Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Nnavojua mm
Kiazi ukiuza gunia moja zaidi ya elf 28
Kamwe hupati hasara

Kiazi kikuzwa chini ya elf 23 NDIO maumivu kwa mkulima
Kimejiotea chenyewe eti. Kuanzia mbolea, dawa,vibarua, ardhi.,mbegu halafu ikulope kwa elf28.
Wakulima wengi hawapigi hesabu ya uzalishaji wanafurahia kushika hela, ila wengi hawapati faida. Kiujumla kilimo chetu hulipa pale kuna mfumuko wa bei.
Mfano mahindi yakirudi bei ya 7000 kwa debe mkulima tayari ana hasara, hivyo anatakiwa atumie akili sana.
 
Mkuuu ukifwata Kanuni zote za kilimo kwa kuzingatia

Ekari moja hukosi gunia kwanzia 60 mpaka 100.

Ukipata gunia 60 ukauza 28k per gunia utapata bei gani?

Jee gharama za kulima na kutunza zitafikia hyo bei uliouzia mpaka ukasema ni hasara?

Na ujue kiazi kinakaa shambani miezi 3_4 basi
 
Nililima heka 50 hizo Hass Ovacado mafinga nilipoangalia gharama msimu wa kwanza nikajikuta nimepata mil 14 ndg zangu hela niliyokua nimeweka pale nilitamani kulia mchozi...ovacado ni shida kubwa sana bora ulime mihogo
Kuwa mvumilivu nilichojifunza kwenye parachichi haitaki uwe na haraka Sana Ili kupata pesa. It takes time na energy nyingi Sana Ila ni permanent crop. Uzalishaji huongzeka mwaka Hadi mwaka . Parachichi inahitajika uwe na subra na usiwe na haraka kupata pesa. Miti ya parachichi angalau ufike maximum 7- 10 yrs ili uanze kapat faida
 
[emoji23] Unazungumzia breed gani? Parachichi inayolimwa na kuuzwa zaidi duniani ni Hass, ambayo inazaa vizuri sana baada ya miaka mitatu

Kwa utunzaji mzuri mti mmoja unapaswa ukupatie Parachichi 1000 net

Huangaiki na madawa ya Mara kwa Mara kwasbb matunda yenyewe hayaingizi wadudu.
 
[emoji23] Unazungumzia breed gani? Parachichi inayolimwa na kuuzwa zaidi duniani ni Hass, ambayo inazaa vizuri sana baada ya miaka mitatu

Kwa utunzaji mzuri mti mmoja unapaswa ukupatie Parachichi 1000 net

Huabgaiki na madawa ya Mara kwa Mara kwasbb matunda yenyewe hayaingizi wadudu.
Miaka mitatu kwa HASS variety iliyobadiwa bado ni uongo kabisa. Miaka mitatu unaanza kutoa matunda machache ambapo huwezi ona faida Yake. Miaka inavyozidi kwenda ndio idadi ya matunda huongezaka na faida huonekana pia
 
Kapande tena, uidraft itawahi kuzaa.
Sojawahi ona miaka hii embe bolibo au dodo inauzwa 100. 3buku.
Embe tu zikifanywa kwa ustadi zinamtoa mtu.
Embae zisizofaa ni sindano zinaoza haraka sana.
Vijana msichelewe, pandeni miti,msisikilize keleke.
Naishi mbali sana kutoka hapo. Na miti iliyokatwa ilikuwa na miaka mingi sana zaidi ya 30.
 
Hiyo ipo, lakini kwenye hivi vitu aisee kuna mbegu za aina nyingi sana. Wiki iliyopita nimeanzisha mradi wa bustani bamia, karoti, nyanya, nyanya chungu, spinachi, mchicha, chaina, matango, tikiti maji, sukuma wiki, pilipili.

Wakati naenda mjini kununua mbegu huko ndiko nilishangaa kukutana na mbegu za maajabu, aisee kuna bamia tangu nizaliwe sijawahi kuziona, ni kubwa kama tango. Wakati wa kununua mbegu za nyanya yule mzee kanipa za aina tatu hivi ila moja wapo kaniambia hiyo mbegu nyanya zake hukaa hata miezi miwili bila kuharibika baadae huwa ni kama zinanyauka vile. Na kuna mbegu zingine za nyanya japo sikuweza kuinua kutokana na bei yake kuwa juu kaniambia hii mbegu ukipanda unauwezo wa kuvuna nyanya zaidi ya miezi mitano
Kwenye nyanya hapo mi ni shuhuda,nilinunia nyanya ikakaa siku 28 bila kuharibika, na haipo kwenye fridge
 
Tungejikita kwenye kuzalisha mazao ya viwanda ie Machungwa, Maembe, Limao za juisi hizi huwa hazina mbegu nyingi, zina maji mengi.

Sasa machungwa ya Tz huvunwa hata kabla ya muda wake, pia yana mbegu nyingi sana
 
Miaka mitatu kwa HASS variety iliyobadiwa bado ni uongo kabisa. Miaka mitatu unaanza kutoa matunda machache ambapo huwezi ona faida Yake. Miaka inavyozidi kwenda ndio idadi ya matunda huongezaka na faida huonekana pia
Ulichosema ni sahihi inapofika miaka mitano (5) ndio matunda yanazaliwa kwa wingi sana
 
Tungejikita kwenye kuzalisha mazao ya viwanda ie Machungwa, Maembe, Limao za juisi hizi huwa hazina mbegu nyingi, zina maji mengi.

Sasa machungwa ya Tz huvunwa hata kabla ya muda wake, pia yana mbegu nyingi sana
Hivi kwa nini tunabeza kila tunachozalisha wakati takwimu zinaonesha TZ ndio mzalishaji mkuu wa mazao hapa EA.
Jana mh. KKabudi kasema Kakao,Kahawa ni nazao bora kabisa yabayopigiwa chapuo huko ulaya ila sie tunabeza sana.
Miaka ya nyuma hapo, BBC waliwahi toa takwimu ya kilimo cha maharage kwa TZ ndio no 1 in Africa na export ni kubwa kuliko nchi yoyote ile .
Inakuwaje sisi tunaona mazao yetu hayafai.
 
watu washazoea kupingapinga, wasamehe
 
Hiyo ipo, lakini kwenye hivi vitu aisee kuna mbegu za aina nyingi sana. Wiki iliyopita nimeanzisha mradi wa bustani bamia, karoti, nyanya, nyanya chungu, spinachi, mchicha, chaina, matango, tikiti maji, sukuma wiki, pilipili.

Wakati naenda mjini kununua mbegu huko ndiko nilishangaa kukutana na mbegu za maajabu, aisee kuna bamia tangu nizaliwe sijawahi kuziona, ni kubwa kama tango. Wakati wa kununua mbegu za nyanya yule mzee kanipa za aina tatu hivi ila moja wapo kaniambia hiyo mbegu nyanya zake hukaa hata miezi miwili bila kuharibika baadae huwa ni kama zinanyauka vile. Na kuna mbegu zingine za nyanya japo sikuweza kuinua kutokana na bei yake kuwa juu kaniambia hii mbegu ukipanda unauwezo wa kuvuna nyanya zaidi ya miezi mitano
Ndio haya nilisema kwenye uzi huu, unataka kufanya kilimo alafu ukienda kununua mbegu unazishangaa.
Ulitakiwa ushangae mbegu kabla hata hujapanga kuzinunua, kuwa na information zote kabla ya kuanza project alafu ndio ukapate experience ya hiyo info kivitendo. Hapo dukani kwa pembejeo hukutakiwa kushangaa ulitakiwa uwe na notebook unasoma namba au jina la mbegu fulani na unapatiwa, sio unaenda kushauriwa hapohapo dukani sasa kama kuna mbegu nzuri zaidi hana utajuaje? Au utajuaje huyo mzee ana akili na uelewa sawasawa, unaweka hela kwenye hearsay badala ya taarifa ya uhakika.

Sehemu unaweza kuamini unachoambiwa ni kwenye sekta ya afya ambapo wanafundishwa strictly kuwa waaminifu na kutoa taarifa sahihi, hii ni kwa sababu taarifa za kitabibu ni ngumu kueleweka na layman na zinagusa maisha ya watu, ukikosea una kesi. Uko kwingine wafanyabishara na wenye taaluma zao wanaweza kuongea kwa kukariri au influence.

Kitu cha muhimu kabla ya kulima ni kupata uhakika wa soko hasa kwa mazao yanayoharibika haraka. Sasa kama ulishangaa mbegu dukani, nina wasiwasi kama hata hayo mavuno unajua utayauza wapi.
 
Tikiti gani uuze hapa Bongo upate Mil 20? [emoji23]

Walianzia mbali Mimi huwa siwasikilizi hata, Mara ufugaji Sungura, Ufugaji wa samaki, Kilimo cha parachichi, tikiti maji, kilimo cha Vanila...then hawakupi kbs soko la uhakika na bei exactly
Wee endelelea kula ugali wa bure kwa dada yako[emoji16] unasubili wakupe soko ndo ukalime

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;

1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)

Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.

Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.

NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
Parachichi ni biashara ya wauza miche na mashamba..

Ukitaka lima kidogo miche 200 inatoshs, itunze hadi uanz3 kuvuna ndio uqekeze zaidi.

Kuna mambo mengi sana

Kupalilia
Kuweka dawa
Kupunguza nyasi
Kumwagilia

Kuna jamaa alikua na ekari 100, amedha tumia zaidi ya mil 200, ameamua kuuza shamba lake lote baada ya kuona hatoboi
 
Umasikini úmekujaa ndo maana upo kwenye porojo huku ukisimulia wengine waliochukua hatua na kufanya

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
We mwanamke unawashwa sana kuchokoza Wanaume sio? Kama Baba yako alikulia kwa Dada yake na mahari akatolewa na Dada ni yeye sio Mimi
Hakuna mwanaume wa hivo labda ni upinde wenzako wanatafuta soko wewe umekaa kwa dada yako unasubili soko liletwe ndo uanze kulima[emoji16] hayo ni Mawazo ya masikini kufikiri hawezi kufanya jambo kwasababu sijui hakuna soko

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mwanaume wa hivo labda ni upinde wenzako wanatafuta soko wewe umekaa kwa dada yako unasubili soko liletwe ndo uanze kulima[emoji16] hayo ni Mawazo ya masikini kufikiri hawezi kufanya jambo kwasababu sijui hakuna soko

Sent from my TECNO CF8 using JamiiForums mobile app
Unasubili ndio nini? Hata kuandika Mwanamke huwezi sasa nani atakuoa, au utaishia kudanga[emoji23][emoji23][emoji23]

Tafuta danga akununulie hata simu utoke kwny TECNO [emoji23]
 
Back
Top Bottom