Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Mkuu,siamini kama ni kweli, labda uwe ulifanya kosa moja,la kuanzisha biashara bila soko.
Au vinginevyo,uwe na uelewa mdogo kuhusu masoko.
Kuna mdau mmoja kasema hutompata mtu atakaekushirikisha mafanikio. Soko likiwepo anataka akupige akulize,na usijue soko.
Kama wewe mwenyewe unaweza, au una watu,jaribu kutafuta connection kwenye makampuni yanayouza nchi za nje. Napojua ni Dubai(kwa mjibu wa watu wa nchi jirani wanaopeleka palachichi na viazi mvilingo huko).
Tatizo kubwa,palachichi nchini humu ni nyingi na watumiaji ni wengi.
Kama umelima una shamba,fatilia. Zamani walikuwa wakisafirisha kwa ndege,ila kwa sasa wanatumia meri. Na hakika ni bandari ya Dar. Kama unaweza pata mzigo wa uhakika si tani moja,mbiki tatu, unawauzia wenye export certificates na masoko yao,kikubwa tu ukidhi vigezo.
 
Ukitumia akili kwenye jambo lolote unalofanya utakwepa mishale kama hii. Nimesoma na kufuatilia sana parachichi kwa China na nimekubali ni biashara ngumu sana.
1. Soko lake kubwa hasa hizo Hass ni China ambapo wao soko lao linapanda na kushuka kutokana na supply wanayopata kutoka Mexico, Kenya, Australia na zaidi ya nusu kutoka Peru. Ikitokea ni msimu wa Peru huko kwingineko bei inashuka sana, muda wa kupiga hela ni pale nchi nyingine zinapokuwa sio msimu.
China iko busy kujitosheleza kwenye parachichi kwahiyo soko litazidi kupungua, na uzuri wa China ni nchi kubwa yenye usawa wa bahari tofauti sana kila eneo hivyo kila upande unaweza zalisha kwa msimu wake na zikawa sokoni mwaka mzima.

2. Teknolojia hatuna. Unavuna parachichi unapakia kwenye fuso utamuuzia nani uko nje? Hamna cold rooms, hamna grading, hakuna refrigerated trucks, hamna kupima quality, water content, protein, texture, ile nyama ya ndani, mbolea haipimwi, ardhi wanatifua tu hata hawajui ardhi gani ina nini na inakosa nini. Tunaenda kienyeji.

3. Serikali inasubiri kutoza ushuru na kodi, yenyewe hata haijui hiyo biashara na kilimo chake inafanyikaje. Hakuna support kabisa sababu parachichi zikiachwa nchi haitokufa njaa.

4. Ni zao lenye usumbufu na linataka mtaji mkubwa. Wakati huo haliuziki ndani, ukikosa soko la nje ukauza ndani unakula hasara kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.

5. Ni zao gumu sana kuuzwa, yani hawa walanguzi wetu wakienda nje uko wanapigwa za uso kirahisi sana. Unatafuta certifications za ubora na kila kitu unapeleka msimu huu, msimu ujao unaweka mtaji wote then Wachina wanapima wanakuta water content kubwa kisa mvua zilizidi uko Niombe. Zinamwagwa, huyo mfanyabiashara atarudi?
Mwaka juzi Wakenya walizuiwa na TFDA ya China kwamba kuna mlipuko wa fruit flies parachichi zao zinaenda na mayai yake. Wakaambiwa ukitaka kuuza menya uuze ile nyama ya ndani. Sasa process ya kumenya na kuuza nyama ya ndani alafu hiyo nyama isiwe nyeusi hata kidogo sio kazi ya kitoto.

Haya yote nimeyajua nikiwa sina mpango wa kulima, ningetaka kulima ningejua mengi zaidi. Sasa mkulima yeye akisikia kwenye redio anaamka na kufyeka eneo atengeneze shamba. Content creators ile ndio kazi yao, kuongea. Usikubali kushikwa masikio
Ni kwamba watu wapo kwenye ukoloni wa kitapeli. Watu wana dili zao,uishi,ufe,haiwahusu.
Unadhani wenye kutoa vibali hizo changamoto hawazijui? Nani akwambie?
Hata kwa mkopo,viwanda vya huko zinatumiwa kufanyia nini? Umeuza kwa hasara,lakini ikishageuzwa kitu kingine inakuja huku inauzwa bei mbaya. Hivyo viwanda vikijengwa huku,wakulima si watakuwa na soko la uhakika?
Huku mafuta ya nazi,utakuta hayana bei,na hayahitajiki kivile. Lakini acha yawekwe kwenye chupa af, yaandikwe kuwa yanatibu nini na nini,na bei yake uone.
 
Ukiona wanasiasa wanahimiza watu walime zao Fulani. Hilo zao achana nalo, Ni mtego.
Ukiona zao halina bodi Wala wanasiasa hawalisemi ujue Hilo Ni dili na wanasiasa wenyewe watakua wanalilima.
Nikuhakikishie, nchi hii hakuna anayemtakia mwenzie mema.
Umeshawahi kumsikia mwanasiasa akihimiza watu walime viazi vya chips ambavyo vinasoko mwana mzima?
Bodi ya Mazao Mchanganyiko huijui?
 
Walituambia Green Gold. Alimanusura nilime. Kuna zao moja hilo hubahatishi
 
Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;

1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)

Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.

Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.

NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
Issue hapa sio parachichi
Miti inatakiwa kwa ajili ya kuboresha hewa....
Ujinga badala tuendeleze ya mbao ambayo ni hela...
Tunapanda matunda pumbu
 
Mkuu nilijiuliza hilo swali kwamba lazima parachichi zizae kwa pamoja mbona viumbe vingine vinazaliwa siku moja ila vina mature tofauti. Naomba hoo elimu ya kuzifundisha zizae mda naotaka.
Zangu ndio zipo hatua ya maua ya pili.
Nalimia njombe ba huku changamoto kubwa ni barafu na jua.
Je ukikomaa na soko la ndani tu je hailipi kweli kama wadau wanavyosema?
Mwaka huu nina project ya heka 20 na watu wana toa tahadhari nami siwezi puuza.
Mashamba yapo kwa sh? Heka moja.
Mkuu
umenena yaliyo kweli kabisaa
kuna mwekezaji alikuja RUNGWE watu walikata mpaka kahawa wakaotesha parachichi
mwaka huu, wakulima wa parachichi mbeya wanalia,,mpaka serekali ya wilaya inawaomba wanunuzi waende.....wakajitokeza wakulima wakachangishana wakapeleka parachichi Njombe na FUSO KADHAA, wamefikisha wakapokelewa,,,ukaguzi umefanyika parachichi zikawa rejected zote tena wakaingia garama tena ya kwenda kutupa

Hiki kilimo kwa NJOMBE waliopiga pesa ni wale waliowahi wakauza MBEGU na wanaosoma ramani TU

Inahitajika ELIMU, mtaji wa kutosha na MUDA otherwise bora tufuge SAMAKI TU wanasema zinalipa
Parachichi hazivumnwi nna kupakiwa kwenye Fuso hapo tu tayari walishapata hasara huwa kuna tray za kuwekea
 
How many stomach are there in Tanzania?
Kwani machungwa hayaozi? Je wameyafanyia nini?
Wakati wataalamu wa lishe wanatabiri kuongezeka ulaji wa matunda halafu sisi tusimamishe uzalishaji.
Ni hivi hakuna uzalisgaji unaotosha kulisha kiwanda cha maana hata mwezi.
Hakuna uzalishaji mkubwavwa parachichi TZ. Kupata hekta 1000 tu zilizokaa pekeake ni kazi.
Suala nitafanya nini siwezi weka hapa, kimsingi tu mwenye akili timamu hawezi ruhusu mzigo wake uoze bali mwehu tu.
Zikianza kukomaa utaona strategy yangu, nitakushirikisha wala usihofu.
kitu kikubwa sana ni kuhamasisha wakulima watoe product nzuri.
Mkuu ten years tocome utashsngaa sana yatakayotokea katika Avocado industry.
Kumbuka Avocado inapandwa na watu wa kila status sio kama pamba.
Fursa hutokea kwa waliothubutu.
Jipe moyo tu mzee baba ila nikwambie ukweli tu kwamba kilimo cha kibongo walanguzi na madalali ndio wanaopiga hela 😂
 
Mkuu
umenena yaliyo kweli kabisaa
kuna mwekezaji alikuja RUNGWE watu walikata mpaka kahawa wakaotesha parachichi
mwaka huu, wakulima wa parachichi mbeya wanalia,,mpaka serekali ya wilaya inawaomba wanunuzi waende.....wakajitokeza wakulima wakachangishana wakapeleka parachichi Njombe na FUSO KADHAA, wamefikisha wakapokelewa,,,ukaguzi umefanyika parachichi zikawa rejected zote tena wakaingia garama tena ya kwenda kutupa

Hiki kilimo kwa NJOMBE waliopiga pesa ni wale waliowahi wakauza MBEGU na wanaosoma ramani TU

Inahitajika ELIMU, mtaji wa kutosha na MUDA otherwise bora tufuge SAMAKI TU wanasema zinalipa
Parachichi ni zao ambalo halitupwi. Cozi likioza unatengeza mafuta, takataka zake unatengeza mbolea. Mbegu yake unatengeza unga. Hao waliotupa walizingua
 
Nililima heka 50 hizo Hass Ovacado mafinga nilipoangalia gharama msimu wa kwanza nikajikuta nimepata mil 14 ndg zangu hela niliyokua nimeweka pale nilitamani kulia mchozi...ovacado ni shida kubwa sana bora ulime mihogo
Hilo nimeligundua mapema sana, kuna mtu alinishawishi nikanunua heka 3 njombe hapo😂 hesabu kwa alizompigia mama watoto kwamba baada ya kuvuna mche mmoja unaweza pata hadi laki 7 nikaona biashara sindio hii sasa.

Nimefyeka miti na kusafisha shamba nikapanda heka 2 kwanza. Siku naenda kuangalia hilo shamba na mazao. Nakuta almost 10% ya miche imekufa 😂 sababu wanasema sijui mvua zilipiga madini yakawa washed away ba blaah blaah kwahio nirudishie tena 10% ya hio miche.

Nikiangalia gharama nilizotumia ndani ya miezi michache hadi kufikia hapo dah nikaona kabisa upkeeping cost za shamba na kile kilichotarajiwa after 3 years ni mbingu na ardhi.

Nimeamua niachane nalo tu hilo shamba. Hamna namna ntaendelea kupoteza hela kule😂
 
Acheni, kateni miti. Mimi siikati na ndio kwanza mwezi wa8 naenda kuchimba mashimo mengine 1500. Na lengo ni kufikisha miche 5000. Wewe kata yako. Chungwa sio Avocado japo yote ni matunda.

Endeleeni kusubiri wachina na warabu, mimi siwafikirii kabisa hao watu.
Binadamu yoyote alieshindwa kuyatawala mazingira yake huyo ni sawa na ng'ombe.
Innovative brain is not for everybody, is something gifted from god and it is for few people.
Mfano mdogo ni kwamba ktk eneo nalolima kuna barafu isio sikia dawa but mimi nimeisha innovate njia yangu ya kuokoa parachichi zangu na barafu huku wengine wakilalama kuungua barafu zao.
Ni hivi siwezi kukuwekeeni njia hapa za kufuata ili muuze hizo Avocado. Nyie ziungue, zidode mkose soko muache mie ndio naongeza mashamba.
Mzungu hajawahi toa siri jinsi anazalisha products zake sasa nyie endeleeni kumsubiri mzungu awafunulie.
Mimi simuhurumii mtu yoyote ambae anashindwa kuuza Avocado zake na wala si ilaumu serikali maana wengi wao hawajawahi fanya chochote cha uzalishaji zaidi wanahitaji kodi yao tu.

Nakupongeza sana kuwa ktk mtazamo hasi kwani wengi mkiwa ktk mtazamo chanya mtafanya njia kuwa ngumu. Walalamishi wakiwa wengi huwasaidia wale wanaofanya mambo yao kwa akili yao.
Wewe ni motivational speaker. Unafanya jambo sasa bila kuwa na strategy, unasubiri baadae ndo ujue utafanya nn
 
Kuwa mvumilivu nilichojifunza kwenye parachichi haitaki uwe na haraka Sana Ili kupata pesa. It takes time na energy nyingi Sana Ila ni permanent crop. Uzalishaji huongzeka mwaka Hadi mwaka . Parachichi inahitajika uwe na subra na usiwe na haraka kupata pesa. Miti ya parachichi angalau ufike maximum 7- 10 yrs ili uanze kapat faida
Hio miaka 7-10 aliyelima mahindi yuko wapi?!
 
Parachichi ni biashara ya wauza miche na mashamba..

Ukitaka lima kidogo miche 200 inatoshs, itunze hadi uanz3 kuvuna ndio uqekeze zaidi.

Kuna mambo mengi sana

Kupalilia
Kuweka dawa
Kupunguza nyasi
Kumwagilia

Kuna jamaa alikua na ekari 100, amedha tumia zaidi ya mil 200, ameamua kuuza shamba lake lote baada ya kuona hatoboi
mi nimeuza heka zangu 3 baada ya kuona maji yatazidi unga in 3 years😂😂😂😂
 
Mkuu umeandika ukweli mtupu, Tatizo la hapa Tanzania wanasiasa wanadanganya sana wananchi
Wengi wa hao waongo ndio madalali
1. Atakutafutia shamba
2. Atakutafutia vibarua
3. Atakutafutia trekta na majembe
4. Atakutafutia mbegu
5. Atakutafutia dawa na mabomba
6. Atakutafutia wavunaji
7. Atakutafutia walinzi
8. Ataongea na watendaji ‘wakulinde’
9. Kisha atauza yeye, atakupa kipande kidogo tuncha income
10. Ma kila step hapo juu anakua anapiga kidogo kidogo

Ogopa uwekezaji na Wana siasa na watu wenye nafasi za kidalali
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Kilimo kwa hapa Tanzania ni U.T.I ya mgongo, (siyo uti wa mgongo.).
 
Leo njombe parachichi bei kilo Moja madalali wanasema ni shillingi 500 na wanapakia lumbesa utaki unaacha . Na parachichi ikiwa over matured awanunui
Duh tutafika kweli.?
Au ndo tutafika tukiwa tumechoka sana
 
Back
Top Bottom