Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Jipe moyo tu mzee baba ila nikwambie ukweli tu kwamba kilimo cha kibongo walanguzi na madalali ndio wanaopiga hela πŸ˜‚
Na huu ndo ukweli nakumbuka kuna mtu alipeleka maembe kiwanda fulani cha juice, kufika tu pale madalali hao kumbe pale kiwandani kuna madalali ambao wao ndo wana connection za kuuza maembe mle kiwandani basi jamaa akagoma kuwapa madalali mzigo wakamwambia utaona, jamaa kuongea na afisa manunuz afisa akamwambia malori ya matunda yana foleni zake hivyo asubiri wiki nzima ndo na yeye atapewa kuingiza maembe yake auze jamaa akasubiri aisee wiki imeisha na embe zimeanza kuiva kupitiliza muda huo woote madalali wanazengea jamaa alegeze msimamo jamaa kumcheki tena afisa manunuzi afisa akamwambia asubirie tu dah jamaa ilibid alegee tu mwenyewe akawapa madalali tena kwa bei ya kutupa tu na ndo ikawa mwisho wa kilimo cha embe
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Kuna siku niliona video clip inasambaa watsup ya RC wa huko Njombe akiwashawishi wale diaspora sijui wanaishi marikani wale kwamba ndani ya mkoa wake Kuna fursa kubwa sana ikiwemo ya kilimo cha parachichi pia viwanda ambavyo vinanunua kwa bei nzuri mno. Sasa sijui wale diaspora walishannua maeneo kwa ajili ya kilimo cha hizo Hass, dah Sema yule RC ukimsikiliza ni pure joy to listen he's talented ana power ya ushawishi, maana alivyouongelea mkoa ni kama wana land use planning nzuri sana hopefully hii ya kg 1 kwa 500 haitawapata diaspora wetu.
 
N kweli lakn nao wanalalamika sahz Bei imekuwa changamoto
 
Mkuu wa mkoa njombe anajitahidi sana kufanya uhamasishaji wa mazao mengi yanayositawi katika mkoa wake mfano Ngano, parachichi, chai , pareto, kahawa, pamoja na miti changamoto ni mifumo jumuishi ya masoko na mikataba ya kuaminika Kwa wakulima wake Kwa baadhi ya mazao
 
Kuna watu kibao wametelekeza mashamba. Usipokua na hela usilime parachichi
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Wakuu wa Mkoa na halmashauri wanajua mchezo wanaofanya. Wanunuzi toka Kenya wanahonga sana.

Umaskini wa Mtanzania ni watawala
Wakulima wekeni umoja mtashinda achaneni na vikao vya halmashauri vya kuwadanganya.

Wanajua mchezo mchafu
Kila anayepelekwa Njombe akiondoka anaondoka millionea.

Watawala acheni kuumiza Watanzania mkawatajirisha WaKenya

Waziri hili linakuhusu ingilia kati

Mfikishieni ujumbe Waziri wa Kilimo

Mnacheza na akili za WaTanzania vile mnataka

Parachichi linauzwa China Europe lina label ya Kenya kumbe ni zao na Tanzania

Wakenya acheni mchezo wenu mchafu.

Njombe fukuzeni wanunuzi wooooote tangazeni kama tenda wakulima woooote bei iwe moja elfu 3 kilo hutaki sogea
 
Tatizo ni aidha Tanzania haina soko la kimataifa kuuzia au maparachichi ya Tanzania hayakidhi viwango.
Sababu haiwezekani Mexico inaelemewa na mahitaji ya soko la parachichi kutoka Canada na US kwa kushindwa kukidhi mahitaji na mpaka Drug Cartels wameaanza kujihusisha na hii biashara ya parachichi kwa jinsi ilivyokuwa na faida.
Halafu huku kwetu tunalima na kulamimika ni zao halina faida
 
Wakigomea kununua hayo maparachichi,wakulima watayapeleka wapi?
 
Tangantika atakwambia yeye ana mbinu. Mimi niliwaonya nikaondoka zangu
Nipo hapa nimerudi jukwaani nilikiwa likizo. Wabena waache wapigwe za USO. Mwaka jana wameniibia miti yangu kama ishirini yenye umri mkubwa pumbabu zao. Mwaka huu wameuza parachichi sh. 200 naomba mungu waendelee kupigwa mpaka waisome namba waache wizi. Wanapata laana ya wizi. Wanatabia ya kuchoma moto hovyo.
Mimi mtoto wa mjini husler sintauza AVOCADO SH 200! Yaani mimi mtoto wa uswazi nikalime BUSH avocado halafu niiuze kwa 200 ! Mimi nina plani yangu, parachichi zangu bado haziijaanza labda mwakani nipo eneo la barafu napambana nakujaribu kufanya innovation mbali mbali kuepusha barafu isiue miti.
By now siwazi kuhusu bei wenye parachichi watajiju. Wakulima waache waendelee kupigwa tu ili wakate tamaa.
Mimi nina PLAN.
 
Ogo tata pole sana .
 
Shamba liko wapi mkuu nifike kukutembelea
 
Sisi wakulima wa mjini tuliaminishwa eti miaka mitatu tu umeshatajirika, tukaambiwa na vanilla sijui aise
 
Shamba liko wapi mkuu nifike kukutembelea
Mkuuu shamba bado. Nipo kwenye ZONE ya barafu na vijana niliwaachia ni wajinga wasio na vision. Lipo Njombe.
Kununua ardhi njombe ni kamali unaweza pata "frost zone" ukaisoma namba. Shamba lilikuwa la PILOT project ili nipate uzoefu nikapande kubwa. Nafikiria kubadili project sitaki mambo ya AVO yanachangamoto nyingi. Mimi bei sioni kuwa ni changamoto kubwa ila kupata matunda ndio mziki. Kuna jirani yangu yeye imekula kwake zaidi ya miti 500 kupigwa barafu, kijana alileta ubishi wa kufunikia barafu, maua yote na majani yameungua.



Hapa barafu ni 500%.
 
Nimekuele
Nimekuelewa sana aisee parachichi tuko nayo hapa makambako ila mh sijaielewa sana hii tunda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…