Ukweli kuhusu kauli ya Papa huu hapa, vyombo vya habari vinapotosha

Ukweli kuhusu kauli ya Papa huu hapa, vyombo vya habari vinapotosha

Sio kweli kabla ya baraka unatubu na kua msafi,baraka sio sacramenti
Hapa umekuwa mwongo, Ukristo maana yake ni matendo safi, unapoingia tu kwenye nyumba ya MUNGU unatubu kuanguka kwako na kuomba utakaso kabla ya mengine yote. Hata KRISTO mwenyewe alisamehe kwanza ndipo akabariki. Hakuna sehemu ambapo alibarikiwa mtu mwenye nia ya kuendelea na dhambi iliyomfanya kuwa mchafu. Kuanguka kupo na ndio maana tukaletewa toba na neema.

Wewe unachosema ni tafauti kabisa na dhana nzima ya kuwa mkristo.
 
Binafsi maelezo yako nimeyaelewa vizuri,suala la kuyakubali ni jambo lingine,ila kuelewa nimeyaelewa.

Kama nimeelewa vizuri ni kwamba papa ameruhusu mashoga wabarikiwe sio kwa sababu ya ushoga wao bali ni kwa sababu ya kuwa wao ni binadamu kama binadamu wengine.

Kwa maana kama ambavyo mwizi akienda kanisani anataka baraka kwa jambo lake ambalo halihusiani na wizi basi padre atambariki na baraka hizo haziendi kwenye kubariki wizi wake huo.

nimeelewa vyema kwamba ushoga ni dhambi kama zilivyo dhambi zingine za wizi,uzinifu,ufisadi n.k

Hivyo kama mwizi,mzinifu,fisadi,mla rushwa huwa wanaenda kanisani kupata baraka tena sio baraka za kubariki dhambi hizo basi na shoga nae pia anayo haki hiyo kupata baraka hizo ambazo hazihusiani na kubariki ushoga.

HOja hizi zina make sense kwa kila mtu lakini nadhani wapo watu ambao watachukuahii kama fimbo ya kuchapa watu fulani.

Baadhi yetu wa dini isiyokuwa ukristo tutatumia fimbo hii kuwachapia wakristo.

Na hata wasioamini dini watatukia hii kama fimbo kuwachapa watu wa dini.

NA pengine hata wakristo ambao sio wa dhehebu hilo watatumia hiyo kama fimbo kuwachapa watu wa dhehebu hili.
Wadhambi kama wezi, wazinzi, waongo, wauaji, makahaba n.k hubarikiwa ili waachane na matendo yao maovu na waenende katika kufanya mema.

Je mashoga wakisha barikiwa wata tengana na kuachana na mapenzi yao ya jinsia moja?

Kwanza hao wadhambi wengine kulingana na kanisa katoliki hupewa baraka pale ambapo hutubu makosa yao kwa kuya ungama kuyajutia na kukiri kuachana nayo.

Je mashoga wakisha barikiwa wata achana?

Au wata endelea kupokea baraka kwenye hali yao hiyo hiyo ya ushoga siku zote?

Lengo kuu na dhumuni la kuwabariki ni nini haswa?

Waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja huku wakipata baraka?
 
Hakuna mkamilifu ndo maana kuna toba. Unatubu ili neema ya Kristo iwe juu yako. Kutubu maana yake kujutia dhambi uliyoitenda. Unachofanya hapa ni kuhalalisha dhambi ya kulawitiana sababu hakuna mkamilifu. Sasa toba ni ya kazi gani kama unaweza kwenda mbele za MUNGU ukiwa mlawiti, mwizi, mzinzi na ukabarikiwa

Swali: Je kanisa limeelekeza walawaiti kutubia dhambi yao ya ulawiti kabla ya kuja mbele za MUNGU kubarikiwa?

Usijibu kisiasa.
Kabla sijakujibu,unajua maana ya sacrament ya kitubio?,unajua baraka inatolewaje?unachanganya vitu viwili kwa pamoja ,baraka haitolewi kwa mtu pekee ,bali ata vitu,umejenga nyumba ,ukaomba ibarikiwe,je hiyo nyumba ikibarikiwa ,uliyejenga utaulizwa umejenga kwa pesa Halali au ya wizi?
Unapeleka mbegu kanisani,zinaombewa kabla ya kwenda kupanda.je padri unataka apeleleze shamba ni lako au lina migogoro
 
Wadhambi kama wezi, wazinzi, waongo, wauaji, makahaba n.k hubarikiwa ili waachane na matendo yao maovu na waenende katika kufanya mema.

Je mashoga wakisha barikiwa wata tengana na kuachana na mapenzi yao ya jinsia moja?

Kwanza hao wadhambi wengine kulingana na kanisa katoliki hupewa baraka pale ambapo hutubu makosa yao kwa kuya ungama kuyajutia na kukiri kuachana nayo.

Je mashoga wakisha barikiwa wata achana?

Au wata endelea kupokea baraka kwenye hali yao hiyo hiyo ya ushoga siku zote?

Lengo kuu na dhumuni la kuwabariki ni nini haswa?

Waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja huku wakipata baraka?
Mkuu, hapa ni kujiongeza tu sababu kinachoendelea kipo wazi haihitaji nguvu kuelewa.

Kaburi hata ulirembe vipi juu ndani kuna maiti. Hapa kinachofanywa na kondoo wa bwana ni kuliremba kaburi ila ukifungua maiti ipo.

Njia sahihi ni kumpinga papa maana ni binadamu sio kuremba remba kinachoripotiwa kuwa kimetoka kwake.
 
Kabla sijakujibu,unajua maana ya sacrament ya kitubio?,unajua baraka inatolewaje?unachanganya vitu viwili kwa pamoja ,baraka haitolewi kwa mtu pekee ,bali ata vitu,umejenga nyumba ,ukaomba ibarikiwe,je hiyo nyumba ikibarikiwa ,uliyejenga utaulizwa umejenga kwa pesa Halali au ya wizi?
Unapeleka mbegu kanisani,zinaombewa kabla ya kwenda kupanda.je padri unataka apeleleze shamba ni lako au lina migogoro
Kulikuwa na sababu gani ya kutolea tamko ushoga kama dhambi hazina uhusiano na kutolewa baraka? Kanisa lina nia ya kurahisisha ushoga kwenye akili za waumini. Ni suala la muda tu.
 
Hiki ndio maana yake, ila watu wanapotosha kwa makusudi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Wapenzi wa jinsia moja wanapewa baraka kwa lengo gani haswa?

Waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja?

Wakati wanapewa baraka watahimizwa waachane au waendelee na mapenzi yao ya jinsia moja?

Wadhambi wengine katika kanisa katoliki hupewa baraka pale ambapo hutubu makosa yao kwa kuyaungama, kuyajutia na kukiri kuachana nayo.

Je mashoga wakisha barikiwa wata tengana?

Au wata endelea kupokea baraka ilhali ushoga ni dhambi kwa mujibu wa ukatoliki?
 
Baraka sio sacrament ,hiyo ni kwa watu wote,ata jambazi akiiba akienda kwa padri,akiomba baraka atapewa,,umeona gari ukaenda kanisani kulibariki,litabarikiwa,kwa hiyo jambazi aliyeiba,padri hati angalia atambariki Kama wengine ,bila kuuliza dhambi yake,kupitia baraka atapata neema za Mungu,Kama ana dhambi atajirudi kwenye toba.
Je mashoga wakisha barikiwa itawafanya waachane na watengane?

Kwamba baraka itawasaidia wasiendelee kuwa wapenzi wa jinsia moja?
 
Ww mwenyewe kwa bandiko hili umeshahalalisha ushoga ndani ya kanisa
Kristo.

Kuhusu wapenzi wa jinsia Moja Papa anasemaje?

Ukweli uko hapa!

"Fiducia suplicans". Ni barua alioandika papa juu ya maana ya Baraka katika uchungaji.

"On the pastoral meaning of blessings"

Katika barua hiyo papa aliandika kujibu maswali ambayo watu wanauliza Sana Kanisa sasa, juu ya msimamo wa kanisa juu ya wapenzi wa jinsia Moja na ndoa za Jinsia Moja. Maana Kila papa katika kipindi chake analazimika kujibu maswali ya kijamii yanayogusa Imani.

Fiducia suplicans n kilatini maanake " n kwamba tusimamie wapi? "On the pastoral meaning of blessing"


Makuhani tusimamie wapi katika maana ya kichungaji ya kutoa Baraka? Papa hazungumzii katika hii barua habari za ndoa ya jinsia Moja, bali Kwa ujumla barua yote anaelezea hasa maana ya Baraka na mapadre watoeje Baraka katika kipindi hiki chenye mchanganyiko wa watu "wema" wenye bidii na pia kipindi chenye maovu yake mchanganyiko.


ANGALIZO
Kwenye hiyo barua papa anatatua changamoto Moja kwamba je mtu huyo mdhambi anaeishi ndoa ya jinsia Moja je anahaki yakubarikiwa?

Hapo hashughuliki hasa na swali eti kubariki ndoa ya jinsia Moja, ameweka wazi kabisa kuwa haifai na haiwezekani.

Kwenye barua anajibu swali kwamba je mtu Mmoja anastahili kubarikiwa? Haisemi abarikiwe kwasabab yeye ni shoga hapana ila kwasabab yeye n mtu.

Kwa maana nyingine je Kanisa liwatenge watu ambao ni mashoga?

Swali hilo limetokea wapi? Huku ulaya nduguzanguni watu hupenda mtu Mmoja Mmoja anakwenda Kwa Padre anamwambia Padre nibariki. Sisi pia huwa mtu unakuta anasafiri anakwenda Kwa Padre, "baba naomba Baraka nasafiri". Padre anambariki. Mtu anapeleka mbegu za kupanda baba naomba Baraka, mwanafunzi anakwenda Kwa Padre baba nimeleta vifaa vyangu vya shule naomba baraka, Padre anabariki.

Watu wakamuuliza papa je mtu mdhambi akimwambia Padre baba naomba Baraka je padre akatae? Aseme Baraka ni Kwa ajili ya watu wema?

Papa akasema Kama akija mtu yoyote akaomba kubarikiwa basi Padre anaweza kumbariki hata kama anaishi dhambi zake kama huyo wa jinsia Moja. Wasibaguliwe kwamba Baraka n ya watu fulan wema

Lakini wasibarikiwe wakiwa wawili kama vile ni wanandoa! Ametoa tahadhari kubwa kuzuia fikra zozote kwamba tunawabariki kama vile Kanisa linaruhusu maisha yao hapana! Ndugu zanguni Baraka sio sakramenti. Ndio maana Padre baada ya Misa anabariki wote hatengi wema zaidi na wakosefu Zaidi. Ila sakramenti sio Kila Mmoja anaruhusiwa. Watu wa ndoa ya jinsia Moja wao pia wamejifungia masakramenti.

Kwa waraka huo Padre anaweza kubariki watu wakiwa katika kundi kama kanisani au kikundi Cha Sala au wasafiri, pia mtu Mmoja Mmoja Padre anaweza kumbariki bila kumuuliza hali yake ya dhambi, hata kama anajua huyo mtu anaishi hali yake ya dhambi Padre ambariki tu. Kwanini maana kupitia Neema za Mungu mtu huweza kubadilishwa pia.

Luka 15:1. Siku moja, watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakaanza kunungunika: “Mtazameni mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi, na tena anakula nao.....

Ngoja tuone baadhi ya nukuu kwenye barua hiyo.

Maelezo hayo yapo kwenye barua hiyo "Fiducia suplicans". Sura ya III

"Blessings of Couples in Irregular Situations and of Couples of the same sex". Kiswahili. Baraka Kwa wanaoishi wawili/kama mume na mke katika mazingira yasiyokuwa ya kiutaratib (utaratib kulingana na Kanisa) na ya watu wanaoishi pamoja wa jinsia Moja kama vile ni mume na mke.


Sasa Kwa kichwa hicho Cha habari anasemea sio tu watu wa jinsia Moja bali hata wale ambao hawapo katika ndoa inayotambuliwa kikanisa. Mfano wachumba wasibariki ndoa, wengine wameolewa mitara wote wanahusishwa kwenye kundi hilo. Papa anasema wote Padre anaweza kumbariki tu mtu huyo mkosefu akija Padre ambariki lakin anatoa mkazo isifanyike Baraka rasmi kama vile n sakramenti. Wala wasijisikie kuwa wanahalalishwa hapana.

Nanakuu hiyo barua
No 31. Uwezekano wa kutoa Baraka Kwa watu kama hao......

32. "Indeed the grace of God works in the lives of those who do not claim to be righteous but who acknowledge themselves humbly as sinners, like everyone else.".

"Hakika Neema ya Mungu hufanya kazi katika maisha ya wale ambao hawajidai kuwa wenye haki, lakini wanaojikubali Kwa unyenyekevu wakosefu "

Papa anasema Baraka hiyo ni Neema ambayo Mungu ataitumia kuwaongoa lakini Neema ya Mungu hufanya kazi ndani ya mtu anaekubali Kwa unyenyekev kuwa yeye ni mdhambi. Watu hao wakubali kuwa wao n wakosefu wampe Mungu ushirikiano.
No 33 "This is a blessing that, although not included in any liturgical rite........, "Hii ni baraka ambayo, ingawa haijajumuishwa katika ibada yoyote ya kiliturujia,

No 36 In this sense, it is essential to grasp the Holy Father’s concern that these non-ritualized blessings "kwa maana hii ni muhimu kutambua mtazamo wa baba mtakatifu kwamba hizi baraka ambazo sio rasmi kama zingine za kwenye ibada........ hapa anaonyesha ni za kawaida sio rasmi kama za kwenye liturjia

39. In any case, precisely to avoid any form of confusion or scandal, when the prayer of blessing is requested by a couple in an irregular situation, even though it is expressed outside the rites prescribed by the liturgical books, this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

39. .......this blessing should never be imparted in concurrence with the ceremonies of a civil union, and not even in connection with them. Nor can it be performed with any clothing, gestures, or words that are proper to a wedding

Baraka hizi zisitolewe Kwa namna yoyote inayoendana na muunganiko kama ule wa ndoa na Wala hata Kwa mfanano zisiendane, Wala zisifanywe kama Kwa mavaz ya ndoa ama ishara au maneno ya kubariki ndoa.

Civil union n msamiati wanaotumia zaidi Kwa watu wa jinsia moja anasema Baraka hizo zisielekee Wala Kwa namna yoyote inayoashiria kitu kama hicho.

Anaependa uisome mwenyewe kwenye mtandao "Fiducia suplicans" kuanzia no 31. Itajitokeza Kwa kiitalianoa lakin mwanzo wa document kushoto kabisa wameorodhesha lugha ya kuchagua bofya " Testo in lingua linglese" itabadilika kuwa Kwa kiingereza.
 
Kanisa limekuwa VUGUVUGU.

Ukienda mbele za MUNGU kuomba mibaraka unapaswa kutubu na kuwa msafi sio umeacha mwanaume mwenzako nyumbani na utarudi ukamlawiti halafu unaenda kuomba mibaraka. Tubu kwanza ukiwa na nia ya kuachana na hayo matendo kisha nenda kwa MUNGU kuomba mibaraka.

Hata mwizi, mzinzi ni hivyo hivyo. Unatubu kwanza kwa dhati. Ukianguka tena unatubu ila moyoni mwako una nia ya kuiacha hiyo dhambi.

ukishatubu inamaana umekuwa msafi na pale unatambuliwa kama binadamu na baraka ni haki yako. Kama si sahihi sasa kuna tofauti gani ya mkristo na walawiti, wezi, wazinzi wasio na roho ya MUNGU ndani yao?
Umefafanua vyema.
 
Icho ndio kilichokatazwa ,ata papa kapinga kwa watu wawili hao kwenda kuomba baraka ,kisha wapewe,imekatazwa kabisa kwa herufi kubwa,lakini akienda mmoja akiomba baraka,padri hatomuuliza kama yeye ni gasho au lah,atapatiwa baraka,apate neema ,Kama kujirudi aweze kujirudi
Hilo si linafanyika kila siku, kwani lilikua linahitaji tamko kwani?
 
Waumini wa kanisa katoliki kazi mnayo, mnataka kufafanua kitu ambacho kimsingi kukifafanua inabidi kujizima data, tunawaangalia tu, ila papa kasema, nyie akina nani mnatolea ufafanuzi tamko la papa?
 
Je mashoga wakisha barikiwa itawafanya waachane na watengane?

Kwamba baraka itawasaidia wasiendelee kuwa wapenzi wa jinsia moja?
Swali lako ilitakiwa liwe je mtu akipata baraka,anapata Nini rohoni?mtu yeyote anapata neema ya Mungu,neema ya Mungu ukiipata unapatwa na hofu ya Mungu,na kuzikataa dhambi,uikshakua na ukaribu Mungu ,roho mtakatifu anakuongoza muda wote,kwa hiyo ata Kama ni shoga,huenda akajirudi ,na kupiga magoti kwa Mungu,yeye anasema japokua dhambi zenu ni nyekundu Kama damu,nitazibadili zitakua nyeuoe kama theluji
 
Hilo si linafanyika kila siku, kwani lilikua linahitaji tamko kwani?
Kabisa. Sasa sijui kwanini kuna watu hawaoni kinachoendelea? Kinachoendelea ni maandalizi ya kuupokea ushoga kwa vizazi vijavyo ndani ya imani. Na hili linafanywa na mashoga wazungu.

Kwenye filamu wamepokelewa, kwenye michezo wamepokelewa, kwenye siasa wamepokelewa kilichobaki ni kanisani na msikitini. Hapa wakiweza basi zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
 
Swali lako ilitakiwa liwe je mtu akipata baraka,anapata Nini rohoni?mtu yeyote anapata neema ya Mungu,neema ya Mungu ukiipata unapatwa na hofu ya Mungu,na kuzikataa dhambi,uikshakua na ukaribu Mungu ,roho mtakatifu anakuongoza muda wote,kwa hiyo ata Kama ni shoga,huenda akajirudi ,na kupiga magoti kwa Mungu,yeye anasema japokua dhambi zenu ni nyekundu Kama damu,nitazibadili zitakua nyeuoe kama theluji
Aisee. Mkuu, we unaona kila kitu kipo sawa?
 
Hii taarifa haipo BBC tu na kama inarudiwa rudiwa sababu ni kanisa kuruhusu hilo. Nia ni kulifanya lizoeleke masikioni mwa kondoo.

Mbona ni rahisi tu. Ni sentensi ndogo tu kutoka kwa papa inamaliza hili suala.

PAPA: Kanisa lilaani ushoga na lisijiusishe kwa namna yoyote na wenye matendo hayo isipokuwa kwa wanaotaka kuyaacha.
Hivi akili zako zina akili? Unawajuwa Illuminati? Nani anacontrol media na world market?

Vitu vingine vipo nje ya level yako ya ufahamu.

Mimi nikitaka habari za Simba nitaingia kwenye App ya Simba siwezi kwenda kuzitafuta kwenye App ya Yanga.

Habari za Papa zitafute Vatican Wana media zao.
 
Labda sio mkatoliki,kwa hiyo kuelewa kuhusu baraka inavyotolewa haujui,baraka ata kila baada ya misa hutolewa pia kwa waumini wote waliopo kanisani,bila kuangalia dhambi za mtu,ingekua inabagua dhambi basi ni wazi baraka zisingetolewa ,maana Hakuna mkamilifu
Baraka hizo hutolewa baada ya ungamo la dhambi ambalo hufanyika wakati ibada ina anza.

Kwenye ibada za wakatoliki kuna kipengele cha "Kukiri dhambi" ambapo Padri husema tukiri makosa yetu, waumini hukiri kwa kusema...[emoji116]

"Namuungamia Mungu mwenyezi nanyi ndugu zangu kwani nimekosa mno kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana ndio maana namuomba Maria mwenye heri bikira daima malaika na watakatifu wote nanyi ndugu zangu niombeeni kwa bwana Mungu wetu"

Kisha padri husema...[emoji116]

" Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu atufikishe kwenye uzima wa milele"

Waumini huitika Amina.

Hapo baraka imetolewa kusafisha matendo yao maovu kulingana na mafundisho yenu ya ukatoliki kwamba kama mtu alikuwa mwizi ame ungama na ataacha wizi wake, kama mtu alikuwa muongo ame ungama na ataacha uongo wake, Kama mtu alikuwa mzinzi ataacha uzinzi wake na kukiri kuachana na matendo hayo.

Sasa je wapenzi wa jinsia moja (mashoga) wakisha barikiwa na kuungama wata achana na kutengana?

Kwamba hawata endelea tena kuwa wapenzi wa jinsia moja?

Au wata endelea kubarikiwa hivyo hivyo kila siku, Huku wakiendelea kufukuana mitaro?
 
Back
Top Bottom