Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Migomba ilifyekwa mno, misitu ikachomwa moto na kuvunwa hovyo ili wapande maparachichi.

Kwa maana waliopanda mwaka juzi saivi wanalia tu,parachichi liliwafaidisha wale watu wa mwanzo kabisa miaka ya 2011 kidogo mpaka mwaka juzi.
Chini ya mlima Rungwe Mwekezaji alikuja akalima akashawishi na wenyeji pia, ambao humuuzia yeye

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Acheni, kateni miti. Mimi siikati na ndio kwanza mwezi wa8 naenda kuchimba mashimo mengine 1500. Na lengo ni kufikisha miche 5000. Wewe kata yako. Chungwa sio Avocado japo yote ni matunda.

Endeleeni kusubiri wachina na warabu, mimi siwafikirii kabisa hao watu.
Binadamu yoyote alieshindwa kuyatawala mazingira yake huyo ni sawa na ng'ombe.
Innovative brain is not for everybody, is something gifted from god and it is for few people.
Mfano mdogo ni kwamba ktk eneo nalolima kuna barafu isio sikia dawa but mimi nimeisha innovate njia yangu ya kuokoa parachichi zangu na barafu huku wengine wakilalama kuungua barafu zao.
Ni hivi siwezi kukuwekeeni njia hapa za kufuata ili muuze hizo Avocado. Nyie ziungue, zidode mkose soko muache mie ndio naongeza mashamba.
Mzungu hajawahi toa siri jinsi anazalisha products zake sasa nyie endeleeni kumsubiri mzungu awafunulie.
Mimi simuhurumii mtu yoyote ambae anashindwa kuuza Avocado zake na wala si ilaumu serikali maana wengi wao hawajawahi fanya chochote cha uzalishaji zaidi wanahitaji kodi yao tu.

Nakupongeza sana kuwa ktk mtazamo hasi kwani wengi mkiwa ktk mtazamo chanya mtafanya njia kuwa ngumu. Walalamishi wakiwa wengi huwasaidia wale wanaofanya mambo yao kwa akili yao.
Rahisi kuongeleka

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Nililima heka 50 hizo Hass Ovacado mafinga nilipoangalia gharama msimu wa kwanza nikajikuta nimepata mil 14 ndg zangu hela niliyokua nimeweka pale nilitamani kulia mchozi...ovacado ni shida kubwa sana bora ulime mihogo
Poole asee, Mm mafinga sehemu gani asee

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Tikiti gani uuze hapa Bongo upate Mil 20? [emoji23]

Walianzia mbali Mimi huwa siwasikilizi hata, Mara ufugaji Sungura, Ufugaji wa samaki, Kilimo cha parachichi, tikiti maji, kilimo cha Vanila...then hawakupi kbs soko
Ufugaji wa samaki unashida gani ndugu?
 
Ukiona wanasiasa wanahimiza watu walime zao Fulani. Hilo zao achana nalo, Ni mtego.
Ukiona zao halina bodi Wala wanasiasa hawalisemi ujue Hilo Ni dili na wanasiasa wenyewe watakua wanalilima.
Nikuhakikishie, nchi hii hakuna anayemtakia mwenzie mema.
Umeshawahi kumsikia mwanasiasa akihimiza watu walime viazi vya chips ambavyo vinasoko mwana mzima?
 
Sahihi ndugu, unastahili PhD kabisa wewe. Huo ndio ukweli
 
Mkuuu
Kwa barafu la makete unalizuiaje kwa mfano

Tupe ABC
Hapa watu wanaona mambo hayawezekani, acga tu wapagawe wafeli wakimbue.
Mie nsha innovate simple method na naendelea na utafiti kuboresha. Natumia simple method.
Leo nimejifunza njia zingine mbili kutoka kwa wenye akili wanao tumia ubongo.
 
Hapa watu wanaona mambo hayawezekani, acga tu wapagawe wafeli wakimbue.
Mie nsha iinivate simple method na baendelea na utafiti kuboresha. Natumua simple method.
Leo nimejifunza njia zingine mbili kutoka kwa wenye akili wanao tumia ubongo.
Story nyingi we sema barafu unaizuiaje simple and clear

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
 
Ukiona wanasiasa wanahimiza watu walime zao Fulani. Hilo zao achana nalo, Ni mtego.
Ukiona zao halina bodi Wala wanasiasa hawalisemi ujue Hilo Ni dili na wanasiasa wenyewe watakua wanalilima.
Nikuhakikishie, nchi hii hakuna anayemtakia mwenzie mema.
Umeshawahi kumsikia mwanasiasa akihimiza watu walime viazi vya chips ambavyo vinasoko mwana mzima?
Mkuu viazi vya chipsi havina soko mwaka mzima na hakuna wanasiasa wanalima hilo zao. Nayo ni perishable goods kama matunda tu.
Mda huu nakwambia bei ime drop from elf 80 mpaka elf 40. Ni bora hata kulima avocado kuliko viazi, very expense na wakulima wengi hawapati faida ispokuwa misimu michache tu na mara nyingi ni mwanzo wa msimu.
Viazi mviringo ndio biashara kichaa bora hata avocado.
Naishi kwenye mabonde ya hili zao na nalima. Ni pasua kichwa.
Kilimo chetu kwa ujumla kinachangamoto mtu akitoboa ujue huyo ni mjanja sana na anatumia akili yake vuzuri.
 
Story nyingi we sema barafu unaizuiaje simple and clear

Sent from my Pixel 3a using JamiiForums mobile app
Tumia akli mkuu. Humu kuna hali ya kudharauliana, hivyo chemsha kichwa.
Zipo njia 5 za kuzuia, 3 zinafafamika 2 nime innovate kwa akili yangu, sijaziona popote.
Parachichi zako zikiungua ndio utazijua, yaani kama wewe kichwa kipo timamu utazijua tu, hutaruhusu ziungue msimu ujao.
mwakani bataka iwe businesses , ntawatembekea watu wanaojielewa niwauzie wazo na vifaa.
Hii ni kwa wale walio ktk barafu kali ambayo haizuiliki kwa njia zilizozoeleka njombe.
Pole mkuu, wajuaji wanasababisha tusiweke solution humu, mwenye dharau muache na dharau yake.
 
Hapa watu wanaona mambo hayawezekani, acga tu wapagawe wafeli wakimbue.
Mie nsha iinivate simple method na baendelea na utafiti kuboresha. Natumua simple method.
Leo nimejifunza njia zingine mbili kutoka kwa wenye akili wanao tumia ubongo.
Tuwekee hapa hizo simple methods nao wajifunze
 
Mkuu viazi vya chipsi havina soko mwaka mzima na hakuna wanasiasa wanalima hilo zao. Nayo ni perishable goods kama matunda tu.
Mda huu nakwambia bei ime drop from elf 80 mpaka elf 40. Ni bora hata kulima avocado kuliko viazi, very expense na wakulima wengi hawapati faida ispokuwa misimu michache tu na mara nyingi ni mwanzo wa msimu.
Viazi mviringo ndio biashara kichaa bora hata avocado.
Naishi kwenye mabonde ya hili zao na nalima. Ni pasua kichwa.
Kilimo chetu kwa ujumla kinachangamoto mtu akitoboa ujue huyo ni mjanja sana na anatumia akili yake vuzuri.
Nnavojua mm
Kiazi ukiuza gunia moja zaidi ya elf 28
Kamwe hupati hasara

Kiazi kikuzwa chini ya elf 23 NDIO maumivu kwa mkulima
 
Nimefanya kilimo cha parachichi kwa miaka nane sasa, nilichokiona ni haya;

1. Kilimo kina mzunguko wake ni mdogo parachichi huzaa kidogo kidogo kadri miaka inavyoenda, unatumia million 10 unapata million mbili.
2. Bei hazijadiliki anayeamua ni mnunuzi unless uwe na mtaji mkubwa ambayo unakuruhusu ku export mwenyewe, na uwe na uwezo wa kuwa na cold room Ili zikikomaa uchume uzihifadhi kama bei hueilewi kwa kipindi hicho (hii mitaji watanzania wengi hatuna). 3. Management ya parachichi ni ngumu sana linahitaji maji kidogo (hapa unaweza manage kumwagilia) linahitaji mbolea za chumvi na mbolea za majani, sumu. Kila nk kwa kiasi kidogo, linahitaji muda Kwa wingi, upatikanaji wa Samadi ni mtihani sana (wengi wamejikuta parachichi zimedumaa na wengine wanazalisha reject kwa wingi) kisa tu wameshindwa kuwa na Samadi, udhibiti wa nyasi (ukweli ni kuwa Ili miti iwe Bora unahitaji kulima badala ya kufyeka nyasi)

Nimefanya observation shambani kwangu panapolimwa pana matokeo kuliko panapofyekwa, distance kati ya mti na mti inamua sana miti iliyokaribu inasumbua sana na mingi huwa haizai vizuri. Hizi issue zimefanya watu tukimbie mashamba yetu, hata kiwango cha pesa kinachotajwa wengi hawapati ni figure za uwongo Ili kujifariji, njoo na hoja zako kupinga zangu hapo juu, zangu ni hizo.

Nashauri kama una pesa zako kidogo lima mazao ya chakula tu viazi, mpunga, mahindi nk hivi vinalipa. Huku pesa ipo na kama location ulipo ni nzuri lima mazao yanayohifadhika like kahawa, miaka miwili inazaa, management yake rahisi. Nalima kahawa makete pia ni mwaka wa tatu tayari nimeanza kuvuna.

NB: Mazao ya chakula ndio kila kitu hizi nyingine tabu umezitafuta.
Hongera, huku nje tunaaninishwa parachichi ni fursa
 
Nikikumbuka kwa bibi kuna mjukuu alishawahi kata miti ya maembe na maparachichi ili kuvuna mbao napata hasira sana. Yule jamaa sintokaa nimwelewe.
Kapande tena, uidraft itawahi kuzaa.
Sojawahi ona miaka hii embe bolibo au dodo inauzwa 100. 3buku.
Embe tu zikifanywa kwa ustadi zinamtoa mtu.
Embae zisizofaa ni sindano zinaoza haraka sana.
Vijana msichelewe, pandeni miti,msisikilize keleke.
 
Nchi za wenzetu zinajali sana walaji.

Tanzania ni nchi ambayo haijali walaji ndio maana Matunda huanguliwa na kupakiwa kwenye mafuso

Nchi zingine mf Marekani nimewahi fatilia youtube kila bidhaa lazima ipite kiwandani kusafishwa na kuwa packed kuanzia machungwa hadi vitunguu lazima viwe packed.

Huku kwetu nenda pale Mahakama ya Ndizi Mabibo utaweza acha kula ndizi

Nenda Temeke, Tegeta Nyuki hakika huwezi kula.

Madawa mengi sana hutumika muda mfupi kabla ya kuvuna, nina Nyanya nimekaa nazo Mwezi na siku 2 haziozi hadi nikazitupa hazina funza wala nini
.
 
Ukiona wanasiasa wanahimiza watu walime zao Fulani. Hilo zao achana nalo, Ni mtego.
Ukiona zao halina bodi Wala wanasiasa hawalisemi ujue Hilo Ni dili na wanasiasa wenyewe watakua wanalilima.
Nikuhakikishie, nchi hii hakuna anayemtakia mwenzie mema.
Umeshawahi kumsikia mwanasiasa akihimiza watu walime viazi vya chips ambavyo vinasoko mwana mzima?
Gharama ya kuzalisha viazi vya kyepe hazimithiriki faida kiduchu... Kuna mazao Yana faida ila ulime kimkakati na pakubwa. Sasa avocado unalima miti 200 unategemea uwe tajiri?!
 
Back
Top Bottom