Ukweli gani mgumu umekubaliana nao baada ya kuwa mtu mzima?

Ni kweli, mwanamke wa kujipigia tu ni rahisi, hata kwetu wanawake ni rahisi sana kuwapata nyie.
Ugumu ni kumpata yule ambaye unampenda/anakupenda au mwenye vigezo unatafuta.
Ugumu ni kumpata yule ambaye unampenda/anakupenda au mwenye vigezo unatafuta.
...hawapo tena walimalizika enzi zetu.....pole kwa kizazi hiki.
 
Somo zuri sana..Hongera Mama..
Asante baba πŸ™πŸ½
Hebu ni dadafulie namba 5 na 7.
Sawa
5. Pesa haitakupa furaha ila itakuheshimisha na kukurahisishia maisha.
Pesa peke yake haitakupa furaha, kama una upweke, utabaki kuwa mpweke, kama hufurahii kazi yako au mahusiano yako, hakuna kiasi cha fedha kitakufanya ufurahie.

Ila pesa inaweza kukutimizia mahitaji yako, ikakupa status kwenye jamii, ukaheshimika, ukathaminika kwa sababu ya kile ambacho unacho. Ndiyo maana unakuta mtu aliyekusanya marafiki au watu sababu tu ya pesa, yeye ndiye mlipaji, watu wanakuja kwake wapate mteremko na si kwa sababu wanampenda au kumfurahia kwa vile alivyo, pesa zikiisha wote wanaondoka.

Furaha inapatikana kwa kufanya kitu unapenda au kutoka kwa jamii au watu unaowapenda au wanaokupenda. Pesa inaweza kukurahisishia michakato ya kuwa nao karibu au kuweza kutatua matatizo yao ila ule upendo na thamani ya kweli lazima viwepo kwanza ndiyo pesa ije juu yake.

7. Familia ambazo wazazi wetu wanatokea (wajomba, mababa wakubwa, mama wadogo, mashangazi etc.) ni watu wa kuishi nao kwa busara sana au kukaa nao mbali.
Entitlement na kutojua mipaka.
Ndugu wengi huwa wanataka kuingilia maamuzi ya ndugu zao, nimeona cases za ndoa kuwa ngumu sababu ya ndugu, wengine wanahamia kwa ndugu hawaondoki, wapo wanaotegemea matatizo yao yatatuliwe kila wanapohitaji etc.

Kuna wakati kazi yangu iliniweka kwenye nafasi ya kuona kesi nyingi za mirathi, hapa ndiyo niliamini adui wa kwanza anaweza kuwa ndugu yako. Mambo ya kudhulumu mali, kuonea watoto wa marehemu etc, ni mengi sana.

Kama unaweza kuchukua tahadhari mapema, weka sawa mazingira ya watoto wako na usije kutegemea ndugu yako atakusimamia utakapoondoka.
 
;Msaada sio haki yangu.
Ni kweli πŸ“Œ
Namba 4. Mwaka umepita sasa hakuna siku nalala nisimkumbuke dada kuna muda ni ndoto bado . sometimes napiga namba yake inaita adi inakata..
Pole sana, maumivu na uchungu ni malipo ya upendo wetu kwa wale waliotangulia.

Nakuombea upate ahueni na faraja πŸ™ !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…