola ,tumeshuhudia vyama vya upinzani vikinyanyaswa na mamlaka ya usajiri na hatujwahi kusikia hata siku moja SISIEMU kikiandikiwa barua na msajili kitoe maelezo.

Tumeona kwa miaka mi5 hakuna nyongeza yeyote ya mishahara kwa watumishi wa umma kinyume na sheria za kazi/utumishi wa umma unavyotaka kwamba mfanyakazi anakuwa entitled na nyongeza ya mishahara kila mwaka,tumeshuhudia watu wanapandishwa vyeo lakini hakuna nyongeza ya mshahara.

Uchumi kupiga mweleka,katika kipindi cha huyu bwana tumeshuhudia uchumi wetu umeipga mweleka kwa kiwango cha SGR ,haihitaji rocket sayansi katika hili,maduka mengi yamefungwa ,biashara nyingi zimefungwa ,masoko ya bidhaa nje zimeshuka, uwekezaji umeshuka.

Kunayanyasa wafanyabiashara wakubwa:-Katika kipindi cha huyu bwana tumeshuhudia wafanyabiashara wakubwa wakipitia kwenye mkono wa chuma ,Mo kutekwa na genge la Bashite na kisa kuchotwa mabilioni kama ransom ,tumeshuhudia manji kufungwa na figisu za hapa na pale mpaka kupelekea Qaulity Group kuwa magofu ya kale na soko la mbaazi kushuka kutoka elfu 3 kwa kilo mpaka Tsh 100 , Lema Northern engineering alifungwa tu baada ya mtu kurani kuingia madarakani na kuchotwa mipesa.

Mambo ni mengi sana tunayaacha kwenye kampeni kupiga pini pesa za nssf/ppf ,kuweka kikotoo kipya etc ukifanya mambo ya hovyo yanayoguza/athiri maisha ya wananchi hakika hakuna atakayekupenda hata ujenge lami hadi milangoni na flyover hadi chumbani.
 
Vyombo Hivi Vitakuwa Wapi Mpaka Asishinde:-
1.TISS
2.PCCB
3.TPDF
4.POLICE
4.PRISON
5.IMMIGRATION
6.FIRE
7.MADAWA YA KULEVYA
😀😁😅😄😃😂

😶🤨😏
Hivi hiyo TPDF, bado kirefu chake ni Tanzania people's defend force au ni Tanzania presedent defence force
 
Magufuli Ni malaika, ndio maana hata ndani ya CCM printer ziligoma ku print form zaidi za utais.
Sasa aje huku ashindane na wanadamu na mashetani, asitumie polisi, TISS, JWTZ wala tume ya uchaguzi, tume iwe huru, wazi na ya haki, atagaragazwa saa moja asubuhi October 28,2020
CCM imekuwa kama Dini Kwa wengine. Ila kuna wasioenda Ibadan Na hasa vijana Na shida zao. Lolote laweza kutokea
 
Kifo hiki ni mpango wa Mungu. Maana ndiye aliyekuwa anategemewa kulazimisha matokeo. Hata 2015 kule Zanzibar ndiye aliyemwamuru Jecha kufuta uchaguzi. Sasa mbabe kafa na uhuru soon utapatikana iwe kwa jasho au damu.
Kwa hiyo watanzania wote 55 milioni tulikuwa tunamuogopa mkapa tu? Please be serious kidogo
 
Hata 2015 mlituambia "Now or Never"

Huyo jamaa yenu hata ndani ya chama tu mpaka sasa katolewa ulimi na Nyalandu, sijui huo uhakika nnautoa wapi kuwa yeye ndiye mgombea.

Ukweli ni kwamba,wanaCCM hawawazi urais 2020 bali target ni kuchukua majimbo yote.
 
Niwaambie tu kuwa hata Mobutu alisifiwa sana kwenye utawala wake , waliomsifia walikuja na sababu lukuki.
Huenda Magufuli amefanya mengi mazuri kuliko hata Mobutu.

Hata yule aliyekuwa Rais wa Malawi walimsifia sana na wapo walioamini kuwa aliyoyafanya yatampa kiti tena kwa mara ya pili.

Mifano ni mingi, muda ni mchache. Kama vile waliomfyatulia risasi Tundulisu walijua tayari kinachofuata ni mazishi tu lakini ikawa tofauti.

Ile nguvu iliyomfanya Lisu awe hai pasi watesi wake kutarajia, the same power ndio itakayomkalisha Lisu madarakani kwenye uchaguzi ujao.

Tutaukumbuka utawala wako Mhe.
Mbaya zaidi Msafisha Njia Wake Hatunae!!Pumzika Kwa Amani Mzee Wetu BWM.
 
Vyombo Hivi Vitakuwa Wapi Mpaka Asishinde:-
1.TISS
2.PCCB
3.TPDF
4.POLICE
4.PRISON
5.IMMIGRATION
6.FIRE
7.MADAWA YA KULEVYA
😀😁😅😄😃😂

😶🤨😏
Hivyo vyombo sio malaika, bali vinaundwa na wanadamu wenye ukomo katika kufikiri na kutenda.
 
Hao ni watu na wao wana familia. Kama watafanya ubabe kuilinda ccm waziwazi, basi kutakuwa na umwagikaji damu na hapo ndipo ule uhuru utakapopatikana. Sababu inaweza tokea vita ya person to person maana wengi tunajuana

Mr Nditolo, you have very strong wishful thinking, hopefully you are student or recent Graduate. Nchi yeyote inapokaribia kwenda kubadilisha watawala huwa kuna ambiancy fullani hivi ambayo hujitokeza. Magufuli kwa mwaka huu tumekwisha mkosa, anagalagaza tuu upinzani.

Ila siasa za kweli zipo kuanzia 2020 mpaka 2025, bahati mbaya tumekwisha poteza askari wa vyeo vya juu wengi mnoo. Na hapa CCM bado wapo hatua ya nne tuu kati ya hatua 11 za kumshugulikia Hasimu/mpinzani wako wa kisiasa

Wako hatua ya Nne ya sheria ya kumshughulikia Chama pinzani na Shindani katika sheria 11 za kumaliza upinzani. Sheria hizi hufanya kazi mara baada ya kushinda uchaguzi. Hufanya kwa kidodo kidodo ili mahasimu wasichanganyikwe. (sababu mkifanya haraka na wakachanganyikiwa wanaweza kusababisha kupotea kwa amani na utulivu katika nchi )

1) Adui yako wa kisiasa unatakiwa umpige sana achakaye kiasi ambacho hata atakapo pata nafasi ya kujibu mapigo, mapigo yake yawe dhaifu sana kiasi ambacho anakuwa hana madhara kwako.

2) Wakati wa mashambulizi ya kisiasa, hakikisha Magenerali ( wakuu wa vyombo vingine vya utendaji wa chama chako wako imara na wakiendeleza mashambulizi na kutoa kipigo maeneo yote ambayo hasimu wako wa kisiasa anaweza kupata usaidizi, au kukimbia au kuepuka mapigo kabla hajapigwa sana na kuchakazwa. ( kukimbia ni moja ya mbinu za kupigana vita)

3) Hakikisha unavunja nguvu za hasimu kwa kiasi kikubwa sana kupitia kuwanyong'onyesha Viongozi wake ambao wana nafasi ya kungundua mapambano ni makali. Hakikisha wanachama wanatenganishwa na viongozi wanao weza kugundua mapambano makali na kijikusanya tena. Ondoa akili bakiza makapi ili waendelee kupoteana.

4) Tumia vyombo vyote vya imani ( faith based) kwa kupitia kivuli na sio moja kwa moja ilI uendelee kuwapiga kwenye nyoyo zao ili wawe waumini wa unayoyataka na pia watiifu kwa mamlaka.

NITAWAPA SHERIA 7 ZILIZO BAKI KWA DOZI KIDODO KIDOGO ( THE ART OF POLITICAL WAR AGAINST THE VANGUISHED). KARIBUNI.

Wapinzani elimikeni siasa Za ubobezi ni sayansi, ELIMIKENI ACHENI UFUASI MFUU.
 
Kifo hiki ni mpango wa Mungu. Maana ndiye aliyekuwa anategemewa kulazimisha matokeo. Hata 2015 kule Zanzibar ndiye aliyemwamuru Jecha kufuta uchaguzi. Sasa mbabe kafa na uhuru soon utapatikana iwe kwa jasho au damu.
Utakuwa tayari kupigwa risasi ya kichwa? Au unazogoa tuu
 
Hao ni watu na wao wana familia. Kama watafanya ubabe kuilinda ccm waziwazi, basi kutakuwa na umwagikaji damu na hapo ndipo ule uhuru utakapopatikana. Sababu inaweza tokea vita ya person to person maana wengi tunajuana
Eti kumwaga damu, upo tayari kupigwa risasi ya kichwa?
 
Ninachokumbuka SPEPTEMBER 2015:
Matokeo

Soft copy
Lowassa =========> 80%

Magufuli ==========> 20%

Hard copy

Lowassa ==========> 39.97%

Magufuli ==========> 58.46%

Makelele ya Tanzania Uswahili shida
 
Hakushinda, maana tulimiminika kwa wingi kwenda kumpigia kura manvi, pamoja na madiwani na mbunge. Kituo changu cha Forest Mpya Mbeya hakushinda ndio maana hata mbunge wetu alikuwana kura nyingi kuliko mbunge yoyote pamoja na rais wa zanzibar.
uyo diwani sasa akaunga juhudi
 
Magufuli Ni malaika, ndio maana hata ndani ya CCM printer ziligoma ku print form zaidi za utais.
Sasa aje huku ashindane na wanadamu na mashetani, asitumie polisi, TISS, JWTZ wala tume ya uchaguzi, tume iwe huru, wazi na ya haki, atagaragazwa saa moja asubuhi October 28,2020
Tume iliyonunuliwa nyumba mpya Dodoma?
 
Back
Top Bottom