Ukweli kuhusu Kanisa Katoliki kuanzisha Dini ya Kiislamu

Ukweli kuhusu Kanisa Katoliki kuanzisha Dini ya Kiislamu

Sijawahi kuona hoja nyepedi na za kipuuzi kama hii la dai la kuwa Ukatili kuzalisha uislamu.

Uzi wako una chai nyingi kiasi ambacho hata nashinda nianze na you na kuona uzi wenyewe ni upuuzi moja kwa moja.

Ukisoma kwa umakini uislamu historia yake Pamoja na Qu'ran kwa ujumla hitimisho linakuja kuwa haiwi kwa uislamu , Qu'ran Pamoja na utume wa Mtume Muhammad (upon him be peace and blessings of Allah) utoke kwa mwengine isipokuwa Allah Mola mlezi wa ulimwengu wote.
Soma pia historia

Ulishajiuliza kwanini nje ya QURAN huwez kupata uthibitisho wa kiakolojia ,au wa kisayansi kuhusu Uislamu

Uislamu Ni dini iliyoanzishwa mwaka 600 AD , Na Roman Catholic wakimtumia Muhammad

IMG_20230507_071832.jpg
 
Kuna wenzio karne nyingi wamepigana na kanisa katoliki wameshindwa,wewe upo kwenu kinyerezi na techno yako unapiga kelele hapa.
 
Shida yenu wazungu walichelewa sana kuandika Historia. Matokeo yake wanakuka kuwatingia habari za uongo na mlivyo siyo watu wa kusoma na kufanya utafiti mnaingia mkenge.

Siku zote huwa nasema hivi anasema Uislamu umeanzishwa na Ukatoliki haujui Uislamu. Mtoa mada Nina maswali yafuatayo juu yako :

1. Naomba utuwekee ushahidi unao onyesha ya kuwa Waraqah alikuwa Mkatoliki na mama Khadija alikuwa mkatoliki.

2. Hizi habari kwa mara ya kwanza zimeanza kusikika lini na kwanini isiwe kabla ?

3. Tuthibitishie ya kuwa yule mtu aliyekutana na mtume na ami yake katika safari zao za biashara alikuwa Mkatoliki ?

Kuna mada huwa zinatia uvivu kuzijadili, sababu Zina uongo.
Jitahidi usome Sana hasa historia ,usijifungie kwenye Quran tu
755476816.jpg
 
MUNGU ALITUMIA WATU GANI KUMSULUBISHA NA KUMUUA YESU?

JIBU

Jibu kwa swali hili lina njia nyingi. Kwanza, hamna shaka, viongozi wa dini wa Israeli walihusika na kifo cha Yesu. Mathayo 26:3-4 inatuambia "Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, kuhani mkuu. Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue." Viongozi wa Kiyahudi walidai kwa nguvu kutoka kwa Warumi kuwa Yesu auwawe (Mathayo 27:22-25). Hawangeweza kumruhusu kuendele kutenda ishara na maajabu kwa sababu hiyo iliwatishia vyeo vyao na nafasi yao ya kidini katika jamii walioitawala (Yohana 11:47-50), kwa hivyo "walifanya mipango ya kumwua Yesu" (Yohana 11:53).

Warumi ndio waliomsulibisha (Mathayo 27:27-37). Kusulubiwa ilikuwa njia ya Kirumi ya kunyonga, iliyoidhinishwa na kutekelezwa na Warumi chini ya mamlaka ya Pointio Pilato, gavana wa Kirumi ambaye alimhukumu Yesu. Askari wa Kirumi waligongerea msumari kwa mikono yake na miguu, kikosi cha Kirumi kilisimamisha msalaba na askari wa Kirumi alimdunga mkuki upavuni mwake (Mathayo 27:27-35)

Watu wa Israeli pia waliridhika na kifo cha Yesu. Wao ndio wapasa sauti, "Asulubiwe! Asulubiwe!" aliposimama mbele ya Pilato (Luka 23:21). Pia waliomba mwizi Baraba afunguliwe badala ya Yesu (Mathayo 27:21). Petro anadhibitisha hili katika Matendo 2:22-23 wakati aliwaambia wanaume wa Israeli, "nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe." Hakika kuuwawa kwake Yesu ilikuwa ni njama iliyowahuzisha Rumi, Herode, na viongozi wa Kiyahudi na watu wa Israeli, makundi tofauti ambayo hayakuwai fanya kazi pamoja tangu mwanzo, lakini wakaja pamoja wakati huu mmoja kufanya njama na kutekeleza lile lisilofikirika: mauaji ya Mwana wa Mungu.

Mwoshowe, na pengine kiajabu, ilikuw ni Mungu aliyemfanya Yesu kufa. Hili lilikuwa tendo la juu sana la haki ya kiungu liliwai fanyika "Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu" (Matendo 2:23) na kwa kusudi kuu. Kifo cha Yesu msalabani kulituhifadhia wokovu mara milioni isiyohesabika na kupeana njia pekee ambayo Mungu angeweza kusamehe dhambi bila kuaibisha utakatifu Wake na haki Yake kamilifu. Kifo cha Yesu ulikuwa mpango kamilifu wa Mungu wa ukombozi wa milele wa walio wake. Mbali na kuwa ushindi kwa Shetani, vile wengine wamekisia, au mkasa usiostahili, lilikuwa tendo kuu la neema ya wema na huruma ya Mungu, dhihirisho la juu la upendo wa Baba kwa wenye dhambi. Mungu alimfanya Yesu afe kwa sababu ya dhambi zetu ili tuweze kuishi bila dhambi na haki mbele zake, haki iwezekanayo pekee kupitia kwa msalaba. "Kristo hakuwa na dhambi, lakini Mungu alimfanya ahusike na dhambi kwa ajili yetu, ili sisi kwa kuungana naye, tupate kuushiriki uadilifu wake Mungu" (2 Wakorintho 5:21).

Kwa hivyo sisi ambao tumekuja kwa Kristo kwa imani tuna hatia ya damu yake iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu. Alikufa ili alipe adhabu ya dhambi zetu (Warumi 5:8; 6:23).
 
Na shida inayowatesa nyie vikanisa vinavyozuka na kupotea ni umoja wa kanisa katoliki,mkijitazama mmeshindwa kuwa kitu kimoja basi mnalazimisha na ukatoliki usambalatike.
 
Hii stori yako ina mapungufu mengi mno ila imani ya Mungu itabaki pale pale maana hakuna mtu anaweza kupigania Mungu Mungu ni kila kitu katika yote anajitisheleza
 
Unahitaji elimu kubwa Sana

Yesu hakuja kubadili TORATI

Muhamad mafundisho yake yanatofautiana pakubwa na Waliomtangulia

Wayahudi sio wajinga ,walipotaka kumuhakiki UTUME wake ,ndipo ugomvi ukaanza

Quran imejaa aya za kuwachukia Wayahudi
Wayahudi wametajwa sana kwenye Quran kwa kuwa wanasifa zifuatazo:
1.nijamii ambayo imepewa elimu kwani asilimia zaidi ya 90 ya mitume wa muungu waliokuwa wanatoka kwenye jamii ya uyahudi.
2. Kutokaana elimu waliopewa walitarajia kuwa mtume wa mwisho pia atatoka kwenye jamii yao, lakini Allah hakumtoa mtume huyo kwenye jamii yao, na hivyo kupelekea kuwa na chuki kubwa kwenye vifua vyao, na katika kutekeleza chuki zao wapo tayari kushirikiana na kila jamii kuhakikisha kuwa binaadamu hawamfuati mtume sahihi ambao wao hawamkubali kutokana tu hatoki kwenye jamii yao. Ndio maana Quran imewazunguza sana ili kumfahamisha Muhammad na watu wafuasi wake kuhusu ubaya wao, na katika hili ni rahisi mara 100 kumkuta mkiristo au anaeabudia asiekuwa muungu kuingia kwenye uislam kulinganisha na wanaojiita wayahudi.
3. Wayahudi kwa kuwa niwatukutu, ndio maana wakapatiwa mitume wengi hata hivyo walikuwa wabishi na waliwauwa baadhi ya mitume wao, vile vile walitaka kumuuwa Jesus,(jesus vile vile ni myahudi) lakini Allah akamlinda na akafananishwa mmoja wa waliokusudia kumuuwa sura ya Jesus na Allah akamchukuwa Jesus kumpleka mbinguni.
Kiufupu Qur an imesimulia karne zilizopita ambazo kwa kiasi kikubwa zilitawaliwa na historia ya mitumei iliotoka kwenye jamii ya kiyahudi
 
Aliacha kanisa linaloonekana acha kujidanganya amlipa Petro funguo, wale wanafunzi wake walikuwa ndio equivalent na maaskofu, wakasambaa na kufungua makanisa, kasome historia ya kanisa vizuri. Yesu hakuacha tuwe disorganized tu eti kanisa la kufikirika.
Yesu hakuacha mtindo wa Rozali, hakuacha masanamu na misingi ya dini ya ukatoliki hakuacha Yesu, hakuacha miungu watu kuabudiwa.

Turudi kwenye mstari KUONGOZWA na Roho mtakatifu.
 
Nyie Mungu wenu Ni Yesu mnashindwa kuelewa kwamba uislam umeanzia kwa nabii Adam nyie mmekomaa na Muhammad saw ambae yeye kaja juzi karne ya 6 uislam ni zaidi ya idea ya kikristo(Roman) ya miungu 3,

Uislam ni kuanzia kwa Adam, Nuhu, ibrahim, Musa wote hao walikua na meseji moja ya Mungu mmoja. Ukiangalia hapo waroma wanaanzia kwa Muhammad kutengeneza conspiracy yao wakizani uislam ulianzia pale ndio maana Kuna vitu vingi wanajichanganya mtume kaja kuendeleza alipoishia Yesu. Wao Yesu ni miongoni mwa miungu Yao halafu wanakwambia watengeze uislam.

Changamoto yao kwanza kitabu biblia yenyewe wameivurugu kweli Mara vitabu 66 Mara vitabu 72 Mara version hii Mara ile..Kama kweli waliunda uislam nilitegemea na Quran waitengenezee version inayokidhi mahitaji ya Sasa.

Chakushangaza hawawezi kuedit hata mstari mmoja wa Quran tangu imeshuka Hadi leo na ndio ishu imewafanya wadate.
Wao wauchezee uroma kwakutengeneza sheria mpya mpya lakin uislam msingi wake hawawezi kufanya kitu na hawakuunda kitu sisi tunaamini kuanzia Ibrahim As na ndie alijenga alkaaba Sasa taratibu za Ibrahim zikoje katka imani? Je Ibrahim na ukatoliki wanaendana? Ukiangalia ibrahim hajawahi kuzungumzia utatu mtakatifu Sasa wao wameupata wapi?

Ushauri wakatoliki wajikite kutngeneza kanisa lao kwanza na hizi Mambo za ushoga zinazowaandama ili dini yao ionekani ninsafi hata watu waanze kuhamia kama maadili katika kanisa lao yameshindikana iweje waweze kukontrol Islam au Wana Baki wanatengeneza theory kurubuni watu.

Kinachowanganya ni kua wao wameacha misingi ya dini wakaunda taasisi wanasema Muhammad aliambiwa awafuate watu wa kitabu sawa.alimanisha afuate Injili halisi aliyokuja nayo Yesu. Lakin Leo hii ukiomba upewe Injili ya Yesu wallahi hupati hata aya moja kutoka kwa waroma kwani wameshaivuruga na kuweka vitu vya maslahi Yao kwajili ya taasisi Yao.

Qurani 2:2

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Hii stori yako ina mapungufu mengi mno ila imani ya Mungu itabaki pale pale maana hakuna mtu anaweza kupigania Mungu Mungu ni kila kitu katika yote anajitisheleza
Weka hayo mapungufu , otherwise ni malalamiko
 
Wayahudi wametajwa sana kwenye Quran kwa kuwa wanasifa zifuatazo:
1.nijamii ambayo imepewa elimu kwani asilimia zaidi ya 90 ya mitume wa muungu waliokuwa wanatoka kwenye jamii ya uyahudi.
2. Kutokaana elimu waliopewa walitarajia kuwa mtume wa mwisho pia atatoka kwenye jamii yao, lakini Allah hakumtoa mtume huyo kwenye jamii yao, na hivyo kupelekea kuwa na chuki kubwa kwenye vifua vyao, na katika kutekeleza chuki zao wapo tayari kushirikiana na kila jamii kuhakikisha kuwa binaadamu hawamfuati mtume sahihi ambao wao hawamkubali kutokana tu hatoki kwenye jamii yao. Ndio maana Quran imewazunguza sana ili kumfahamisha Muhammad na watu wafuasi wake kuhusu ubaya wao, na katika hili ni rahisi mara 100 kumkuta mkiristo au anaeabudia asiekuwa muungu kuingia kwenye uislam kulinganisha na wanaojiita wayahudi.
3. Wayahudi kwa kuwa niwatukutu, ndio maana wakapatiwa mitume wengi hata hivyo walikuwa wabishi na waliwauwa baadhi ya mitume wao, vile vile walitaka kumuuwa Jesus,(jesus vile vile ni myahudi) lakini Allah akamlinda na akafananishwa mmoja wa waliokusudia kumuuwa sura ya Jesus na Allah akamchukuwa Jesus kumpleka mbinguni.
Kiufupu Qur an imesimulia karne zilizopita ambazo kwa kiasi kikubwa zilitawaliwa na historia ya mitumei iliotoka kwenye jamii ya kiyahudi
Hizi Ni porojo za Quran ambayo imeandikwa na hao hao Wakatoliki
 
Na shida inayowatesa nyie vikanisa vinavyozuka na kupotea ni umoja wa kanisa katoliki,mkijitazama mmeshindwa kuwa kitu kimoja basi mnalazimisha na ukatoliki usambalatike.
Unaijua HUKUMU YA YULE KAHABA MKUU (Roman Catholic)?


[https://cdn][https://www]

AMINI MITUME WAKE

SURA YA BIBLIA YA KILA SIKU



Ufunuo wa Yohana 17



1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;
2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.
3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.
4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.
5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.
 
Ukitaka kuujua Uisilama soma hii kitabu jinsi Uisilamu Uinsilamu ulivyoansishwa Islam org
 
Hahaha. Wasabato bana. Vip mkuu hiv wale waliokuwa airport wanataka kusafiri bure wameishia wapi? Nakumbuka uongo wa the great dissappointment
Mbona unashindwa kujibu mada unawalaumu wasabato ,wanahusika Nini hapa?


Dr Rivera Mjesuit Ni msabato?
 
Mbona unashindwa kujibu mada unawalaumu wasabato ,wanahusika Nini hapa?


Dr Rivera Mjesuit Ni msabato?
Hana hoja ni conspiracy za mitandaoni. Labda mi nimuulize swali. Yeye anatumia biblia ipi. Hii ya wakatoliki yenye vitabu 72
Au ya orthodox n Coptic yenye vitabu 84
Au hii ya waprotestant yenye vitabu 66. Atupe jibu na kwanini anaamini hilo jibu ndio biblia sahihi.
 
Ona waislamu wanawake huvaa kama masister
Wanafunga kwaresma au ramadhani
Wote wanavaa kanzu na uvumba upo
Wote wanapigania dini zao na kufa kama mashahidi
Wote wanaotumia tasibihi
Wote wanaombea wafu waende peponi
Wote dini zao zinamchanganyiko na upagani
Pole sana
 
Ukitaka kuujua Uisilama soma hii kitabu jinsi Uisilamu Uinsilamu ulivyoansishwa Islam org
HAKUNA MWARABU HATA MMOJA ALIYEWAHI KUWA MWISLAMU KABLA YA MUHAMMAD USHAHID HUU HAPA


QURAN 34:44

QURAN 43:21~22,

QURAN 51:52,

QURAN 3:164 NA QURAN 62:2
 
Back
Top Bottom